Kituo cha kusaidia waathirika wa mafuriko chafungwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kituo cha kusaidia waathirika wa mafuriko chafungwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Saint Ivuga, Dec 23, 2011.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Dec 23, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,252
  Likes Received: 19,383
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Kituo cha kusaidia waathirika wa mafuriko chafungwa
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Thursday, 22 December 2011 20:05 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0digg

  Keneth Goliama
  KITUO cha kupokelea watu walioathirika na mafuriko katika Wilaya ya Temeke, Dar es Salaam kimefungwa baada ya wathirika wa maafa ya Mvua kutojitokeza.Kituo hicho ambacho kipo Shule ya Kibasila, Wilaya ya Temeke, mkoani Dar es Salaam baada ya waathirika kutokwenda katika kituo hicho tangu jana.

  Kwa mujibu wa Mlinzi wa Shule ya Kibasila Mandina Buku, alisema tangu kituo hicho kiandaliwe kwa ajili ya kupokea waathirika wa mafuriko, hakuna hata mtu mmoja aliyefika pale kupata huduma.
  Alisema wasimamizi wasaidizi wa maafa, walikaa muda mrefu, lakini watu hao hawakufika kupata msaada.

  Katika hatua nyingine, Muuguzi wa zamu katika Hospitali ya Temeke, Shamimu Ronda alisema mtu mmoja tu, alifika katika hospitali hiyo baada ya kuangukiwa na ukuta katika maeneo ya Mbagala.

  Ronda alisema hakuna majeruhi zaidi waliofikia katika hospitali ya Temeke tangu jana baada ya kutokea mafuriko makubwa jijini Dar es Salaam kuanzia juzi.

  Uwanja wa wa Ndege
  Uwanja wa Ndege wa Mwlimu Julius Nyerere ulionekana kuendelea kutoa huduma ya usafiri licha ya maji kujaa katika uwanja huo.Mwananchi ilifika katika uwanja huo na kuona wasafiri wakiendelea na shughuli zao kama kawaida na wengine ndai ya uwanja na kutoka.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Dec 23, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,252
  Likes Received: 19,383
  Trophy Points: 280
  wwaathirika wako wapi? au wako bussy kutafuta vitu vilivyobebwa na maji
   
 3. Baba Imani

  Baba Imani Member

  #3
  Dec 23, 2011
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 79
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Nadhani siku hizi watu Wa dar hawaogopi maji kama zamani!
   
 4. MwafrikaHalisi

  MwafrikaHalisi JF-Expert Member

  #4
  Dec 23, 2011
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 1,746
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Wilaya ya Temeke haijaathirika kama Kinondoni na Ilala. Ni matatizo madogo madogo tu. Everything is undercontrol huku
   
Loading...