Kituo cha mabasi ya mkoani Mbezi Louis chakamilika, kufunguliwa rasmi 25/02/2021, Ubungo kufungwa rasmi Jumatano

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,840
141,765
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Kunenge amesema Jumatano hii ndio siku ya mwisho kwa kituo cha Ubungo kutumika na kuanzia Alhamis kituo kipya cha Mbezi kitaanza kutumika.

Naye kamanda Mambosasa amesema wapiga debe wa Ubungo hawatakiwi kuonekana stendi mpya ya Mbezi na kwamba stendi hiyo haitakuwa na wapiga debe.

Maendeleo hayana vyama

--

mbezi.jpg

RC Kunenge amesema hatua hiyo imekuja baada ya kukamilika kwa miundombinu yote muhimu ikiwemo majengo, maegesho, barabara na ofisi za kutoa huduma.

Aidha, RC Kunenge amesema tayari Serikali imekutana na wadau wote husika ikiwemo chama Cha Wamiliki wa Mabasi TABOA na wote wamejiridhisha kuwa kituo kimekamilika na kipo katika hali nzuri ya kutoa huduma hivyo wapo tayari kutoa huduma.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Sporah Liana amesema ifikapo siku ya Jumanne watafanya kikao na Wafanyabiashara wote watakaokuwa wakitoa huduma ndani ya jengo na siku ya Jumatano watakutana na Wamachinga, Baba lishe na Mama lishe kwa ajili ya kuwekeana mikakati ya biashara.

Naye Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema Jeshi la Polisi limejipanga kuhakikisha abiria wote wanaosafiri au kuingia kituoni hapo hawapati usumbufu wa aina yoyote.
 
Maisha ya DAR yanazidi kuwa magumu nakumbuka kuna jamaa aliishi zaidi ya miaka 5 ndani ya stand ya ubungo kila kitu anamaliza ndani ya stand
Huyo mwambie tu ahamie Kigamboni au Kimbiji akalime matikiti au mihogo halafu aje auze Jijini wakati wa mavuno!

Hadi kufikia 2025, naamini kila Mtanzania atakuwa ameshafanikiwa kuisoma namba ya huyu mzee wetu. Wafanyakazi walau tumeanza kuzoea zoea kwa sasa.
 
Back
Top Bottom