Kituo cha Mabasi cha Magufuli kimegeuka soko kwa sababu ya usimamizi mbaya

andoza

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
2,050
2,000
Hawa machinga mimi nashauri waondolewe hata katika ya miji mikubwa wao watafutiwe sehemu nyingine. Machinga wamekuwa kero kubwa
Mkuu,Wapelekwe wapi?au wafukuzwe unamaanisha?Hii issue ya wamachinga ni issue ya kisiasa.Ushauri wangu ni Rahisi Tu.Badala ya vile vitambulisho vya hayati uwekwe mfumo maalum wa kuwatambua pamoja na maeneo waliyopo,Aina ya bidhaa etc ili kuhakikisha kwamba hawaharibu mpangilio wa mji.
 

edwayne

JF-Expert Member
Apr 5, 2013
5,392
2,000
Wawepo mdani na nje lakini kwa utaratibu
Je katika ramani walitengewa.. Yani sometimes huwa tuna idea za ajabu. Eti wakitengewa sehemu huwa wanasema wateja hawaendi.. Hivi huwa najiuliza kuna mtu anagoma kwenda hospitali kisa ipo mbali.. Binadamu lazima afuate huduma popote ilipo kama anahihitaji.. Machinga wanatakiwa wakae sehemu moja magengeni huko sio barabarani.. Yani hatutemebi kwa raha
 

mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
10,904
2,000
Kusema Wamachinga waachiwe kwenda kutandaza bidhaa za Airport ni kuwaumiza?

Ndio ni kuwaumiza sababu wao wanafuata soko. Huko airport kuna watu wengi kama bus stand? Na hao watu wanahitaji huduma zao???

Ulishawahi kujiuliza kwanini projects kama machinga complex zilifeli??

Ukibarikiwa kuvaa viatu usiwakebehi waliokosa sababu Mungu anaweza kukunyang'anya miguu
 

atlas copco

JF-Expert Member
Jun 15, 2015
4,675
2,000
Nilipita pale wiki2 zilizopita nikaambiwa vyakula haviruhusiwi kuingizwa kituoni kwa sasa ila vinapatikana upande wa pili wa kituo
Pia niliambiwa ujenzi unaendelea... na ukikamilika kila kitu kitakua sawa
Uliambiwa kama nan labda,mbona unajikweza sana?,mwendazake zama zake zimeshapita hizi ni zama zingine ukae ukilijua hilo
 

Demi

JF-Expert Member
Nov 22, 2016
24,030
2,000
Je katika ramani walitengewa.. Yani sometimes huwa tuna idea za ajabu. Eti wakitengewa sehemu huwa wanasema wateja hawaendi.. Hivi huwa najiuliza kuna mtu anagoma kwenda hospitali kisa ipo mbali.. Binadamu lazima afuate huduma popote ilipo kama anahihitaji.. Machinga wanatakiwa wakae sehemu moja magengeni huko sio barabarani.. Yani hatutemebi kwa raha
Watengewe sehemu nyingi nyingi, masokoni na karibu na vituo vikubwa vya daladala/mabasi. Barabarani waondoke kwa kweli
 

edwayne

JF-Expert Member
Apr 5, 2013
5,392
2,000
Watengewe sehemu nyingi nyingi, masokoni na karibu na vituo vikubwa vya daladala/mabasi. Barabarani waondoke kwa kweli
Kipindi magufuli anaingia waliwaondoa wote njiani sijui kilimkuta nini akawarudisha.. That was bad move.. Mambo yanatakiwa yafuate mipango iliyopangwa.. Ukiacha holela holela ndio kujenga jiko na choo sehemu moja
 

Rodwell mTZ

JF-Expert Member
Nov 16, 2012
371
500
Umeandika sanaaaaaaa kwanini hawa wamachinga wanakuumiza hivi?

Waache wenzio wapate rizki sababu nao wana mahitaji kama yako japo hawana kazi sawa na yako
Ni kweli Kila mtu anahaki ya kupata riziki,lakini kuwe na mpangilio maalumu mfano stendi kama hiyo imefunguliwa wajengewe soko jirani wapate riziki zao huko,kama walivyojenga pale Simu 200 Sinza.
 

mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
54,361
2,000
Hata mimi nilitaka kuitaja zambia sababu ndio nchi walau tunaendana kiuchumi, Lungu katuzidi sana, stendi yake biashara zote ziko kwenye fremu kubwa na vifremu vidogo, hakuna bidhaa iliyomwagwa chini wala vimeza meza. Highway yao ya kutokea huku kwetu hakuna banda la turubai utaliona linapepea pembeni mwa barabara, na sehemu za biashara zote highway ziko mita kadhaa kutoka barabarani. Angalau ndicho nilichokiona kwa mwaka huo 2018 nilipokua hapo sijui kwa sasa.

Huku mambo yaliyofanyika kwa miaka mitano mfululizo sidhani kama kuna kiongozi atayekuja kuweza kupambana na machinga wanaopanga biashara zao hadi mabarabarani. Itabidi kutumia mabavu kuwaondoa which sio sahihi au kuwaomba sana na kuwanyeyekea wahame, kitu ambacho nacho hawatatii.
Ona bus terminal ilivyokuwa ndani kuko kimpangilio,biashara na shuguli zinafanyika
Vizuri...
Hapa kwetu mambo ni ovyo kabisa
Na hali hii vibaka wakabaji washaingia mule

Ova
 

May Day

JF-Expert Member
May 18, 2018
4,089
2,000
Kama wanaosimamia wameshindwa kazi wapewe usaidizi. Tatizo sio wafanyabiashara wadogowadogo.
Mimi niliwahi kusema hata kwenye hili la hawa kina Mama wanaopanga bidhaa barabarani...kuna Watu hawafanyi kazi zao walizoajiriwa kwazo.

Binaadamu wakati mwingine ni kama Ng'ombe, lazima awepo mmoja wa kuwaongoza wakae kwenye mstari.

Ndio maana wenye akili zao walikuja na wazo la kuweka taa za kuongozea Magari, la sivyo kila kukicha Magari yangekuwa yanarundikana kwenye njia panda na kukwamia hapo maana kila mmoja anataka apite yeye kwanza.

Hao waliopewa dhamana za mipango miji wanakula mishahara miaka nenda rudi na bado tu hawapati ufumbuzi wa kuwapanga Machinga na kina Mama wauza mboga.
 

nguvu

JF-Expert Member
Jun 13, 2013
10,674
2,000
Hakuna haja ya kuwagusa kama ina maana ya kuwaondoa
Ila ipo haja ya kutengeneza mfumo mzuri wa wao kuwepo kwa manufaa ya wote
Kwa idadi yao ni lazima uwapunguze tu maana wanafanyia biashara hata sehemu sio sahihi sasa ukiwapa eneo hawatatosha labda uwapangie siku za kuja na hapo bado watamkumbuka JPM
 

mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
54,361
2,000
Down town posta hapo
Come on.........yaani mji mzima vibanda vibanda

Ova
20210416_125044.jpg
 

atlas copco

JF-Expert Member
Jun 15, 2015
4,675
2,000
Mnafiki wewe unaetamani kuona wamachinga wakitaabika badala ya kutoa maoni ya kuboresha


Niliambiwa kama mama D, una swali lingine??
Unayejikweza ni wewe unayetamani kuwauwa machinga na familia zao.... mfyuuu
Ndio maneno umebaki nayo hayo,kama ni maoni member wengine wameshatoa huko juu lkn bado unayapinga,ndio maana kuna jamaa amekuuliza ww upo upande hueleweki na mm ndio nakwambia tena acha unafiki,jiwe hasafishikiiiii
 

mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
10,904
2,000
Ni kweli Kila mtu anahaki ya kupata riziki,lakini kuwe na mpangilio maalumu mfano stendi kama hiyo imefunguliwa wajengewe soko jirani wapate riziki zao huko,kama walivyojenga pale Simu 200 Sinza.

Hayo ndio maneno
Bado ujenzi unaendelea na watakapomaliza nadhani changamoto nyingi zitaisha
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom