Kitu gani hutokea Wakili mtarajiwa anaposhindwa kulipa Admission Fee kwa wakati?

LIKUD

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
15,111
27,096
Kuna Bwana mdogo mmoja kanisikitisha Sana. NI hivi baada ya kufaulu law school alifanya petition ya kuwa admitted na akafanikiwa Hadi hatua ya APPEARANCE.

Ngoma ikaja kwenye malipo kabla ya admission ceremony ambayo according to him yana cost kama laki 5 na ushee.

Namfahamu huyu dogo kupitia mdogo wangu coz mdogo wangu pia anaapishwa hiyo tarehe kumi

Nimetoka kumtext now namuuliza maandalizi ya sherehe vipi ananiambia bro nimekosa hela ya kulipia TLS na Judiciary ( laki tano)

I was like kwanini usingenichek Mimi ningekuazima? He was like sikutaka kumsumbua yoyote nimeona nisubiri mpaka mwezi wa kumi na mbili

Niliguswa Sana. Jamani ukiwa na Tatizo talk to people unaweza kupata msaada.

Sasa am asking myself kitu gani hutokea pindi wakili mtarajiwa anapokosa kufanya malipo? NI kwamba ndio admission yake inafutwa au anaweza kuapishwa kipindi kitakachofuata?

And utakapofika muda huo atatakiwa kuandika barua au unakuwaje?

TLS na wizara ya Sheria badilisheni utaratibu. Hawa vijana wakishafaulu waacheni waapishwe bure Bila malipo yoyote wengi wanatoka familia masikini kumwambia atoe laki tano ni kumuonea bure
 
Siunaandika barua mkuu,Mimi huwa silipi kwa wakati,nawapima wakikubali nakula
 
Kazi ya uwakili nayo imekuwa ngumu sana
mawakili wanaongezeka kazi zimebaki pale pale....
Huyo dogo anytime anaweza kulipia...
akipata hiyo 500000
 
Sababu ya uzi ni nini hasa? Majibu yote nina uhakika umeshayapata kutokana na majibu ya wakili msomi.
 
Kazi ya uwakili nayo imekuwa ngumu sana
mawakili wanaongezeka kazi zimebaki pale pale....
Huyo dogo anytime anaweza kulipia...
akipata hiyo 500000
So anunue joho na siku ya admission ceremony ahudhurie?
 
Uapisho ni wa jumla jumla yy tayari namba ya uwakili anayo na hilo ndio la muhimu, hiyo laki tano ni ya kulipia leseni yake
Hapo poua . Basi nikadhani labda akienda kutakuwa na mambo ya kuonyesha receipt za malipo au watakao kuwa wamelipia ndio watakao itwa.
 
Kweli TLS iwaache jamaa wasiwe wanalipia maana wengi wametoka familia masikini....
 
Mkuu, admission hufanyika baada ya wahusika kukidhi vigezo vinavyotakiwa. Vikubwa ni kufaulu law school, kuwasilisha petition na kufanya malipo yanayotakiwa. Kwakuwa hakufanya malipo, hatawekwa kwenye orodha ya watakaoapishwa ingawa anabaki kuwa ametimiza vigezo vinginevyo na anaweza kuapishwa wakati mwingine. Hata kama mhusika angekuja kusema jambo hilo hapa JF, naamini angepata msaada.
 
Kuna Bwana mdogo mmoja kanisikitisha Sana. NI hivi baada ya kufaulu law school alifanya petition ya kuwa admitted na akafanikiwa Hadi hatua ya APPEARANCE.

Ngoma ikaja kwenye malipo kabla ya admission ceremony ambayo according to him yana cost kama laki 5 na ushee.

Namfahamu huyu dogo kupitia mdogo wangu coz mdogo wangu pia anaapishwa hiyo tarehe kumi

Nimetoka kumtext now namuuliza maandalizi ya sherehe vipi ananiambia bro nimekosa hela ya kulipia TLS na Judiciary ( laki tano)

I was like kwanini usingenichek Mimi ningekuazima? He was like sikutaka kumsumbua yoyote nimeona nisubiri mpaka mwezi wa kumi na mbili

Niliguswa Sana. Jamani ukiwa na Tatizo talk to people unaweza kupata msaada.

Sasa am asking myself kitu gani hutokea pindi wakili mtarajiwa anapokosa kufanya malipo? NI kwamba ndio admission yake inafutwa au anaweza kuapishwa kipindi kitakachofuata?

And utakapofika muda huo atatakiwa kuandika barua au unakuwaje?

TLS na wizara ya Sheria badilisheni utaratibu. Hawa vijana wakishafaulu waacheni waapishwe bure Bila malipo yoyote wengi wanatoka familia masikini kumwambia atoe laki tano ni kumuonea bure
Uyo bwana mdogo kakudanganya usikute hata law school haku PASS
 
Back
Top Bottom