Kitu cha kushangaza kwa sasa iweje serikali iingilie Maamuzi Harmashauri ya Tarime? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kitu cha kushangaza kwa sasa iweje serikali iingilie Maamuzi Harmashauri ya Tarime?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by IsayaMwita, Aug 18, 2008.

 1. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #1
  Aug 18, 2008
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Ni baada ya wale wafanyakazi 8 wa halmashauri hii kutimuliwa na madiwani wakidhaniwa kuwa walihujumu sh, bilion 1, pesa za walipa kodi, sasa serikali imeamuru warudishwe kazini,hiyo imethibitika baada ya kupokea barua toka ikulu, jambo la kushangaza barua hii imebainisha kuwa madiwani wa Tarime walikosea kuwasimamisha kazi hao wafanyakazi,

  Swali la kujiuliza hapa ni vipi serikali ipinge maamuzi ya wale madiwani wakati hao ndiyo waliothibitisha upotevu huu wa pesa hizi?

  Kwani ikiwa jimbo linaongozwa na vyama pinzani maamuzi yake si sahihi kwa maslahi ya Taifa hili?

  Wana JF hili mnalionaje?
   
 2. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #2
  Aug 18, 2008
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Heshima kwako wa kwetu.
  Kinachofanyika hapa ni siasa mbaya sana, kama anavyoziita mh.Sitta, siasa za maji taka.
  Ni katika harakati za CCM kutaka kuwavunja nguvu wana mageuzi na wanademokrasia wa tarime lengo likiwa ni kutaka kulirudisha mikononi mwao jimbo la tarime.
  Si unakumbuka vile vi dola laki mbili uongozi wa wilaya na mkoa walivyo vikomalia!Cha ajabu ni kwamba kati ya halmashauri zote zilizopata hako ka mgao ka dola 200,000 ni tarime tu ndipo serikali kuu iliingilia kati kupinga matumizi yaliyokuwa yameidhinishwa na baraza la madiwani wa halmashauri ya tarime.
  Huu ni mkakati endelevu wa kuirudisha nyuma wilaya yetu kwa wivu wa kijinga kwakuwa wanaoiongoza halmashauri hiyo ni wana CHADEMA.
  Serikali inayowatetea mafisadi na wahujumu uchumi utaipata wapi katika dunia hii zaidi ya Tanzania, serikali ya CCM?
  Lakini ukweli ni kwamba hatutarudi nyuma, tutakwenda nao sambamba mpaka kieleweke!
  Vitisho vyao na ubabe wao mbona tumeshauzoea, na tunazidi kuimarika kila kukicha tunazidi kupata nguvu ya kukabiliana na maovu yote hayo.
  Na hao watumishi watafute mahali pengine pa kufanyia kazi, kwetu tarime hatuwezi kuwaruhusu waendelee kutufisadi.
   
 3. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #3
  Aug 18, 2008
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,844
  Likes Received: 1,110
  Trophy Points: 280
  Mkuu Isaya, natanguliza heshma. Inavyoonekana umelichukulia suala hili kwa munkari zaidi kuliko uhalisia wake. Ningependa kusema machache katika maeneo niliyopigia mstari.

  Kuhusu Madiwani kukosea, hilo no jambo linalowezekana kabisa. Madiwani katika Halmashauri nyingi wamekuwa wakifanya makosa katika kuwashughulikia watumishi wanaotuhumiwa kwa makosa mbalimbali. Kanuni za nidhamu zipo wazi. Na hiyo barua ya Serikali kuu ni lazima itakuwa imeeleza mahali walipokosea madiwani.

  Kuhusu kuthibitisha kosa, kanuni za nidhamu zinaeleza wazi kwamba mtumishi anaposhutumiwa kutenda kosa, anaandikiwa barua na Mkurugenzi kumtaka kutoa maelezo ya maandishi ndani ya siku 14. baada ya hapo, Mkurugenzi anatakiwa kuunda kamati ya maafisa wenye vyeo vya juu kuliko mtumisha anayetuhumiwa. Taarifa ya Kamati hiyo inaweza kuthibitisha kosa la huyo mtumishi au kupendekeza hatua za kuchukua. Hivyo ni vigumu kuamini kwamba madiwani walithibitisha upotevu wa fedha (ipo nje ya kanuni).

  Suala la ubaguzi, hii si kweli ni inferiority feelings. Serikali imekuwa ikipinga maamuzi ya Halmashauri nyingi pale inapoona maamuzi hayana maslahi kwa Taifa. Kumbuka Serikali Kuu kwa kupitia TAMISEMI inaweza kupinga uamuzi wa Serikali ya Mtaa (Halmashauri) pia inaweza kuivua mamlaka Halmashauri na kuipatia taasisi nyingine kadri itakavyoonekana inafaa. Kumbuka yaliyotokea Dar miaka ya nyuma. Serikali imewahi kupinga maamuzi ya Halmashauri za Singida, Songea nk juu ya kuwasimamisha watumishi pasipo kuzingatia kanuni.
   
 4. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #4
  Aug 18, 2008
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,523
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180

  Mkuu heshima mbele.

  Naunga mkono hoji yako juu ya uamuzi wa serikali wa kuwarudisha kazini watumishi hao. Hata hivyo kwa waliowahi au wanaofanya kazi kwenye hizi Halmashauri watakubaliana nami kuwa Madiwani wamekuwa kikwazo kwa utawala wa Sheria katika Halmashauri zao aidha kwa sababu ya umbumbumbu wa Sheria au kwa kuongozwa na jazba zinazosababishwa na visasi. Utakuta Sheria imeweka utaratibu mzuri tu wa namna ya kushughulikia matatizo ya wtumishi wanaokikuka sheria na taratibu lakini wao hukurupuka na kutoa uamuzi bila ya kuzingatia utaratibu uliowekwa na Sheria.

  Mkuu Isaya kama ukipata fursa ya kuziona hizo barua za kuwarejesha ni lazima utakutana na sentensi ya maneno "UTARATIBU WA KUWACHUKULIA HATUA ULIKIUKA SHERIA"

  Hapa ndipo zinapoliwa Halmashauri nyingi kwani waweza kuta ni kweli kuwa kosa limetendwa na watumishi lakini zimetumika njia wrong za kuwashughulikia.

  Hili ni tatizo kwa Halmashauri zetu hata na Taasisi nyingi za Umma hapa nchini.
   
 5. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #5
  Aug 18, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  zipo kanuni za utumishi wa umma ambazo zinapaswa kufuatwa katika masuala haya. si suala la madiwani kukaa tu na kuamua kumfukuza mtu kazi. kwani hao madiweani walikuwa mwajiri wa watumishi hao? wamepata wa[i nguvu za kuwafukuza kazi?
   
 6. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #6
  Aug 18, 2008
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mpita Njia,

  Ilikuwaje hao Madiwani wakapata nguvu ya kuwasimamisha kazi hao watumishi? lakini mbona imekuwa muda mrefu(miaka 3?) sawa lakini ni sheria gani hiyo itayomrinda MWIZI?

  Lakini hatupati shida, yaani haka ni kakichocheo tu, CCM mna kazi kweli kwa sasa,

  Tunashukuru kwa kutufundisha utawala wa sheria,

  Hebu hapa Tarime tuna Madiwani wangapi wa upinzani?

  anayejua idadi yao naomba aje kajibu.
   
Loading...