Kituo cha Mafuta cha TOTAL Mlimani City na unyanyasaji/udhalilishaji kwa wananchi

Yaani haiingii akilini eti unaruhusu watu wenye magari wanapaki maeneo yale yale wanajaza mafuta ila kupita kwa miguu eti ni hatari nadhani CRDB na Absa na NBC kama sikosei wanazo ATM zao hapo wanapozuia watu wasipite waingilie kati kuna mtu anawahujumu na hana taarifa za msingi. Juzi nusra nilianzishe na masecurity coz haina mantiki me sijui nani anahusika wapi na nini nachojua hapo sehemu kuna huduma za kifedha na fuel filling
ATM zipo kwa wanunua mafuta si wakimbiza upepo na infantria (wasichana wa hall 3 walikuwa wanatuita infantria wakati tunajaribu bingo)
 
Habari kwenu Wadau!

Sheli ya Total ambayo ipo eneo la Mlimani City imekuwa na utaratibu wa hovyo wa kuwanyanyasa Watembea kwa Miguu kwa muda mrefu!

Utaratibu huo umeanza tangu kipindi cha sherehe za Christmas mpaka leo hii! Ukiwa unatembea kwa Miguu, unaendesha baiskeli au ukiwa Mazoezini hauruhusiwi kupita kwenye eneo la Sheli hiyo!

Wapo Walinzi wa Kampuni (nitaweka Jina soon) wenye Silaha ambao wamejipanga pande zote za Sheli kuzuia watembea kwa Miguu! Utaratibu huo haukuwepo miaka yote! Iweje leo unakuja utaratibu wa ovyo kiasi hiki?

Utaratibu huo wa hovyo umepelekea watu kutengeneza njia mbadala ya kuzunguka Sheli kitendo ambao kimeendeleea kuharibu Mazingira kwa Wananchi kujitengenezea njia zao wenyewe!

Tunataka kujuzwa kama utaratibu huu ni mpya kwa Sheli za Mkoa wa Dar es Salaam na kwingineko Nchini au ni Ubabe wa wenyefedha? Itakumbukwa Sheli hii bado ipo kwenye hifadhi ya Barabara na hivyo kuzuia Service Road inayotokea Mlimani City kuja roundabout ya kuelekea kwa Mama Kamche to Calabash! Kitendo cha kuzuia muendelezo wa service road ndio maana watu wamekuwa wakipita chini ya Paa la Sheli hiyo!

Lakini kwenye Sheli kuna huduma za Kibenki, Supermarket na Biashara ya Vilainishi vya Magari nk.

Tunaomba Mamlaka zinazohusika, ikiwemo Ofisi ya RC Kunenge kuingilia kati unyanyasaji na uzalilishaji unaoendelea kwenye Sheli ya Total pale Mlimani City!

Goodluck Mshana
Mimi sio mjuzi wa mambo ya kiusalama
Ila nijuavyo sio salama kufanya kituo cha mafuta njia ya watemebea kwa miguu
Mfano: Hutakiwa hata gari likiweka mafuta lizimwe kabisa, driver asiwashe sigara wala asivute sigara akiwa kituoni, na pia kuepuka vitu vyote vinavyo tumia nishati ikiwemo simu nk
Sasa sijui utawezaje kuwasimamia watembea kwa miguu wajue taratibu za kituo cha mfuta. Sio vizuri kusema kuwa hutujaona kituo kikalipuka kwa sababu ya sigara lakini ni vizuri kuchukua tahadhari kuepuka kuja kutafuta mchawi...
ILA ni kweli kuwa ipo haja ya mamlaka husika kuwatengenezea njia mbadala ya watembea kwa miguu na baiskeli ambayo ni salama kwao na kwa kituo
 
Kituo kimekula eneo la service road, na kublock wanaotumia barabara kwa miguu sasa hapo kosa ni la kwao kwanini ujenge kituo kwenye service road, na hyo service road wameblock vipi Raia wanaoenda mwenge lufungila na kwingine watumie njia ipi. Wengi mnalaumu mleta nada bila kujua kosa ni la kituo ku block njia ya kutokea hyo service road.
Ni sawa usemayo. Basi habari ziwafikie manispaa sijui tanroads. Kama kweli wamechukua eneo la service road hatua zitachukuliwa. Ila Kama eneo ni la kwao wanayo haki ya kukataza mtu kupita.
.
.
Najiuliza tu wanajiamini nini kuchukua eneo la service road na wahusika wakae kimya. Kuna kitu hakipo sawa kama ni hivyo.
 
Na wakishughulikia hyo Hali ni lazima hcho kituo kiondolewe hapo Mana Kiko njiani kabisa, siku zote tumepita hapo why now wa block, maana uwepo wa hicho kituo kisingewepo iwepo njia rahisi ya kuingilia mlimani city na watu wenye magari yanayoenda chuo kikuu, na makongo.
Yes napaelewa ingawa sijapita miaka mingi kwa miguu. Basi huu uzi utawashtua wahusika.
 
Nilipokuta utaratibu huu kipuuzi Mwezi December nikahoji! Majibu yao yalikuwa ni hayo hayo tu. ”Kuna tukio limetokea” simple as such yani!
Bro wanazuia watu kupita ndani ya eneo lao au nje ya eneo?
Kama ni nje ya eneo wanakosea.
Kama ni ndani ya eneo lao karibu na pump za mafuta unakosea kulalamika
 
Niwashukuru Wadau na JF kwa ujumla! Baada ya uzi huu naona utaratibu umerudi kama zamani! Jana nimepita kufwatilia na kukuta Watembea kwa Miguu wakipita eneo hilo bila kizuizi! Wale Walinzi wa kampuni wenye silaha nao wamepunguzwa kwa asilimia kubwa! Leo tena nitapita kufwatilia utekelezaji!
 
Niwashukuru Wadau na JF kwa ujumla! Baada ya uzi huu naona utaratibu umerudi kama zamani! Jana nimepita kufwatilia na kukuta Watembea kwa Miguu wakipita eneo hilo bila kizuizi! Wale Walinzi wa kampuni wenye silaha nao wamepunguzwa kwa asilimia kubwa! Leo tena nitapita kufwatilia utekelezaji!
Safi Sana aisee waache kutesa raia
 
Tena mi naona kawastay sana kwa mda mrefu, ingekua Mimi tokea naanza kuwekeza hapo ningeshaifunga hiyo njia
 
Back
Top Bottom