Kituo cha traffic Chemba mkoa wa Dodoma hamtendi haki

gambakuffu

JF-Expert Member
Jul 2, 2010
422
411
Kuna huyo askari anaitwa remigius mwenye no. H. 4760 PC Remigius . Basi huyu bwana mnamo tarehe 11.07.2020 majira ya saa4 asubuhi nikielekea jijini Dodoma kikazi, nikiwa mwendo mdogo wa spidi chini ya 50km kwenye eneo lao la kizuizi kama ilivyo kawaida nikasimamishwa tena kibabe yule askari akaniomba leseni nikampa then akaniamuru nishuke nione mwendo wangu.

Wakati namfuata kuelekea kwenye gari yao akanionyesha simu inayoonyesha nina mwendo wa spidi 83km kitu ambacho sikuafiki na hapo hapo akawa ametoa invoice yenye kumbukumbu ya malipo ya tsh. 30k niilipe ndani ya siku7.

Wa kweli ni masikitiko yangu kueleza hili kwa mwendo ule wa spidi chini ya 50 nikapigwa faini hadi watu niliokua nimeambatana nao wakashangazwa na mmoja kueleza sasa tunatishwa kupita eneo hili la chemba kwani hata kwa mwendo kasi kidogo wakiamua kukupiga faini utapigwa tu.

Jeshi letu la polisi naomba mmulike huu uwozo kwani kwa kitendo nilichofanyiwa hakikuwa cha kiuungwana kabisa.

Nawasilisha!
 
Kachague sahihi 25-10-2020!

Uvccm, uwt, wazazi na polisi ni ndugu.

Shana eqn
A=B.....i)
B=C......ii)
A=C......iii)
A=B=C....iv)

Ambapo A ni polisi
B ni serikali na C ni ccm.


Amehamishiwa CCP moshi kuwafundisha hesabu za aina hii watumishi wajao na waliopo wa polisi hapo unategemea nini?
 
Back
Top Bottom