Kitu gani cha kijinga uliwahi kufanya ulipozama kwenye mapenzi?

Alikua single maza nikamchukua yeye na mtoto wake nikaa nao getto kila kitu nawahudumia, huku mtoto nikampeleka shule

Bi mkubwa alikuja kujua alimaind sanaa kwanini nakaa na mke wa mtu (Mwanamke mwenye mtoto) ndani, me nikapuuza maneno nikaendelea kuishi nae,

Jamaa yake alikuja akamuomba msamaha full kupiga magoti huku analia demu akakubali akamsamehe wakaludiana,

Huwa nikaa nikafikiria najutaga sanaa kupoteza mda wangu na gharama zangu kwake pamoja na kufanya yote hayo hakuwa na shukrani hata kidogo
Najutiaga sana hiki kitu mpaka kesho siwezi sahau
Dooh, polee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nilimpiga kizinga mshua na bi.mkubwa, kama laki hivi (kwa miaka ya 2000 ilikuwa pesa nyingi) nikajimwambafy nikamuiba mtoto wa getikali nikaendanae mikadibeach nikaspend laki yoteeee halafu niliambulia kumpiga mate tu, niliporud home nilichezea kifinyo cha hatari na demu nae akachezea kwao keshoyake akanitumia sms SIKUTAKI TENA.....
 
We jamaa ni Legend
Miaka kdhaaa nyuma uko nilipokua kidato cha Tatu.

Kuna SAA LA Ukutani Mzee alitoka nalo uko kwa wabudha (ilikua nzuri sana ,maana kila mgeni aloingia sebuleni hakua acha kuuliza iliponunuliwa ).


Nililibeba nikaenda kumpa Demu wangu ..Demu naye sijui aliuza .
Alafu tukaja KUACHANA iyoiyo cha tatu.



Sema sitosahau zile bakora nilizopewa!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
😂 😂 😂 😂
Nisamehe mkuu, nimeshindwa kuvumilia hii 'stand-up comedy' imenivunja mbavu..!!

Huu utakuwa ni mchanganyiko wa lugha 3 mfululizo.!
Jamaa ameamua kuchangamsha tu. Hapo mwisho ameandika kiingereza safi, atakuwa anajua anachokifanya.
 
Bado kwa kweli kushikwa akili na mtu maana sinaga akili za kukurupuka.
 
Zivunjike tu ndo hali halisi hiyo..

Ugonjwa wa namna hiyo huwa unakuachia ukiwa umelazwa zikija hela za ugua pole! Sasa kimbembe pata ahueni rudi nyumbani watu wasilete hela za pole na zile ulizonazo ziishe!! Ugonjwa huja mara mbili zaidi na ukikuta watu wamechoka kukuletea hela za ugua pole jua kikulacho ki nguoni mwako! Nakwambia kuna faulo shetani mwenyewe huwa hazisimamii anaacha mambo yajipe yenyewe viungo vyako vinakuuwa maana vimekuchoka huna hela😂😂!!
Kenzy....... you made my Day..... unajua napitia hii hali... Nacheka utafikiri mazuri
 
Ilikuwa tukitoka kanisan namsindikiza mpaka kwao kwa miguu ni mbali kwel kwel kisha nikimfikisha narudi kwetu ambako ni safari kama ile ile mara 2 yake yan nikirudi nyumban nalala kama ndama kwa uchovu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mm kuna kitu nilikuq nataka nifanye kesho saa 1830 ila baada ya kusoma uzi huu basi nishaona cha kijinga halaf wastage of money.Sifanyi ng'oooo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom