Kituo cha anga za mbali kimetengenezwa kwa ushirikiano wa mataifa mbalimbali

Mzawa_G

JF-Expert Member
Feb 27, 2014
504
1,070
Marekani na Urusi walikubaliana kuanza ujenzi wa kituo hicho katika miaka ya 98 ambapo baada ya kuanza ujenzi mataifa mengine yalijitokeza kuomba kuungana katika ujenzi wa kituo hicho kwa pamoja

Mataifa kama Marekani , Urusi , Canada Umoja wa ulaya ndio nchi zinazounda uwanachama wa wamiliki wa kituo hicho cha anga za mbali huku Urusi na Marekan ndio nchi pekee zinazomiliki sehemu kubwa katika kituo hicho ,

Kituo hicho kilipelekwa anga za mbali kwa vipande vipande ambavyo viliungwa kwa pamoja na kuunda chombo hicho kikubwa sana angani , Marekani akiwa na vipande 8 , Urusi akiwa na vipande 6 na vipande 3 vikiwa vya mataifa mengine yaliyobaki huku Canada akimiliki mkono wa ufanyaji kazi zote za nje ya kituo hich

Malengo makubwa ya uwepo wa kituo hicho yalikuwa ni kuweka uwepo wa kiumbe mwanadamu katika eneo lengine kabisa mbali na uso wa dunia yetu na sababu nyengine ni kufanya chunguzi mbalimbali za maisha ya mwanadamu nje ya dunia yetu ili kutambua ni vipi mwili wake kwa ujumla utakavyoweza kumudu hali tofauti na iliyopo juu ya uso wa dunia yetu na sababu ya mwisho kabisa ni ufanyaji chunguzi za anga

Idadi kubwa ya wanaanga mbalimbali wameshaweza kufika na kuishi katika kituo hicho tangu kituo hicho kiwepo huko anga za mbali na huku mwanaanga aliyeweza kukaa siku nyingi zaidi kituoni humo ni yule mwanaanga Peggy Whitson aliyekaa siku 665 kituoni humo

Kituo hicho kina upana wa kiwanja cha mpira wa miguu ambayo upana wake ni mita 100 na kina jumla ya uzito wa tani laki 4 na elfu 20 huku chombo kikiwa na mifumo mbalimbali ya computer 50 zenye kuratibu masuala mbalimbali ya huduma za mawasiliano na mambo mengine ya kimipango ndani ya kituo ,

Kituo kinazunguka dunia kwa umbali wa kilomita zisizopungua 400 kutokea usawa wa bahari , ambapo kinaweza kuzunguka dunia kwa zaidi ya mara 16 kwa muda wa masaa 24 huku wanaanga wakiweza kuona mawio na machweo kwa mara 16 kwa kila kipindi

Chombo hichi kinazunguka dunia kwa kasi ya 7.2 km/s ambapo hii ni kasi ya mzunguko wa orbit ya kwanza ( orbital velocity speed) kama chombo kitafikia kasi hii basi kitaweza kubako hapo na kuzunguka dunia bila ya tatizo kwa muda wote huo , sasa hapa tukubaliane kituo hichi hakitumii nishati kuzunguka dunia bali wakati wa kupelekwa kwake kilipelekwa kwa kasi kubwa hivyo huweza kuendelea kutumia kasi hiyo hiyo katika kuzunguka dunia na kama kasi ikipungua kuna utaratibu wake wa uongezaji kasi ili irudi kama ilivyokuwa , ili kuepusha kituo kuweza kuanguka chini , kumbuka kituo kitakapoacha kuzunguka basi kitarudi chini kama maembe yanavyoanguka

Weightlessness ndio kitu wanachokutana nacho wanaanga ndani ya kituo hicho sio kama eneo libakopita kituo hakuna kani ya uvutano hapana , ni kwamba katika eneo hilo kani ya uvutani ipo ila kwa uchache ambapo huuliwa na kasi ya chombo hicho na kufanya kama vyote vilivyopo ndani vionekane kama vipo kwenye eneo lenye kani 0 ya uvutano , kumbe ni kitendo cha kila kitu kupoteza uzito wake

#Gerald
#Elimu_ya_anga_tanzania
FB_IMG_1665178690067.jpg
 

pilato93

JF-Expert Member
Jun 28, 2014
6,022
5,911
Kinatumia nishati gani kujiendesha na kuendesha mifumo yake yote ya umeme?
 

vibesen xxx

JF-Expert Member
Jul 23, 2022
2,432
4,264
Maisha ndani ya chombo yakoje?

Mtu anatokaje ndani ya chombo na kurudi duniani? Na akarudi na nn?

Wanaenda uko wanaenda na nn na wanaingiaje?

Chombo kikiharika kwa nje wanatengenezaje?
 

Tsh

JF-Expert Member
Aug 26, 2021
4,750
9,547
Hii ni moja ya uthibitisho kuwa Urusi na USA wanaweza kuwa kitu kimoja pale kunapotokea mazingira ya kuwafanya hivyo. CHAWA hili si la kulisahau wakati wa kuvaa uzalendo.
 
2 Reactions
Reply
Top Bottom