Kitu gani kiliikumba hii familia ya kifahari pale Magomeni

TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Feb 26, 2018
2,490
3,534
Habari wadau..!

Maisha kweli ni fumbo, mpaka leo sijapata kujua undani wa familia ile ya kifahari pale Magomeni Mwembechai.

Kuna siku nilikuwa na project maeneo yale ya Magomeni nilifika site lakini nikajikuta kuna baadhi ya vifaa vya kufanyia kazi sikubeba. Hivyo nikaona sio kesi ngoja nijiongeze kutokana na mazingira ya site ikanibidi nigonge hodi nyumba za jirani kuomba msaada.

Bahati nzuri natizama mbele nikaona ghorofa kubwa kama floor moja ikabidi nisogee niombe msaada,bahati mbaya nilivyofika pale kila mtu alikuwa amenikunjia sura kama tuna ugomvi hakuna aliyepokea salamu yangu wote niliowasalimia.

Nikaona hapa kuna tatizo ,watu walikuwa wengi kwenye ghorofa kama kuna mkutano waume kwa wake wa rika zote.Ikabidi nimsogelee binti mmoja nijaribu kuongea naye labda anaweza nisikiliza ila nilipoanza kuongea naye tu,nilisikia sauti ikitoka ghorofa ya juu kwa ukali ikiuliza "huyo ni nani na anataka nini hapa?"

Hapo ikabidi nitazame juu na kumjibu mtu yule kwa kuzuga na kusahau kilichonipeleka pale nikajikuta na jibu "mimi ni mgeni nahitaji huduma ya choo".Kabla sijajibiwa na yule mtu kule ghorofani kuna mzee alikuwa pembeni akanambie nenda kushoto utaona choo.

Kiukweli watu wa pale walikuwa wakali sana na hawapendi wageni kabisa ,duuh wakati nipo chooni nikaanza kuchunguza nini kina endelea kwenye ghorofa hii ya kifahari.

Ni ajabu sana ndio nilipogundua kumbe wanauza pombe za kienyeji a.k.a matapu tapu,nilijisaidia na kutoka haraka sana sikuongea na mtu yeyote ikabidi niende nyumba zingine za jirani kuomba msaada wa vifaa vya kufanya kazi yangu.

Je, nini kiliikumba familia ile ya kifahari mpaka kugeuza ghorofa ya kifahari kuwa club ya kuuzia matapu tapu bila shaka kutakuwa na historia ndefu sana.
 
magomeni mapipa×2

sinza kwa wa janja na kinondoni

Screenshot_20210709-090821_Quora.jpg
 
Mkuu tambua tu kwamba maisha hua yanabadilika kwa kasi sana. Ukizunguka zunguka mitaani hasa mijini utakutana na maghorofa ambayo hayajamaliziwa mwaka wa 20 huu, mapagale, viwanja/mashamba yaliyotelekezwa nk.

Mara nyingi maeneo kama hayo unakuta labda alieanza hiyo project alifariki na aliowaacha hawakua na uwezo wa kuendeleza. Au unakuta yupo ila maisha yamempiga. So mambo ni mengi mkuu.
 
Sasa ilikuaje wanakuwa wakali wakati walevi na ukali ni kama maji na mawese
Na mimi nilitaka kuuliza juu ya hili. Sehemu yenye biashara ya ''ma-taptap'' mara nyingi inakuwa na watu friendly na ni wakarimu sana. Hapa mkuu TheDreamer Thebeliever kuna namna. Siyo ''taptap'' tu au pengine inatumiwa kuzuga. Uwezekano mkubwa ni kiwanja cha ''unga'' au gongo au vyote kwa pamoja. Magomeni kwa unga ndiko kwenyewe. mrangi pengine anapajua.
 
Na mimi nilitaka kuuliza juu ya hili. Sehemu yenye biashara ya ''ma-taptap'' mara nyingi inakuwa na watu friendly na ni wakarimu sana. Hapa mkuu TheDreamer Thebeliever kuna namna. Siyo ''taptap'' tu au pengine inatumiwa kuzuga. Uwezekano mkubwa ni kiwanja cha ''unga'' au gongo au vyote kwa pamoja. Magomeni kwa unga ndiko kwenyewe. mrangi pengine anapajua.
sikutaka kuongelea upande huo,maana sijaziona hizo biashara kwa dakika tatu nilizojibanza chooni.Ila wenyewe ndio wanajua wanauza nini hasa mbali na pombe chafu🙄🙄🙄
 
Back
Top Bottom