Kitu gani unakumbuka zamani ukiwa mdogo mkicheza mpira wa 'manailoni'?

Niliwahi kutoa kucha ya dole gumba baada ya kukosea timing ya kupiga ule mpira. Niliificha home wasijue hadi kidole kikatoa ufunza, dawa ilikuwa ni mchanga tu hadi kucha mpya ikarudi.

Mwenye mpira ndiye hatakiwi kukwazwa, maana anaweza kuuchukua, alafu asiondoke akabaki hapohapo na nyie hamna cha kumfanya
 
Niliwahi kutoa kucha ya dole gumba baada ya kukosea timing ya kupiga ule mpira. Niliificha home wasijue hadi kidole kikatoa ufunza, dawa ilikuwa ni mchanga tu hadi kucha mpya ikarudi.

Mwenye mpira ndiye hatakiwi kukwazwa, maana anaweza kuuchukua, alafu asiondoke akabaki hapohapo na nyie hamna cha kumfanya
Hiyo hatari sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mchezo tulikua tunaucheza unaitwa "Angaisha bwege" hapa mnaweza mkawa kundi hadi watu kumi halafu akachaguliwa mmoja kua awe bwege wa kutafuta mpira katika wale tisa, ilikua ni jipu kwangu yani kila time bwege nakua mimi halafu huo mpira kuupata kwake ni msoto.

Tukija kwenye "kaokote" huu ulikua mchezo wa kurusha mpira halafu mwenzako anapiga utapoenda kutua unatakiwa uufate ukauokote halafu umrushie tena, hapa victim anayepata shida ni yule mrushaji na ili aepukane na hiyo shida inatakiwa akirusha mpira yule jamaa anayepaswa kuupiga aupige halafu kabla hujatu chini nawe uupige. Hapo adhabu inaendwa kwake anaanza yeye kurusha halafu wewe unakua m-butuaji.

Aah yani hapa napo ilikua ni adhabu kwangu maana kulikua na lijamaa hilo linamashuti ukirusha tu mpira linaupigia mbali usawa wa mita mia yani ile angle ya kusalimika kwa kupiga mpira huipati
 
Niliwahi kutoa kucha ya dole gumba baada ya kukosea timing ya kupiga ule mpira. Niliificha home wasijue hadi kidole kikatoa ufunza, dawa ilikuwa ni mchanga tu hadi kucha mpya ikarudi.

Mwenye mpira ndiye hatakiwi kukwazwa, maana anaweza kuuchukua, alafu asiondoke akabaki hapohapo na nyie hamna cha kumfanya
Ulikuwa unapigia dochi Hata Mimi nimetoa sana kisa madochi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mchezo tulikua tunaucheza unaitwa "Angaisha bwege" hapa mnaweza mkawa kundi hadi watu kumi halafu akachaguliwa mmoja kua awe bwege wa kutafuta mpira katika wale tisa,

ilikua ni jipu kwangu yani kila time bwege nakua mimi halafu huo mpira kuupata kwake ni msoto

Tukija kwenye "kaokote" huu ulikua mchezo wa kurusha mpira halafu mwenzako anapiga utapoenda kutua unatakiwa uufate ukauokote halafu umrushie tena, hapa victim anayepata shida ni yule mrushaji na ili aepukane na hiyo shida inatakiwa akirusha mpira yule jamaa anayepaswa kuupiga aupige halafu kabla hujatu chini nawe uupige. Hapo adhabu inaendwa kwake anaanza yeye kurusha halafu wewe unakua m-butuaji

aah yani hapa napo ilikua ni adhabu kwangu maana kulikua na lijamaa hilo linamashuti ukirusha tu mpira linaupigia mbali usawa wa mita mia yani ile angle ya kusalimika kwa kupiga mpira huipati
Zubaisha bwege ukipigwa tobo unautafiuta Mara mbili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi nakumbuka matukio kadhaa.

• Kwanza mwenye mpira lazima awe mshambuliaji namba 9

• Ukiwa bonge lazima uwe kipa

• Refa akikupa kadi anakuvunjia kipande kabisa cha plastiki ya njano anakupa ukae nacho

• Mwenye mpira hata akipiga nnje akikomaa kwamba ni goli hamna kipingamizi

Wewe unakumbuka nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
Nakumbuka zile ligi zawadi zilikuwa ndogo mkiibuka mambingwa,,

Ila cha ajabu mko radhi hata kuvunjana miguu,, dah

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama huna kiwango kama watu hawatoshi we ndo unachaguliwa ila ujue hawachelewi kukufanya sub au unakaa kipa.

Kama we ni mwenye mpira na siyo mbabe kumaliza mechi unadaka mpira unatoka nduki kuelekea nyumbani.

Kama huna namba lazima unifanye rafiki wa mwenye mpira kinafki.

Wenye hasira ambao hawakupata nafasi mpira ukitoka badala ya kurudisha wanauongezea spidi uende mbali wachukue wenyewe.

Aisee kulikuwaga na raba za kike zinaitwa LOSSO zinakamba unafunga hadi juu ya henka,mi nilikuwa naiba za dada yangu naenda kupiga nazo mpira

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom