MAPUMA MIYOGA
JF-Expert Member
- Jan 30, 2013
- 3,792
- 2,362
Toka niko mtoto na sasa ni mtu mzima, late 30's sijawahi kuona uwekezaji wowote wa Serikali katika wilaya Iramba.
Kumekuja habari za zahanati na shule za secondari, ni wananchi ndio waliouza kuku zao kujenga shule zile na zahanati.
Miundombinu kama ya kilimo ndio kabisa hakujawahi kuwa hata na mbolea za ruzuku kama zile zinatolewa mikoa mingine, wananchi wanahangaika kama hawako Tz hii hii.
Shule za zamani kama Lulumba na Tumaini ambazo ni miaka ya early 70's mpaka leo hata ukarabati tu haufanyike, watoto wanaishi kwenye mabweni kama mapango.
Nikiangalia mikoa mingine ujenzi wa miundombinu umepamba moto, kuna shule za kiwango cha juu sana zinajengwa kwa pesa ya Serikali, nauliza huku Iramba sio Tanzania hii hii?
Kuwaona mawaziri au Rais mpaka uchaguzi waje kuomba kura, kwanini huu ubaguzi?
Iramba tunahitaji na sisi tule sehemu ya mkate wa nchi hii sambamba na wengine katika nchi.