Kituo cha Mabasi cha Magufuli kimegeuka soko kwa sababu ya usimamizi mbaya

Hakuna haja ya kuwagusa kama ina maana ya kuwaondoa
Ila ipo haja ya kutengeneza mfumo mzuri wa wao kuwepo kwa manufaa ya wote
Sasa huo mfumo wa wao kuwepo maeneo hayo utauweka vipi?mfano mzuri mbagala zile sehemu zote za daladala kupakizia abiria wamezichuka wao, hakuna parking tena!!service road zote wamechukua, yaani watu sasa wanalazimika kupita barabara ya magari kitu ambacho ni hatari.ina maana kuendelea kuwepo wao ni kero kwa wengine!!pale mbagala kuna ujenzi wa mwendo kasi vibanda vyao vingi vimetolewa, heeee bwana juzi amevamia barabara ya mtaa wa kwenda BIASI, wameufunga wote hakuna tena cha gari wala pikipiki kutumia njia hiyo!!kwa sasa sheria za halimashauri zitumike tu kwani zipo ila ziliwekwa pembeni kwa sifa za mtu mmoja tu.wewe umeshawahi kuona wapi sehemu kama POSTA(DSM)Mtu anatumia jiko la kuni/pumba kupikia ?huo moshi balaa!!ukimgusa tu" eeee baba yetu rais wa wanyonge wanao tumeanza kunyanyaswa huku".
Mfano mwingine jana nimeona pale stendi mpya ya magufuri mtu ana cartons 100 za maji ya kunywa ameziba eneo kubwa la wasafiri, kuambiwa yeye hana sifa za kuitwa machinga kilio kwa mwenda zake!!
 
ubungo bus terminal inatakiwa wasafiri tu ndio waruhusiwe kuingia ndani ya stendi kama wanavyofanya airport .
Jengo limejengwa zuri na kubwa kuleta taswira ya kisasa na kimataifa basi uendeshaji uwe wa kimataifa na kisasa.
Bila udhibiti kutakuwa na wezi Wengi.
Wamachinga watengewe sehemu maalumu kuuza bidhaa zao pembeni ya stendi bila kuingilia wasafiri ndani ya stendi na kuleta usumbufu
 
Hakika inashangaza na Kusikitisha kabisa. SERIKALI inashindwa kuweka na kusimamia Utaratibu Mzuri wa Uendeshaji wa Kituo cha Mabasi cha Magufuli kwa kumwaachia Wafanyabiashara kutandaza na kupanga bidhaa zao kwenye Corridor na sehemu za kupumzika Abiria.

Hivi kusimamia hilo mpaka aje Mzungu? Mbona Viongozi wetu wazembe sana kwenye mambo ya Msingi?

Tunawaomba Wahusika wawaondoe wafanya Biashara wanaopanga na kutandaza bidhaa zao kinyume na Utaratibu.
Leute pics basi tuzione.
 
Usimamizi unakuja na kuwaondoa hao wafanyabiashara wadogo,ama wawapange wakae humo kiutaratibu
Nakuambia huko mbeleni kituo hicho kitakuwa kama d@mpo

Ova
TRUE na yote hiyo kwasababu ya kufanya mambo kwa pupa na bila kuwa na standards!! Kwa fedha zilizotumika hapo tungeweza pata soko zuri na bora kuliko hilo lisilo na mpangilio mzuri!
Nashawishika kuamini JIWE alijua hana muda merfu duniani hivyo alikuwa anafanya mambo yake haraka haraka ndio maana hakuwa anajari ubora wa miundombinu yake aliojenga!! He compromised quality for quantity!!!
 
Kumbukeni, hii nchi ni masikini sana
Tuwaacheni wamachinga watafute riziki, kadri uchumi wa nchi utakavyokua na maisha ya watu kuboreka basi changes nyingi zitafanyika
 
Usemacho ni kweli kabisa! Huwezi kuamini kama ni stendi bali ni soko sawa na Kariakoo!
 
Kama wanaosimamia wameshindwa kazi wapewe usaidizi. Tatizo sio wafanyabiashara wadogowadogo.
Tatizo ni wafanyabiashara na sio wasimamizi...

Mfano wewe hapo ukikojoa au ku poop eneo si rasmi kwa shughuli hiyo, utailaumu mamlaka za usafi kuktokukuelekeza mahali pa kumaliza shughuli zako??

Ustaarabu waafrika hatuna na ndio msingi wa vyanzo vya kuonekana tu mafukara wa fikra na matendo...
 
Mfumo mzuri ni ndani ya stand ya basi kuwe na mabasi na ofisi za tiketi za mabasi ndo maana ikaitwa stand ya mabasi. Huduma nyingine ziwe nje ya stand.

Sasa na wachungaji nao wakitaka kuja hapo kutafutwe utaratibu? Mama ntilie? Shoe shinners? Watu wa network marketing? Woote watafutiwe utaratibu?

Huwezi tengeneza kitanda kisha ukatafuta utaratibu mzuri wa kulala na mabeseni yaliyojaa maji, kuna siku utalowa. Wawaache tu ili hatua zikichukuliwa ieleweke.

Kuna mkoa nipo watu wamefunga barabara ya lami kwa nyanya na vitunguu.
Nimelike mara tatu.
 
Hiki kama kituo cha basi kinatushinda tutaweza kusimamia ndege tunazoendelea kununua zilete faida!???
 
Tatizo la Marehemu Jiwe alitaka kutengeza 'cult' (kama kadini kake mwenyewe chenye wafuasi wanaomuona masiha). Na ili kulitimiza hili akatarget wale wa kipato cha chini sana na kujitwika utetezi hewa.

Kutimiza dhamira yake alikwenda kinyume na mfumo wa kistaarabu ili tu aonekane anajali sana, alifanikiwa kupata wa kumuabudu lakini athari yake inakera wengi zaidi.

Leo hii kupita kariakoo ni tabu maana kumejaa wamachinga kila sehemu, ukija ilala boma barabara imekuwa soko la nyanya na vitunguu.

Na hiyo stendi ya mabilioni ishakuwa kama tandika tayari, yote sababu ya kiumbe mmoja tu aliyetaka kuwa mungu na leo hayupo tena.
Chukua katoni ya image wine nalipa
 
Kila nchi kuna kumwaga na sehemu kama hizo! Hata London! Wewe ukiona hapa kufai huko chagua sehemu za posta posta, Agakhan, oysterbay na kwingineko penye watu wachache. Watanzania walio wengi maisha ya miksanyiko ndiyo wanapenda!
Acha ujinga wewe London hakuna ushamba kama huuu
 
Tatizo la Marehemu Jiwe alitaka kutengeza 'cult' (kama kadini kake mwenyewe chenye wafuasi wanaomuona masiha). Na ili kulitimiza hili akatarget wale wa kipato cha chini sana na kujitwika utetezi hewa.

Kutimiza dhamira yake alikwenda kinyume na mfumo wa kistaarabu ili tu aonekane anajali sana, alifanikiwa kupata wa kumuabudu lakini athari yake inakera wengi zaidi.

Leo hii kupita kariakoo ni tabu maana kumejaa wamachinga kila sehemu, ukija ilala boma barabara imekuwa soko la nyanya na vitunguu.

Na hiyo stendi ya mabilioni ishakuwa kama tandika tayari, yote sababu ya kiumbe mmoja tu aliyetaka kuwa mungu na leo hayupo tena.
Brain zero ndiyo atashindwa kuwapanga hao watu.
Wapangeni tu. Kila mtu anahaki ya kufanya biashara hapa stand.
Huo ndiyo ustaarabu.
Kama kondakta wa daladala anaweza kupanga abiria wake na wote wakafika salama iweje ninyi wasomi iwashinde?
Use your brain.
 
Umeandika sanaaaaaaa kwanini hawa wamachinga wanakuumiza hivi?

Waache wenzio wapate rizki sababu nao wana mahitaji kama yako japo hawana kazi sawa na yako
Yaani wamachinga wamekua sio watanzania tena. Yaani ni ubaguzi wa hali ya juu kwa hawa vijana wamachinga. Badala ya watu walete hoja nzuri ya kuwasaidia ndio kwanza wao wanaona kero hawavijana kuwepo hapo na kutafuta rizki zao. Ni kweli ndani ya hao vijana kuna vibaka lakini ingekua vizuri tuwe na roho za huruma. Hata kama leo tuna weza kula na kushiba na kulala mahali pazuri lakini ya kesho tusisahau, mungu ni kubwa na mwenye uwezo wa kutupiga chini mara mmoja na sisi tukahangaika kama hao vijana.
Ushauri ni kwa serikali tu. Wajitahidi kuleta mipango mizuri ya maeneo ya biashara humo humo ndani ya stendi. Watengenezewe mazingira mazuri na wapewe ikiwezekana kwa bei nafuu na Pia wote watakao fanya biashara hapo wapewe elimi kwanza kabla hawajaanza biashara zao.
 
Hakuna kituo kibaya kama cha Magufuli, mara mia turudi ubungo.
Hakuna sehemu ya kula..siku nimewahi asubuhi natafuta sehemu ninywe chai sikupata, wamejaa mama ntilie walioweka vyakula kwenye ndoo.
Kwenda toilet...vyoo vimejaa tumepanga foleni. Nilikereka sana
Nani ataweka mgahawa sehemu ya mamantilieni wengi na bei iwe hiyo hiyo wakati mwenye mgahawa atahitajika kulipa Kodi na gharama zingine, twende kwenye toilet hiyo stendi imejengwa kwaajili ya abilia na toilet kwaajili ya abilia sasa machinga wengi maana yake ndo watatumia hizo toilet muda wote na abilia watajiju wenyewe kweli haki ya abilia imeminywa kwenye hiyo stendi na pa kusemea hakuna, labda abilia waende bungeni kudai haki zao wabunge wawatete kwenye serikali.
 
Back
Top Bottom