Kwa baadhi yetu tunaomfahamu vizuri mama Nyoni muda mrefu, anavyosemwa katika jf si sahihi ni kupakwa matope na wasiomtakia mema. Huyu mama ni kiongozi mzuri, anayejua analolifanya na kupenda wafanyakazi waliochini yake. Ana msimamo thabiti kwa jambo analoamini yuko sahihi na huwa na vielelezo kwa kila jambo analofanya. Kwa mtu yeyote ambaye anajua Menejimenti, a professional manager anaweza kuongoza sehemu yoyote ya kazi si lazima awe na taaluma husika. Wale wanaofikiri madaktari ndio wanaweza tu kuwa viongozi wa wizara ya afya ni wazi hawajui menejimenti ni nini. Mama Nyoni ni meneja, ndio maana kama Makatibu wakuu wengine na hata mawaziri si lazima awe wa taaluma husika ya wizara. Ni vyema kumhukumu mtu kwa matendo yake na haki yake apewe.