Kituo cha Mabasi Magufuli bei ya pango hadi Tsh. 1,200,000/= kwa siku

Midas Touch

Senior Member
Jan 23, 2008
178
182
Sasa kama mjasiriamali amepewa fremu ili auze maji na soda ndani ya kituo ghorofani kwa kodi (rent) ya Tsh. 36,028,200/= kwa mwezi sawa na Tsh. 1,201,000/= kwa siku uhalisia uko wapi! Machinga wanauza maji na soda hizo hizo ndani na nje ya kituo hicho hicho kwa rent ya kitambulisho chake cha Tsh, 20,000/= kwa mwaka sawa na Tsh. 55 kwa siku.

Attached ni mchanganuo wa bei ya pango kama ulivyoidhinishwa na DCC kabla haijavunjwa na Hayati Rais Magufuli mwezi February 2021 wakati wa uzinduzi.

Data hizo ni kutoka waraka ulioidhinishwa na aliyekuwa Mkurugenzi wa DCC uliosomeka "“Majina ya walioshinda zabuni ya upangishaji maeneo ya biashara na utoaji huduma mbalimbali katika Kituo Kikuu cha Mabasi Mbezi Luis 2020”

Mipango mingi ya ajabu ya aina hii kupitia TAMISEMI imeshindwa kama vile: Bus stand ya Dodoma, Machinga Coplex ya pale Ilala, Mwal Nyerere Airport Terminal 3, machinjio ya Vingunguti nk.

Ummy Mwalimu take action please, hapo hakuna biashara.
Data hizo ni kutoka andiko G. Kombe.

MIRACULOUS RENTS AT MAGUFULI BUS TERMINAL.jpg
 
Back
Top Bottom