Kitu cha muhimu zaidi kuzingatia ili uwe na mapenzi mazuri unayofurahia

Infinite_Kiumeni

JF-Expert Member
Jan 23, 2023
382
661
Ukiona unapata shida kwenye mapenzi, hauridhiki na mapenzi unayopata, hauridhishwi kitandani. Kiasi kwamba unaona hutokuja kupata mapenzi ya kweli. Au umekata tamaa ya kufaidi mapenzi.
Usijali kitu cha kwanza cha kuzingatia ni.

Kuwa mkweli na nafsi yako
Usianze kulaumu mtu wa nje, usianze kumlaumu mpenzi wako, badala yake anza kujiangalia wewe mwenyewe. Anza kujiangalia ni kitu gani kinakufurahisha zaidi. Mpenzi wako sio malaika, hawezi kuotea unachokitaka kitandani/ kwenye mapenzi. Anza kujizingatia na ujue unahitaji nini.

Kuwa mkweli kwa nafsi yako inamaana kwamba, achana na kila kitu unachofikiria kwamba mapenzi/ mahusiano yaweje, ufanye mara ngapi, mapenzi ni kwa ajili ya kitu fulani tu, mpo kwenye mahusiano kwa ajili ya watoto tu, au chochote ulichokaririshwa kuhusu mapenzi na mahusiano.

Na uanze kujiuliza we mwenyewe unahitaji nini, kipi kitakufanya ujisikie raha zaidi. Jiangalie na ujue hamu yako kimapenzi ikoje.

Kitu gani kitaukonga moyo wako, unapenda ufanyiwe nini kitandani, unapenda kuwa na mapenzi aina gani, unapenda mtu mwenye malengo hani kimahusiano, unapenda mavazi gani mpenzi wako avae yakuvutie, unapenda kuambiwa nini/ lugha gani itumike kitandani, unapenda uwe na mtu anayejitegemea au anayekutegemea, unapenda mpenzi wako awe ni mtu wa kwenda maeneo yapi, badala ya kuishi kwenye mawazo usiyotaka/ uliyokaririshwa?!

Sababu huwa inakera kuwa na mtu asiyejua anataka nini. Hamu naye inaisha haraka na mapenzi yanakuwa kama mnalazimishana badala ya kufurahia.

Kama we umashajijua ukweli wa ndani unataka nini, hautampa shida mpenzi wako kukuridhisha. Pia itakua rahisi kumpata unayeendana naye. Kwa kuwa hutokuwa na muda na mtu asiyejijua anataka nini.

Ni muhimu kujiuliza hayo kabla ya kuwa na mpenzi. Baada ya kujua unachokitaka ndipo uanze kutafuta mpenzi, lakini kama tayari unaye, mnaweza fanya hilo zoezi la kujuana pamoja badala ya kulazimisha mahusiano na kukaa kusubiri muujiza kwamba unatamani mahusiano/mapenzi yako yawe unavyotaka.

Nikutakie siku njema.
 
Back
Top Bottom