Kitu gani ukikisahau mahali lazima ukirudie?

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
21,713
35,514
Kuna kitu ambacho ukikisahau mahali iwe nyumbani, Ofisini, au mahali popote lazima uahirishe uendako au uchelewe ili ukirudie? Kitu gani ambacho kitakulazimu kukirudia na kuchelewa uendako??

  1. Kadi za atm
  2. Funguo
  3. Mkoba[pochi]/Wallet
  4. Leseni ya udereva
  5. Mpakato
  6. Tablet
  7. Simu
  8. Hela
  9. Chaja za simu
  10. Au chochote
Mi nikisahau simu nyumbani hata kama sipo mbali na naenda kazini sirudi aisee ntakuta simu zilizokosekana na meseji.
 
Narudia kilicho na umuhimu na chenye gharama, mbali na hapo huwa sirudi;

Nakumbuka enzi zile kurudia kusajili upya laini ilikuwa haraka tuu, ikitokea nimesahau simu ikiwa ndogo narudia kusajili tuu laini mbele kwa mbele;

Kadi ya Benki, kama ina hela sawa lakini kama haina ya nini potelea mbali mbele kwa mbele nitaandika ripoti ya kupotea, funguo nayo kama kufuli la elfu 2000 navunjaga kuliko kutumia gharama kubwa kurudi,

Pesa ikishasahaulika maana yake unayo nyingine .
 
Nauli ya mwendokasi lazima nirudie maana nitaendaje kazini? wakati wa kurudi sio issue maana nitapata kazini.
Kuna siku nilisahau simu wakati naenda kazini, nilivumilia siku nzima na niliporudi nyumbani kutoka kazini sikukuta missed call wala msg yoyote
 

Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom