Kituo cha bajaji Majumbasita- Dar: Kinachosubiriwa ni maafa!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kituo cha bajaji Majumbasita- Dar: Kinachosubiriwa ni maafa!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sisimizi, Jan 21, 2010.

 1. Sisimizi

  Sisimizi JF-Expert Member

  #1
  Jan 21, 2010
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 490
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Ukiwa unaelekea Gongolamboto (Barabara ya Kisarawe/Pugu), utakutana na njia panda ya kwenda Segerea/Kinyerezi na ndiyo hiyohiyo inayoelekea kituo cha POLICE staki shari - UKONGA.

  Upande mmoja wa barabara inayokwenda kituo cha POLICE stakishari na Segerea/ Kinyerezi umegeuzwa na kuwa kituo cha pikipiki aina ya Bajaji. Kwahiyo upitaji wa magari na waenda kwa mguu nao umekuwa ni wa shida mno. Magari hayawezi kupishana vyema nk.
  Kila mara ukipita eneo hilo utakuta magari yamekwaruzana wakati wa kupishana kwa sababu Bajaji zimeegeshwa upande mmoja wa barabara!!

  Sasa ninajiuliza hivi:

  Mamlaka zinazohusika, zinasubiri mpaka vifo vitokee katika eneo hili ndipo waondoe kituo cha Bajaji ndani ya eneo la barabara?

  Pili, askari wa usalama barabarani wanaokuwa wakiongoza magari pale njia panda, kwani hawaoni tatizo hili lililopo pale?

  Ni mamlaka ipi ambayo imeamua kuanzisha kituo cha Bajai katikati ya barabara???

  Hivi viongozi wa eneo hilo la Ukonga - majumbasita, wanaishi kweli wakiwa na uelewa thabiti wa shughuli zao?

  Hivi kweli, viongozi wamekosa eneo maalumu la kuegesha bajai mpaka wajekutenga eneo katikati ya barabara?

  Ndugu zangu, kwa nini tushindwe kuthibiti hata utokeaji wa maafa yaliyo ndani ya uwezo wetu kuyazuia yasitufike?
   
 2. Dreamliner

  Dreamliner JF-Expert Member

  #2
  Jan 21, 2010
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 2,034
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Hawa jamaa wa Bajaji, wameambiwa wahamie mbele kidogo kabla ya kuvuka reli. Lkn kutokana na njaa zao na njaa za maaskari, wanawaachia wanafanya kazi zao na askari wanapita hapo hapo na hakuna anayesema au kuchukua hatua yoyote... Mheshimiwa KOMBE where are you?
   
 3. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #3
  Jan 21, 2010
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Mkuu ukiweza kuweka picha hapa ya hicho kituo itakuwa safi sana.
   
 4. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #4
  Jan 21, 2010
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Mkuu ukiweza kuweka picha hapa ya hicho kituo itakuwa safi sana.
   
 5. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #5
  Jan 21, 2010
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Tuwatafutie sehemu tu jamani ila wasifukuzwe kwani wamekuwa nyenzo ya muhimu sana kwenye maisha ya watanzania wa daraja la chini
   
Loading...