Kituko gani kimeshangaza tangu serikali ya awamu ya tano iingie madarakani?

geraldincredible

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
2,036
7,220
Kituko gani cha kisiasa kimeshangaza tangu serikali ya awamu ya tano iingie madarakani.Mimi ni kitendo cha mkuu wa nchi kuwaambia wananchi wafyatuane watoto wengi halafu kesho yake waziri wa afya akaja kukanusha anasema mkuu alikuwa anatania.Hakika nilishangaa sana vipi kwenu wakuu
 
Mwakiwembe kutamka watu wasioane hadi wawe na vyeti vya kuzaliwa, siku ya pili Zisonje akakanusha. Zisonje alinikata stimu sana maana nilishapata sababu ya kutooa. Ningekuwa nasingizia cheti cha kuzaliwa
 
Hapa kazi tu, lakini mapato ya serikali yanapungua. Ni dhahiri awamu hii ni ya ovyo, haina 3d thinking.
 
Kituko gani cha kisiasa kimeshangaza tangu serikali ya awamu ya tano iingie madarakani.Mimi ni kitendo cha mkuu wa nchi kuwaambia wananchi wafyatuane watoto wengi halafu kesho yake waziri wa afya akaja kukanusha anasema mkuu alikuwa anatania.Hakika nilishangaa sana vipi kwenu wakuu

Rais aruhusiwi kutania?? Je akiwa wa mbuzi mtafurahi? Tafakari ni muhimu bila kutenda
 
Tembelea tanzania ujionee NYUMBU wakipiga stori wakiwa wana kunywa maji kwenye makundi. Endeleeni kujadili KAULI za mkuu hata zile za utani MNATAKA mzijadili Duh

Hakuna sababu ya kua mkali nina uhakika ww ndio nyumbu tofauti yenu jinsia..shwain
 
Mwakiwembe kutamka watu wasioane hadi wawe na vyeti vya kuzaliwa, siku ya pili Zisonje akakanusha. Zisonje alinikata stimu sana maana nilishapata sababu ya kutooa. Ningekuwa nasingizia cheti cha kuzaliwa

Haaaahaaaaa mie demu wangu alivyosikia aliwai kwenye RITA kunitafutia cheti cha kuzaliwa
 
Kituko gani cha kisiasa kimeshangaza tangu serikali ya awamu ya tano iingie madarakani.Mimi ni kitendo cha mkuu wa nchi kuwaambia wananchi wafyatuane watoto wengi halafu kesho yake waziri wa afya akaja kukanusha anasema mkuu alikuwa anatania.Hakika nilishangaa sana vipi kwenu wakuu

Mimi nilishangaa tu pale ambapo Mtu mmoja hivi alivamia Kituo kimoja maarufu cha Habari cha Clouds kinyume na Sheria za nchi yetu halafu yeye Kesho yake bila haya na akiwa mkavu kabisa huyo Mtu akamtetea na kumpa moyo kuwa aendelee kufanya Kazi kwani atamlinda.
 
Ahadi za malaika mkuu kuiheshimu na kuilinda katiba, ahadi ya kupambana kwa ajili ya wanyonge, ahadinya kupambana na mafisadi na rushwa. Ahadi zote ni UONGO MTUPU! Pia nimeshangazwa sana na jinsi analivyodharau Bunge na pia kuidharau ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali hadi kufikia CAG kulalamika hadharani kuhusu kushindwa kufanya kazi zao na malaika mkuu kukaa kimya bila kutia neno lolote kuhusu malalamiko ya CAG.

Hili la Bashite nalo limeniacha mdomo wazi na kuzidi kushindwa kumuelewa huyu mtu na akili yake inavyofanya kazi. Halafu kuna wapuuzi wachache wanadai eti hakuna ushahidi wa kutosha dhidi ya Bashite!
 
Mimi nilishangaa tu pale ambapo Mtu mmoja hivi alivamia Kituo kimoja maarufu cha Habari cha Clouds kinyume na Sheria za nchi yetu halafu yeye Kesho yake bila haya na akiwa mkavu kabisa huyo Mtu akamtetea na kumpa moyo kuwa aendelee kufanya Kazi kwani atamlinda.

Hhahahaha hiki kikubwa nadhani ndio kimezaa matamko mengi kama Sipangiwi na lile la vyombo vya habari
 
Back
Top Bottom