Kitu gani unapenda ujifunze na kukiunda katika workshop ijayo ya electronics

Transistor

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
970
1,461
Nimekua nikiendesha workshop kadhaa za electronics,ambapo tumekua tukijifunza na kuunda projects tofauti tofauti za electronics ambapo idea ya projec hizo nilikua nazitoa mwenyewe.

Kwa mwezi wa nane kuna workshop nyingine,lakini ningependa katika workshop hii wadau waseme wao wenyewe idea za projects ambazo wana penda wajifunze na kuziunda katika workshop ijayo.

Lengo hapa ni kjifunza kuunda vifaa ambavyo vinaweza kuuzika kwa jamii ili muundaji aweze kupata kipato,au kwa namna moja au nyingine ubunifu wake huo iwe sehemu ya ajira yake.

Unaweza kupendekeza project yoyote katika nyanja za Analogy pamoja na Digital,

Si lazima idea hiyo iwe umesha wahi kuunda,hapana hata kama una wazo la ubunifu wenye tija unaweza kulitoa,sisi tunaangalia kama liko ndani ya uwezo wetu,ili tuweze kuliingiza katika projects zetu tutakazo ziunda wakati wa workshop hiyo.

Kumbuka kile unacho pendekeza kiwe na uwezo wa kuuzika katika jamii yetu,kiwe ni hitaji la jamii.

unaweza kutuma idea yako hapa au kupitia email yangu ya datetz18@yahoo.com.

Karibuni.
 
ukibuni mosquito repellent tool........yaan utengeneze tool inayogenerate frequency za kufukuza mbu na wadudu wengine utauza sana
 
Back
Top Bottom