Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Magera na mwenziw Sais OP yetu JK walihenyeshwa sababu kuna katoto ka brigedia walikuwa wanakazingua aisee si ndo simu ikapigwaa toka juu mbona kiliwakaa palee...!! Ilikuwa jau sana aisee
Kale keupe alikitia banzi siku ya intro to camp usiku danger coy akafanya watu tusimike usiku mzima dgo akasepa usiku ya mguu hadi kwao akarudishwa siku tatu mbele jamaa.akaqekwaga ndan 6 week ndo ikawa pona pona yetu
 
Nilikuwa nachukia sana MRADI,
Pale JKT Makutupora opereshen miaka 30 ya Uhuru.
Afande Mwshamba wa C - COY alikuwa anaudhi sana .
Kila siku Kujenga baraza ya Mchanga kisha asubuhi anaikanyaga na kuivuruga.
Huu tulikuwa tunauita Mradi.
 
Wakongwe wa Mafinga JKT (1980), Eagle Coy, Operation Tija hatutamsahau Afande Masoda, Kapteni Mangwembe na Sajenti Mungure. Kero ya pale ilikuwa baridi kali mno na unapangwa gadi Changarawe; Dah hakuna rangi utaacha kuona. Kingine ni kutokuwepo kwa viti au fomu za kukalia. Kila siku kwenye Chenja lazima ukae chini kwenye mchanga/vumbi sio kuchuchumaa i.e makalio lazima yaguse ardhi - Unachafukaje!!
Kero nyingine ilikuwa ni kufyagia asubuhi- kuna giza na mifagio tunaikata wenyewe kwenye kapori ka miti ya Miwati pembeni mwa barabara (smart Area). Hako kapori kalikuwa ni mahali pa kujisaidia haja kubwa wale wanaokuwa Kota gadi. Sasa kwa giza hilo huoni chini na utakanyaga sana mavi. Matokeo yake Mnanukaje mtakapoenda kwenye uji kwa mwendo wa kunyakuwa-nyakua..
Sali/Omba siku hiyo usikutane na Afande Nusumungu.... yupo "Heey! Zoezi limebadilika... Nyumaaa geuka'....." na ngarambe ndo inaanzia hapo.
...I love those Old Good Days .
Respect mzee wetu.

Una kumbukumbu nzuri.
 
833 KJ oljoro...a place to remember OP miaka 50 ya muungano,machenja na mabio...Mambo ya kitundu...Kuna afande alikua anakuja anawaamsha kistaarabu wakati wa kwenda na ishara ni harufu ya sigara anayovuta...muda wa kurudi akikuta umelala inakula kwako
 
Tulipigwa route march danger coy nzima baada ya kuimba "Zaina Zaina mtoto wa kitanga Zaina lete raha Zaina..."

Pia kuna mwenzetu alipelekwa lupango kosa lake ilikuwa "kujongo" kazi akapewa extra drill kumbe alikuwa ana malaria kali akilalamika MP anaongeza adhabu mpaka akaanguka... akafia njiani akikimbizwa hospitali ... John's coner
Huyu bwana tulikuwa naye lupango
 
Kabla sijaenda JKT nilikuwa mwoga,bwege, low self-esteem esteem ,confidence,domo zege,mvivu,legelege

Nilipotoka kule nilikuwa mtu tofauti kabisa na nilishukuru mwenyewe hadi leo kwa kuenda kule
 
Niliwahi tongozwa na demu kombaini nzima wakajua

Basi wakati chenja zile kucheza wanamleta kwangu pumbavu zao
 
Nimefanya uchunguzi mdogo kwa vijana walioko vyuoni, hali inasikitisha sana.

Vijana hawana nidhamu siyo tu ya kazi hata ya muda.

Vijana hawana maono ya maisha yao binafsi au taifa. Maisha hawayajui kabisa hata wale wengine waliotokea maisha ya hali ya chini lakini hilo halijawafanya wawe 'humble'. Wana 'sense of entitlement'. Wanatamani tu na kudhani wanastahili vitu vizuri bila kuvifanyia kazi.

Vijana wa siku hizi, mvua tu ikinyesha ni kisingizio cha kutokwenda darasani au kutimiza wajibu fulani.

Vijana hawana maadili ya kuwa wakweli na waadilifu. Wanagerezeana kwenye mitihani, wengine kazi za makundi wanalipa wafanyiwe na wengine. Ukiacha wafanye kila mtu peke yake, vitest tu zero zinakuwepo za kutosha.

Huko JKT wanapokwenda baada ya kumaliza Form 6, wanajifunza nini sasa?
 
Back
Top Bottom