Kitu pekee kisichokuwa na ubaguzi duniani ni fedha

Makirita Amani

JF-Expert Member
Jun 6, 2012
1,781
3,074
Duniani kuna ubaguzi wa aina nyingi,
Kuna ubaguzi mkubwa kwenye rangi kwa baadhi ya maeneo.
Kuna ubaguzi wa dini pia.

Upo ubaguzi wa jinsia, kabila, elimu, na mengine.
Lakini kuna kitu kimoja ambacho hakina ubaguzi.
Kitu hicho ni FEDHA,

Hakuna mahali ambapo fedha inabaguliwa duniani.
Nenda popote duniani na watu watataka uwape fedha.
Uwalipe unaposafiri, unapokula, unapolala na mengine mengi.
Hakuna mtu atakuambia hataki fedha yako.

Hii ina maana kwamba, fedha ndiyo kitu pekee kinachotuleta pamoja, bila kujali dini, rangi au kabila.

Ukiwa na fedha, una nafasi ya kushirikiana na wengine.

Hili linaifanya fedha iwe ndiyo kitu muhimu kuliko vyote duniani, ukiondoa hewa unayopumua bure.

Ni muhimu ukawa na msingi sahihi wa kifedha.

Hivyo soma kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA FEDHA ujifunze misingi sahihi ya kifedha itakayokutoa kwenye umasikini na madeni na kukupeleka kwenye utajiri na uhuru wa kifedha.

Kupata kitabu hiki, piga simu 0678 977 007.
 
Wasio na fedha wanabaguliwa nayo inachochea ubaguzi. Kifo ndio mpango mzima.... hakuna ubaguzi hata uweje utakufa
 
Wasio na fedha wanabaguliwa nayo inachochea ubaguzi. Kifo ndio mpango mzima.... hakuna ubaguzi hata uweje utakufa
Ni kweli, usipokuwa na fedha utabaguliwa, lakini ukiwa nayo hakuna atakayeikataa fedha yako kwa sababu yoyote, kila mtu ataitaka fedha yako.
Ndiyo maana ni muhimu uwe nazo za kutosha.
 
Fedha ina ubaguzi mkubwa sana, kwa nini wengine wanazo wengine hawana?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli, fedha ina tabia ya kuwakataa watu wenye tabia fulani na kwenda kwa wale wenye tabia fulani, lakini unapokuwa nazo, hakuna atakayezikataa.
Muhimu ni kujua tabia zipi zitavuta fedha kuja kwako, kisha kuwa nazo ili uwe na fedha na usibaguliwe.
 
Back
Top Bottom