Kituko cha mwaka: Mpangaji aua paka wa mwenye nyumba, alazimishwa kula mzoga

Ningekuwa mwenye Nyumba ,angeondoka saaa hiyo hiyo. Unaanzaje kumuua paka au kiumbe yeyote anayefugwa kisa tu uchafu wako. Kumbuka kutunza kiumbe chochote ni gharama , huyo paka aliugua akatibiwa, anapewa Chakula, malazi nk wewe from no where unamuua. Kwa MZUNGU anakuua na wewe.
 
Hbr Za Jioni Jf.Leo Mida Hii Nimeshuhudia Ugomvi Kati Ya Mpangaji Na Mwenye Nyumba.Mpangaji Kaua Paka La Mwenye Nyumba Eti Limeiba Maziwa Ya Mwanae.Baba Mwenye Nyumba Anamlazimisha Muuaji Ale Nyama Ya Paka Aliemuua.Hapakaliki Zogo Lililopo Hivi Sasa.Inakuaje Paka Tu Mtu Atoe Povu?

uswahilini kuna vituko!!!!
 
Mie navyompenda paka wangu aisee angeuona mlango huyo mpangaji haraka sana.sitaki mchezo na paka wangu
 
Nyumba za kupanga visa haviishi aisee..kikubwa ni kujikwamua uwe na kwako tu!
 
Duh kuua kiumbe kwa ajili ya maziwa tu!! Huyo ame over do!!! Yaani ni sawa kafanyiwa vibaya lakini ametoa adhabu kubwa sana... Mwenye nyumba nae ana haki ya kureact japo sio kwa kumlisha nyama ya paka mpangaji wake
 
Masikini mpangaji!! Najua hajazoea kula nyama ya paka,,ila maziwa na paka bora paka,,paka kahudumiwa tangu utotoni afu unamuua kisa maziwa,,labda kama maziwa yalikuwa ni ujazo wa kontena la bandarini,or else hakutakiwa kumuua,angedai maziwa yake tu.
 
Ningekuwa mwenye Nyumba ,angeondoka saaa hiyo hiyo. Unaanzaje kumuua paka au kiumbe yeyote anayefugwa kisa tu uchafu wako. Kumbuka kutunza kiumbe chochote ni gharama , huyo paka aliugua akatibiwa, anapewa Chakula, malazi nk wewe from no where unamuua. Kwa MZUNGU anakuua na wewe.
Mkuu kua mkweli toka lini paka wa uswahilini akatibiwa?binafsi sijawahi kuona mi naona mpangaji yupo sahihi
 
Back
Top Bottom