Kituo Cha Kimataifa Cha Mikutano Arusha AICC Chaingiza Mapato Zaidi Ya Shilingi Bilioni 11

mamayoyo1

JF-Expert Member
Jul 25, 2018
1,011
1,019


Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imewasilisha hotuba ya mpango na Makadirio ya Bajeti ya wizara kwa mwaka wa fedha 2019/2020 , bungeni jijini Dodoma ambapo kituo cha kimataifa cha mikutano Arusha AICC kimeendelea kuwa kitovu cha diplomasia ya mikutano hapa nchini na kuchangia katika uchumi wa taifa.

Akiwasilisha hotuba ya Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mei 30, 2019 bungeni jijini Dodoma ,Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof.Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi amesema hadi kufikia Mwezi April ,2019 kituo cha mikutano ya kimataifa cha Arusha AICC Kimeingiza mapato ya Sh.Bil.11,Mil.428 laki 8 ,68 elfu na mia 998.

Kati ya Fedha hizo,Sh.Bilioni 2 ,Mil.76,laki 7 ,71 elfu na 27[2,076,771,027] zimetokana na huduma za mikutano 342 iliyofanyika katika kituo cha AICC ambapo mikutano 32 kati ya hiyo ni ya kimataifa na 310 ni ya kitaifa.

Prof.Kabudi amefafanua kuwa ,Sh.Bilioni 2,Milioni 244 , laki 5,na 32 elfu na mia 662 [2,244,532,662] zimetokana na huduma za mikutano katika kituo cha mikutano cha kimataifa cha Julius Nyerere ,Sh.Bil.3,mil 556,laki 5 na 96 elfu na mia 819[3,556,596,819] na Sh.bil.3,mil.550,laki 9,na 68 na mia 490 [3,550,968,490]ni kutokana na huduma za hospitali.

Aidha,Prof.Kabudi amesema ,kuhusu usimamizi wa kiuchumi Ripoti inaonesha kuwa Tanzania imeendelea kutekeleza mipango ya Maendeleo ikiwianishwa na mpango wa Maendeleo Endelevu wa Umoja wa Mataifa [2030] na Agenda 2063 ya Umoja wa Afrika,Mpango wa Miaka mitano[FYDP II 2016/17-2020/21] unaweka mkazo katika mageuzi ya viwanda na maendeleo ya Rasilimali watu kama njia sahihi ya kuifikisha nchi katika uchumi wa kati ifikapo 2025.

Hata hivyo,Successor Strategy ya Zanzibar 2016/17-2020/21 imepatia ufumbuzi maeneo mengi yaliyokuwa yameainishwa kama mapungufu kama mpango kazi wa APRM.

Katika hatua,nyingine Prof.Kabudi katika hotuba yake amesema chuo cha Diplomasia kimeendelea kutoa mafunzo na kufanya tafiti katika masuala ya Diplomasia ,uhusiano wa kimataifa na usuluhishi wa Migogoro na kulinda Amani.

Chuo cha Diplomasia kinatoa Mafunzo ya Lugha saba [7] za kigeni ambazo ni kiarabu,kichina,Kifaransa,kiingereza,Kireno,Kihispania,na Kikorea na hadi sasa kinafanya Mazungumzo na Serikali ya Kirusi ili kufadhili mafunzo ya Lugha ya Kirusi na Mwaka 2018/2019 kilidahili Jumla ya wanafunzi 1,029 katika ngazi za cheti,Stashahada,Shahada na Shahada ya Uzamili.
 
Back
Top Bottom