Kitu gani kiliikumba hii familia ya kifahari pale Magomeni

Habari wadau..!

Maisha kweli ni fumbo, mpaka leo sijapata kujua undani wa familia ile ya kifahari pale Magomeni Mwembechai.

Kuna siku nilikuwa na project maeneo yale ya Magomeni nilifika site lakini nikajikuta kuna baadhi ya vifaa vya kufanyia kazi sikubeba. Hivyo nikaona sio kesi ngoja nijiongeze kutokana na mazingira ya site ikanibidi nigonge hodi nyumba za jirani kuomba msaada.

Bahati nzuri natizama mbele nikaona ghorofa kubwa kama floor moja ikabidi nisogee niombe msaada,bahati mbaya nilivyofika pale kila mtu alikuwa amenikunjia sura kama tuna ugomvi hakuna aliyepokea salamu yangu wote niliowasalimia.

Nikaona hapa kuna tatizo ,watu walikuwa wengi kwenye ghorofa kama kuna mkutano waume kwa wake wa rika zote.Ikabidi nimsogelee binti mmoja nijaribu kuongea naye labda anaweza nisikiliza ila nilipoanza kuongea naye tu,nilisikia sauti ikitoka ghorofa ya juu kwa ukali ikiuliza "huyo ni nani na anataka nini hapa?"

Hapo ikabidi nitazame juu na kumjibu mtu yule kwa kuzuga na kusahau kilichonipeleka pale nikajikuta na jibu "mimi ni mgeni nahitaji huduma ya choo".Kabla sijajibiwa na yule mtu kule ghorofani kuna mzee alikuwa pembeni akanambie nenda kushoto utaona choo.

Kiukweli watu wa pale walikuwa wakali sana na hawapendi wageni kabisa ,duuh wakati nipo chooni nikaanza kuchunguza nini kina endelea kwenye ghorofa hii ya kifahari.

Ni ajabu sana ndio nilipogundua kumbe wanauza pombe za kienyeji a.k.a matapu tapu,nilijisaidia na kutoka haraka sana sikuongea na mtu yeyote ikabidi niende nyumba zingine za jirani kuomba msaada wa vifaa vya kufanya kazi yangu.

Je, nini kiliikumba familia ile ya kifahari mpaka kugeuza ghorofa ya kifahari kuwa club ya kuuzia matapu tapu bila shaka kutakuwa na historia ndefu sana.
Kuna kitu haujakiweka sawa katika stori yako hii.

Popote pale pauzwapo pombe hasa hayo mataps huwa kuna ukarimu wa kuzugia wateja.

Sasa hapo pa kufokeana na kushitukiana yaonesha haukupachunguza vizuri, yawezekana pakawa na biashara nyingine haramu nyuma ya pazia!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mjini mambo ni mengi mzee nyumba ya hivyo tena magomeni mengi hufanyika, wale watu walivo kuona kutokana na mwonekano wako waliona wewe sio mwenzao na wakashusha pumzi kukuchorea ramani labda usiwe shushu.
 
Back
Top Bottom