Uzi Maalum wa maswali na masuala mbalimbali yahusuyo Kodi, ushuru na masuala mengine yanayowahusu TRA

Wadau habarini za mida hii,
Leo nilikuwa kwenye mchakato wa kulipia mapato ya biashara yangu TRA ila nilipofika kwenye ofisi zao nikaambiwa napaswa kuhamisha TIN yangu kutoka nilipoikatia (mkoa tofauti na nilipo) kuleta mkoa nilipo ndipo niweze kulipia mapato...Naombeni uzoefu kwa yeyote ambaye alishafanya hii, utaratibu wa kuhamisha ukoje?....

Asanteni
Hili silifahamu kwa kweli,ngoja na mimi nisubirie majibu ya wanaojua...
 
Mimi nilishakuwaga na tatizo kama ilo. Mpaka leo sijajua hatima yangu, mwaka 2012 nilifungua TIN ya bihashara pale Mwanza. Lakini mlolongo wa kupata Leseni ya bihashara ikawa ngumu nenda uku rudi uku mpaka nikashindwa kupata Leseni ya bihashara. Sasa mwaka 2013 nimerudi zangu home DSM. Wakati zoezi la kubadilisha wote wenye Leseni za gari kuwa na izi za electronics wakasema uwe na TIN Number. Kwenda Samora pale Posta (DSM) wakaniambia tayari TIN Number unayo nikachukua Leseni ya Gari. Mwaka 2016 nikabadilisha leseni kama kawaida lakini mwisho wa mwaka 2016 likaja zoezi la kufanya update za TIN Number zote apa Tanzania. Sasa naenda pale Kimara Baruti kufanya update ya Tin number, wakaniambia faili lako la Tin number lipo Mwanza wakanipa namba piga uku na uko sikufanikiwa kuamisha ilo faili la Tin number kutoka Mwanza kuja Mkoa wa Ubungo wa ktk TIN Number. Sasa apo uwa najiuliza TRA, uwa ufanyaji wao upoje kwa mikoa ya TRA. Maana ilishindukana mpaka leo sijapata muda wa kurudi pale Mwanza Tanzania kwa ajili ya kuamishia pale Kimara DSM. Na wenyewe walikuwa wananiambia piga simu lakini hakukua na response yoyote kutoka TRA Mwanza mpaka wakawa wanasema nisafiri mpak Mwanza kwa ajili ya kubadilisha iyo Tin number kuileta apo Kimara DSM

Sent from my Infinix X5515 using JamiiForums mobile app
Hapo cha kufanya ni kuandika barua kwa meneja wa tra/mkoa au wilaya sehemu ulipofungulia hilo file, ziwe mbili hata ukimpata mtu anayekwenda mwanza unampatiaa anazipeleka zitagongwa mhuri moja itabakia huko nyingine watampatia, unakuwa umemaliza baada kama ya wiki moja file litahamishiwasehemu uliyoitaka. Lakini kwa simu utakesha.
 
Wadau habarini za mida hii,
Leo nilikuwa kwenye mchakato wa kulipia mapato ya biashara yangu TRA ila nilipofika kwenye ofisi zao nikaambiwa napaswa kuhamisha TIN yangu kutoka nilipoikatia (mkoa tofauti na nilipo) kuleta mkoa nilipo ndipo niweze kulipia mapato...Naombeni uzoefu kwa yeyote ambaye alishafanya hii, utaratibu wa kuhamisha ukoje?....

Asanteni
Ni kwamba ulikua na biashara huo mkpa ukahamisha ama ulikata tin kwa matumizi ya leseni etc?
 
Nshafanya hiyo, pigia mtu simu alieko mkoa unaohama aende pale TRA mkoa utokao akaongee nao physically. Wakati huo TRA wa huku wanatuma mail yenye scanned letter uliyoandika kwa meneja wa kule. Anachoenda kufanya huyo jamaa ni kupush hao wa mkoani wahamishe details zako kuja mkoa unaotaka.
 
Nimeenda TRA tena leo asubuhi wataalamu kuufanyia kazi ushauri wenu na nikapewa barua ya kuhamisha TIN kutoka mkoa niliokuwepo, mimeijaza nikaambiwa by jumatatu utaratibu utakuwa umekamilika; Nimeandika namba yangu pale wamesema nitapewa ujumbe. Nitawapa mrejesho wiki ijayo....

Ila nimeambiwa siwezi kulipia mapato mpaka TIN itakapohamishwa... Hapo kwenye ushauri namba 2 mtaalamu nipe maelezo zaidi tafadhali nifahamu channel ya kupitia
2. Malipo
Nakushauri nenda tawi jingine na waombe moja kwa moja statement ya malipo ya kodi unayotaka kulipa, utasaidiwa. Leta mrejesho km utaenda Tax Service Centre nyingine
 
Wadau habarini za mida hii,
Leo nilikuwa kwenye mchakato wa kulipia mapato ya biashara yangu TRA ila nilipofika kwenye ofisi zao nikaambiwa napaswa kuhamisha TIN yangu kutoka nilipoikatia (mkoa tofauti na nilipo) kuleta mkoa nilipo ndipo niweze kulipia mapato...Naombeni uzoefu kwa yeyote ambaye alishafanya hii, utaratibu wa kuhamisha ukoje?....

Asanteni
Yani umeshindwa kuwaambia wakusaidie kukupa muongozo unakuja kutusumbua huku. Aya Njoo nikueelekeze ila utafidia muda wangu
 
Wadau habarini za mida hii,
Leo nilikuwa kwenye mchakato wa kulipia mapato ya biashara yangu TRA ila nilipofika kwenye ofisi zao nikaambiwa napaswa kuhamisha TIN yangu kutoka nilipoikatia (mkoa tofauti na nilipo) kuleta mkoa nilipo ndipo niweze kulipia mapato...Naombeni uzoefu kwa yeyote ambaye alishafanya hii, utaratibu wa kuhamisha ukoje?....

Asanteni

Hao TRA ndo wenye hilo jukumu la kuhamisha. Ulipaswa hayo maswali uwaulize ulipokuwa nao ofinini. Sasa unatuuliza huku ili tukakusaidiekuuuliza au?
Humu pia kuna watu wa TRA yawezekana wakakusaidia
 
Wadau nimeleta mrejesho..Ukifika TRA kuna barua ya maombi ya kihamisha TIN ambayo unaijaza, inasainiwa na Manager kisha inatumwa kwa Manager wa tawi ulikotoka ili TIN yako ihamishwe....ni swala la muda mfupi tu TIN inakuwa imehamishwa na unaweza kufanya malipo...Asante sana wadau kwa ushauri wenu na maoni yenu.
 
Asalaam Alyekum,
Tumsifu Yesu Kristo wanajamvi,

Leo nimeona bora nawajulishe wanajamvi pia TRA kupitia hizi kurasa zetu pendwa za JamiiForums ya kwamba kituo cha mafuta cha Lake oil kilichopo Buguruni Malapa jiji Dar-es-Salaam hawatoi risiti pindi unapoenda kununua mafuta, kisingizio chao kikubwa ni kuwa machine zimeharibika.

Sasa taarifa kwenu TRA, wamulikeni hawa Lake Oil maana miezi miwili nyuma nililiona hili nikaona sio kesi ila wiki jana nikapewa tena taarifa hiyo hiyo kuwa machine za risiti ni mbovu.

TRA, ni kweli mnakaa miezi miwili bila kwenda kutengeneza zile machine za risiti?

Usiku mwema wapendwa.
 
Kuna sehemu nyingi sana huwa hawatoi risiti ila ww umeona ni hicho kituo tu. na hiyo inaonyesha ni kiasi gani unachuki na hicho kituo cha mafuta.
 
Mkuu, bilashaka ulienda na gari na ndio ukakutana na dhahma hiyo.
Basi naomba nimupongeze tu kwamiliki chuma huko Daslam, hayo ya riaiti minaona ni umbeya tu chunga usije ukasutwa....
 
Back
Top Bottom