Kitu gani kinakusumbua leo wakati wewe ndiyo mbegu pekee iliyofanikiwa kupevusha yai?

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
3,907
6,700
Biology inasema baada ya tendo la ndoa mbegu za kiume zinazoingia kwa mwanamke ni takribani mbegu milioni mia tatu (300,000,00) na zote huanza kuogelea kuelekea kwenye ovum (yai)

Kati ya hizo mbegu milioni 300 zinazofanikiwa kufika sehemu husika kwenye yai nj mbegu 500 tu, nyingine huchoka mapema na kufa njiani.

Vilevile katika hizo mbegu 500 zilizofanikiwa kufika kwenye yai ni mbegu moja tu ndiyo hushinda na kuingia ndani kutengeneza kiumbe.

Mbegu hiyo ni wewe unayesoma post hii. Biology inatuambia kuwa ulikimbia mbio na kuwashinda wenzio milioni 300 na ndio maana leo hii upo Duniani.

Usingekukuwa mshindi katika mbio zile leo usingekuwepo Duniani.
Je umeshawahi kufikiri juu ya hili?
Ulikimbia bila macho, mikono wala miguu na ukashinda. Ulikimbia bila elimu yako, ujuzi wala vyeti na ukashinda!
Ulikimbia tena bila msaada wa mwingine yeyote na ukashinda.

Ni kitu gani leo cha kukufanya uwaze kushindwa katika maisha kiasi cha kukata tamaa?
Sasa unayo macho, mikono na miguu, una elimu, ujuzi na maarifa zaidi unaongozwa na maneno ya mwenyezi Mungu kwanini uwaze kushindwa?
Ulizaliwa ukiwa mshindi usiishi maisha ya kushindwa wewe ni shujaa wewe ni zaidi ya hivyo ulivyo hakuna kama wewe.
FB_IMG_1545906474759.jpeg
 
Tusisahau kwamba mbegu hiyo iliyozishinda zingine ilikuwa na chromosomes mbili X na Y ikakutana na yai la mama yako lenye chromosomes X na X. Kama wewe ni wa kike jua kwamba ulisababishiwa na mbegu ya baba yako ambapo X yake iliungana na X ya mama yako. Kama ni me, Y ya baba iliungana na X ya mama yako.
Nyie wanaume mke wako akizaa jnsia yoyote ujue wewe ndo umeisababisha.
 
Kama najiona yule pale juu na spidi yangu kama usain bolt..
Asante my late mama kwa kuona thamani yangu na kunitunza hadi kunizaa..tabu nimekutana nazo tangu tumboni mwa mamangu lakini sitokata tamaa.
 
Tukumbuke kuwa Y cromosome wakati wa mshindo ndo zinakimbiza upepo kwa kasi kubwa hivyo zinawahi kuzifikia X cromosome za mwanamke, tatizo Y cromosome ziko weak sana kwenye joto na Acid, ndio maana Mungu aliweka Korodani zininginie nje kupunguza joto ili kuziokoa Y, lakini pia ni vizuri kumwandaa mwanamke vizuri ili atoe alkiline itakayosaidia kuneutrolize acid inayotokana na mabaki ya mkojo katika njia ya uzazi ya mume na mke ili y zipone wakati wa mshindo, kinyume na hapo x zinaikuta x na kzaliwa mwanamke,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli ulijiamini before consciousness sasa leo uko conscious haujiamini.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
nakumbuka enzi hizo naitwa sperm nilikimbia mbio fupi na ndefu kwa wakati mmoja.
 
Nafikiri! Hivi hizi mbegu zikimagwa "sehemu si stahili", wanajua kuwa hapa hakuna ya kukimbizana au wanaanza tu mbio kama kawaida????
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom