Kituko gani alikufanyia mtoto wa mwenyeji wako ulipokuwa ugenini huwezi kukisahau hadi leo hii?

Mwaka flani wageni walikuja nyumbani mtoto akamuomba mama ake simu acheze game mama yake akamwambi imezima chaji na hapakuwa na umeme toka asubuhi

Mama wa huyo mtoto akanambia mpe Basi simu yako acheze game maana ataanza sumbua hapa..nikamjibu haina ilioko ni ya kutumia akili sana sio game last kitoto ..mama yake akasema kuliko Alie we mpe ashindwe

Au mpe a download anajua kutafuta game zake...nikamjibu mwache Alie hii sio PS
 
Miaka furani bhana kuna likizo tulikwenda kwa sista wazo kwenye kota zile sasa asabui dada yangu na ndugu wakike wa mume wa dada asubui walikurupuku na mtoto wa sista akatikisa kabati ambali juu yake kulikuwa na kinanda cha dogo kanunuliwa kama toy achwze kikaanguka na kuvunjika sasa ile mimi natoka wakanitaja mimi shemeji alinipa Kofi la maana tokea siku ile mpaka leo sijawai kuumaliza usiku kwake na hata nikienda basi nampeleka mtu hata nikikutana nae njiani yeye wala watoto siwasalimii na nashukuru watoto wake nimesahau hata sura sizikumbuki
Iyo hatari
 
Mimi nilienda kwa mama mkubwa wa mchumba wangu,tukakuta kajukuu kake pale kadogo kapo chekechea,ni kajanja sana nikmpa simu yangu nikamuwekea game acheze,nikawa naendelea na story na yule mama mara ghafla kikampelekea simu bibi yake kumuonyesha mi nikajua kamewin ile game kumbe kanamuonyesha video ya porn iliyokuwa mule.Niliishiwa pozi kabisa.
Mimi nakumbuka siku moja nikiwa ugenini, huyu mtoto wa mwenyeji wangu aliing'ang'ania radio yangu na mwenyeji wangu akaniambia tumsubirie asinzie watamnyang'anya nakumbuka walinipatia radio yangu saa nne usiku toka saa 12 jioni

Niliwamindi familia yote ila basi tu hawakujua

Weka na wewe cha kwako hapa,
 
Nilienda kwa kaka yangu wa tumbo moja.
Nipo sebuleni naangalia TV, mtoto wa bro alitoka shule. Alipofika hata hakunisalimia.
Kakasimama katikati ya TV, nikamwambia toka hapo, bado tu. Nikamwambia tena. Kakazima TV kakaingia chumbani.
Nikawasha, nikasubiri kanatoka chumban. Nikakashika, nikakapa kifinyo.
Usiku bro anakuja, kanamwambia. Nimempiga. Bro akasema, huyu akileta ujinga piga.
Wazazi wa sasa, jitahidini kuwalewa watoto wenu katika tabia njema ndiyo maana hata ndoa za siku hizi zinavunjika kwa sababu ya malezi.
Namshukuru sana mama yangu, ametulea katika maadili mema. Sisi nyumbani ukimkuta mgeni lazima umsalimie halafu unaenda kucheza nje. Mgeni aletewe hata soda halafu nawe unataka unywe naye kipigo utakachopata.
huwaga kuna jicho unakatwaa aisee usipoelewaa wew bhasii... utajikuta upo nje kucheza
 
Back
Top Bottom