Kitu gani ulikiwa unapenda kufanya utotoni lakini ulikosa uhuru kwa wazazi?

Zacht

JF-Expert Member
Jul 17, 2020
1,009
2,196
Hello!

Nadhani kila mtu anakitu ambacho kinampa furaha akikifanya Mimi binafsi kungalia movie ndio hobby yangu kubwa Sana ,na enjoy Sana kuangalia.

wakati nipo mdogo nilikuwa naangalia Sana muvi hadi nasahau muda kula yaani nilikuwa nikienda asubuh basi kurudi jioni ,nikirudi home nachezea fimbo zangu,naoga ,Nakula chakula changu cha mchana siku imeisha Kesho tena (kwa weekend na likizo) siku za shule nikitoka tu shule saa kumi nipo bandani.

Nilikuwa mteja hadi jamaa alitaka kunipa kazi ya kusimamia Banda lake yaana niwe muonyesha tv wake 😃 just imagine,na nikisema Leo Sina hela napita free .

Shida ikaja kwa wazee baada ya kuona sifanyi vizuri dalasani wakaja kungundua muvi ndio sababu basi nikapigwa ban nisionekane banda la video Kaka zangu wakapewa kazi wakiniona tu banda la video wanipige .

Nilikuwa naangalia kwa tabu Sana nilikuwa nakaa malangoni kama konda ili tu niwaone ma-bro wakija na sio kwamba nilikuwa zero kabisa class no Lkn marafiki zangu walikuwa top five Mimi top 10 nilikuwa nanusa na kupotea kwahy mzee akaona solution kunikataza.

Nilikuja kupata freedom kdogo baada ya ku perform vizuri form two nikapewa hadi na simu kama zawadi (bro anilipa ,mzee baadae akanipora)

Sasa nimekuwa mtu mzima lakini Bado muvi Bado napenda Sana kungalia ,hakuna wakunipangia wala kunizuia ingawa wazee walikuwa sahihi .wewe ulikua unapenda kufanya Nini.?

NOTE:
-Movie ni sana,
-Movie ni fasihi (simulizi).
-Tofauti ya movie na kusoma kitabu ni kwamba muvi unaangalia(unasimuliwa), kitabu unasoma
-Movie ni summary ya kitabu.

Kwahiyo usidhani kungalia movie ni utoto na kupoteza muda kama muumini wa hii nadharia think again.

Share kisa chako
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom