costercoster
Member
- Dec 2, 2018
- 66
- 46
Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya ndani naomba uingilie kwa jicho la tatu matendo maovu yanayofanywa na polisi wa nyakanazi , hawa polisi hawafuati maadili ya kazi ya jeshi la polisi, kwani kwa sisi wakazi wa huku wakigundua tu una pesa either umeuza shamba au mifugo basi jiandae kukamatwa na kubambikizwa kesi zsizo na miguu, unatakiwa utoe chochote ili uachiwe. Sio hayo tu hata wale watumiao usafiri wa magari yao binafsi wamekua wakisumbuliwa sana na hawa askari. mara nyingi tunashuhudia askari hawa wakiwandikia wenye magari makosa hata saba nakutakiwa kuwalipa cash huku wakitishia kumpiga mtu risasi. Wao wanajisifu kwamba kwa maeneo haya ya nyakanazi mtu hawezi kupita na gari lake bila kuacha angalau elfu shirini kwao kwani wao ndio watawala wa eneo hilo na wanaweza kufanya lolote na kwa yeyote.
Kwamfano juzi kati hapa walikua wakijisifu kwamba wamepokea risasi 200 zinatakiwa zitumike na kuisha ndani ya wiki 1, je huu si unyanyasaji kwa raia wasio na hatia? yani ili upoite nyakanazi ni lazima ulipe kwao kodi isiyopungua elfu 20? Polisi hawa baadala ya kua msaada kwa sisi wananchi wao wamekua maadui namba moja kwa uhai wetu na mali zetu. Juzi kati wamemtoza jamaa mmoja faini ya sh 120,000 moja wapo ya makosa ikiwa ni mlio mbaya wa gari.
Tunaomba utusaidie, labda kwa kuwarudisha tena CCP labda hawakuelewa vizuri majukumu yao.