Kitu ambacho CCM haitaki ujue, lakini leo nitakujulisha! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kitu ambacho CCM haitaki ujue, lakini leo nitakujulisha!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Nov 20, 2008.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Nov 20, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kitu ambacho CCM haitaki ujue ambacho leo Utakijua!

  Makala iliyotoka Tanzania Daima Jumatano 19 Novemba, 2008


  Kama wewe ni mwanachama au umewahi kuwa mwanachama wa Chama cha Mapinduzi usiendelee kusoma makala hii. Unaweza ukajikuta unashikilia “Roho Mkononi”. Makala hii imewalenga wale wote ambao hawajui siri kubwa ya CCM siri ambayo leo nitaifunua. Kwa vile wana CCM wenyewe wanaijua siri hii hivyo kitendo changu cha kuiweka hadharani leo ni kama vile mtu kutoboa siri ya sanaa ya mazingaombwe na kuvunja mwiko wa usiri unaotawala fani hiyo. Hivyo, kwa wale wana CCM mtajitendea hisani kubwa kama utaacha kuendelea kusoma makala hii kwa sababu kuendelea kuisoma kunaweza kukusababishia chuki, hasira, kero, n.k dhidi ya mwandishi. Ni onyo hilo.

  Chama cha Mapinduzi kinataka wananchi wajue mambo mengi sana. Kinataka wajue kuwa ni chama safi, ni chama ambacho kinapigana na ufisadi, na ndicho ambacho kimefungua milango ya “maendeleo” nchini. Kinapenda wananchi “wafumbue macho” na kuona mafanikio ya aina mbalimbali ambayo yametokea nchini chini ya utawala wa serikali yake. Mara nyingi viongozi wake wamekuwa wakisisitiza kuwa asiyeona maendeleo ambayo yametokana na utawala wa CCM basi huyo si mkweli kwani mtu yeyote anaweza kuona maendeleo hayo na kuyahusisha na utawala wa Chama cha Mapinduzi. Haya yote serikali ya CCM inataka ujue.

  Hata hivyo kuna mambo ambayo CCM haitaki wananchi wajue kwani ni kama siri ya familia ambayo haitakiwi kutoka “nje” mitaani. Ni kama vitu vinavyofanywa “Nyuma ya Mapazia”. Ni jambo la siri kubwa ambalo endapo Watanzania watalijua kwa hakika linaweza kusababisha matatizo makubwa kwa chama cha Mapinduzi. Jambo hili CCM inajitahidi kila kukicha kulificha kama mtu afichaye hazina aliyoipata kwa taabu. Hivyo juhudi zozote za kutoa siri hii ambayo CCM haitaki itoke na kupokelewa zitakumbana na upinzani mkali, kejeli, vitisho, dharau na hata uadui wa wazi. Hiki wanachokificha ndiyo siri kubwa ya familia ya CCM, siri ambayo leo tutaiweka wazi ili wananchi wajue nini kinaendelea.

  Chama cha Mapinduzi hakitaki wananchi wajue kuwa ni kutokana na uongozi wake, sera, utendaji, na mwelekeo wake ndio sababu ya kuwa na migongano tunayoishuhudia leo hii kitaifa. Ni kutokana na utawala wa CCM ndio maana hadi leo hii jiji la Dar-es-Salaam limeshindwa kuweka mfumo mzuri wa maji taka ambao ungeondoa kabisa tatizo la mafuriko katika barabara zetu na kulifanya jiji la Dar-es-Salaam kuendelea kupendeza siyo kwa majengo marefu tu yenye rangi nzuri lakini likiwa na mazingira mazuri na ya kuvutia hata wakati wa mvua! Kukosekana kwa miundo mbinu mizuri ya maji taka karibu miaka 50 ya utawala wa CCM ni matokeo ya Chama hicho na serikali yake. Hili hawataki watu wajue.

  Chama cha Mapinduzi hakitaki wananchi wajue kuwa tatizo la upatikanaji elimu ya juu nchini ni matokeo ya sera, na mwelekeo wa serikali iliyoundwa na Chama hicho. Leo hii tunavyozungumza yawezekana utakuwa umeshasikia kuwa baadhi ya wanafunzi au viongozi wa wanafunzi watakuwa wamefikishwa mahakamani au wanapangwa kufikishwa mahakamani kufuatia mgomo wa wanafunzi wa vyuo vikuu ambao umesababisha wanafunzi katika kampasi mbalimbali kutimuliwa.

  Matatizo ya elimu ya juu leo hii nchini hayakuletwa kama zinavyoletwa “Salamu toka Kuzimu”. Matatizo haya hayakutumwa na “Malaika wa Shetani” bali ni matatizo ambayo yametokana na uongozi wa kisiasa wa chama tawala cha Mapinduzi. Kwa muda mrefu sasa sisi wengine tumepigia kelele suala la bodi ya mikopo, na jinsi gani bodi hiyo imeoza na ina kila harufu ya ufisadi. Tulipopiga kelele baadhi ya watu walituona tuna “Roho ya Paka”. Walituona kama watu ambao tunajaribu kutafuta sifa au kujaribu kudhalilisha watu fulani fulani.

  Hata hivyo miaka miwili baadaye ukweli unazidi kudhihirika kuwa serikali ya CCM imetelekeza elimu ya juu na badala yake imeaiacha idode kwa kufuata sera ambazo hazifanyi kazi, za kibabe na ambazo msingi wake ni ubaguzi wa hali ya maisha ya watu. Mara nyingi msemo wa viongozi wa serikali ya CCM ni kuwa leo hii Tanzania hatuwezi kutoa elimu ya juu bure. Kuna baadhi ya watu wanataka watu waamini hivyo. Ukweli ni kwamba bado Tanzania tungekuwa na viongozi wazuri, wenye maono ya mbali, na wenye ujasiri wa maamuzi tungeweza kabisa kutoa elimu ya Juu kwa kila kijana wa Kitanzania. Tatizo la elimu ya juu nchini siyo suala la uwezo hata kidogo bali ni suala la uamuzi.

  Leo Chuo Kikuu kimefungwa, wanafunzi wametimuliwa na serikali inajisifu kwa kukaza uzi ule ule. Hata hivyo wanachokifanya kinajulikana nacho ni kuwa serikali ya Chama cha Mapinduzi haina nia ya kutatua matatizo ya elimu ya juu. Nimebahatika kuona ripoti iliyotathmini matatizo ya taasisi za elimu ya juu ambayo ilikuwa imekusudia kutafuta chanzo cha migomo mbalimbali ambayo imekuwa ikijirudia rudia mara kwa mara. Mara nyingi migomo hii imewafanya wanafunzi wa vyuo vyetu vya elimu ya juu wajisikie kama vile wamo “Mikononi mwa Nunda”.

  Ripoti hiyo ambayo unaweza kuisoma kwenye mwanakijiji.com inaeleza kwa undani kabisa hali ilivyo kwenye vyuo vyetu vikuu na kutoa mapendekezo ya hatua gani zichukuliwe kukabiliana na matatizo mbalimbali. Hata hivyo kama ilivyokuwa ripoti nyingine zinazotolewa na serikali ya CCM ilibakia kuwa ni ripoti tu ambayo haijafanyiwa kazi inavyostahili. Hii iripoti ilikabidhiwa kwa Waziri tarehe 1 Juni 2004. Leo hii miaka minne baadaye ripoti imefichwa kabatini na serikali ya CCM inaendelea kutumia mabavu ya kunyamazisha sauti za wanafunzi.

  Kitu ambacho serikali hii haitaki watu wajue ni kuwa haina uwezo, nia, au ujasiri wa kukabiliana na matatizo ya elimu ya juu nchini. Ni rahisi zaidi kwa viongozi wa serikali kutumia nguvu ya polisi na kukamata watu usiku na kuwapeleka mahakamani kwa mbwembwe kuliko kukokaa chini na kukabiriana na matatizo ya wanafunzi.

  Ushahidi mzuri ni jinsi gani walishughulikia suala la wale vijana wetu waliokwama Ukraine karibu mwaka mmoja na zaidi uliopita ambapo serikali ya Kikwete iliamua kuwasusa na kuwarudisha nyumbani kwa nguvu. Ni wakati ule ndipo nilipotambua wazi kabisa kuwa hatuna viongozi wenye uwezo wa kutatua matatizo hasa ya elimu ya juu zaidi ya viongozi wababe ambao wanapenda kutumia vitisho na kushindwa kwa hoja. Hili CCM haitaki wananchi wajue.

  Leo hii tunaishi kama tuko kwenye “Dimbwi la Damu” ya ufisadi. Ukiangalia kwa haraka haraka unaweza kufurahia kusikia watuhumiwa wa wizi wa fedha za EPA wamefikishwa mahakamani. Kuna watu ambao wanatarajia wananchi watoe pongezi au kuonesha kuridhika na viini macho hivyo. Ukweli ni kuwa serikali ya CCM haijaamua kushughulikia matatizo ya Benki Kuu na ufisadi uliokithiri pale na matokeo yake wamechagua “ka akaunti” ka EPA kuwa kama geresha ya utawala wa sheria.

  Serikali hiyo hiyo inajua kabisa ni mambo mangapi ya kifisadi yametokea Benki Kuu na ambayo hata kuanza kuyachunguza hasa haijaanza. Suala la Mwananchi Gold, Deep Green Finance, Meremeta, Minara Miwili ya Benki Kuu ni mfano tu wa matatizo ambayo gharama yake ni mara nyingi ya “tujisenti” tulichochotwa Benki Kuu. Leo hii serikali hiyo inapendekeza shilingi bilioni karibu 70 zipelekwe kwenye kilimo badala ya kupeleka kwenye elimu. Hivi kuna ubaya gani kwa serikali hii kuamua kupeleka fedha hizo kwa wanafunzi ambao wako chuoni sasa hivi na kuondoa hii haya angalau kwa mwaka huu ya kukosekana kwa fedha za kuwasomesha vijana hawa?

  Hili serikali ya CCM haitaki wananchi wajue.

  Chama cha Mapinduzi na serikali yake kimeshindwa kuonesha uongozi wa msingi katika kuleta matumaini kwa wananchi hasa kwa kusimamia utawala wa sheria. Leo hii sheria zetu zinafanywa zionekane kuwa ni za upendeleo kwa watu wachache huku watu wengine wakijifanya kuwa ni miungu watu.

  Mara kadhaa mwaka huu jeshi letu la Polisi ambalo liko chini ya serikali inayoongozwa na Chama cha Mapinduzi limeendelea unyanyasaji wa wananchi kwa kukamata watu kinyume na sheria na kuwaweka kizuizini. Nakumbuka vizuri walivyokamatwa vijana wa jamiiforums.com mapema mwaka huu, na ninakumbuka walivyokamatwa vijana kule Kyela kwa kuja na mabango ya kumpinga Mwakipesile kwenye mkutano wa Rais Kikwete. Nakumbuka jinsi yule mlemavu alivyosekwa lupango kwa kosa la kutaka kufuatilia ahadi ya Rais wake.

  Siku ya Jumamosi na Jumapili jeshi hili ambalo linaongozwa na serikali ya Chama cha Mapinduzi liliamua tena kwenda kuwakamata na kuwashikilia wale inaodhania kuwa ni wachochezi wa mgomo wa wanafunzi nchini. Liliwashikilia katika namna ya kificho huku likigoma kuruhusu ndugu au jamaa wa vijana hao kujua walipo. Hata mkuu wa Upelelezi wa Kanda Bw. Mkumbo alipofuatwa kuelezea walipo kina Mtatiro aliwakwepa na kuwagandisha ndugu za Mtatiro bila kuwaambia ndugu yao anashikiliwa wapi.

  Ina maana kuwa katika utawala wa serikali hii ya CCM bado wananchi wanaishi kwa hisani ya watawala kwani watawala kwa kutumia vyombo vyao vya dola wamejishawishi kuamini kuwa wanaweza kufanya lolote lile, kwa mtu yeyote yule na jaribio lolote lile la kuwahoji litachukuliwa kama ni “kupanda chuki, kuleta uchochezi na kutishia amani”!

  Ndugu zangu hata mgomo huu wa walimu ambao kama ungefanyika ulivyopangwa ungetetemesha nchi nzima unathibitisha tu kile ambacho wengi tayari wanakijua (ingawa wenyewe hawataki wajue kuwa tunajua) ni kuwa serikali ya CCM ndiyo chanzo cha migomo hiyo kwani ni wao pekee wenye uwezo wa kutafuta suluhisho la kweli (kama walivyofanya siku ya Jumatatu). Hivi ni kwanini hadi watu watishie mgomo ndiyo uhakiki wa madai ya walimu unafanywa tena kwa kasi ya ajabu? NI kwanini hadi watu watishie migomo ndio serikali inaingilia Shirika la Reli? Je wakati umefika sasa kwa watumishi wa ATCL nao kugoma ili serikali iingilie kati? Je wakati umefika kwa wananchi wa Tabora kuanza kuandamana labda serikali itakumbuka kuna watoto 19 waliokufa kizembe kwenye jengo la NSSF?

  Wakati umefika tusizungushane na kuhadaiana; kama mafanikio yaliyopo leo Tanzania ni matokeo ya sera nzuri na uongozi mzuri wa CCM basi matatizo yaliyopo nayo ni lazima wawe tayari kuyakubali kuwa yametokana na sera na uongozi wao mbaya. Haiwezekani kocha apewe sifa wakati timu imeshinda lakini wakati timu ikifungwa tuanze kulaumu wachawi!

  Chama cha Mapinduzi ndicho kinahusiana moja kwa moja na utendaji kazi wa taasisi za serikali. Taasisi hizi zile ambazo unaweza kuziona hata “Dar-es-Salaam Usiku” zote zinahusiana moja kwa moja na Chama tawala.

  Hata hivyo swali kubwa ambalo sisi sota tunakabiliwa nalo ni kuwa kama kweli tunataka kuikabili CCM kama ilivyo na kuweza kuisababisha ibadilike yawezekana tukarudi na akili zetu, lakini je “Tutarudi na roho zetu”?

  Kama itakuwa hivyo nina uhakika Watanzania wote siku moja watatambua ni kwa kiasi gani Chama cha Mapinduzi kimekwaza kasi ya mafanikio na maendeleo ya Taifa letu. Na siku hiyo ambapo Watanzania wataoweza kuibadili CCM kwa chama kingine kuweza kushika hatamu za uongozi wa Taifa hapo ndipo kwa hakika sisi sote tutafurahia “Zawadi ya Ushindi”. Ushindi ambao wengi wetu tunauongojea na kuufanyia kazi; ushindi ambao kwa hakika utakuwa ni ushindi mnono tena mtamu.

  Hii ndiyo siri; siri ambayo Chama cha Mapinduzi hakitaki wananchi wajue kuwa matatizo yanayotokea sasa ambayo tukiyaorodhesha yatajaza juzuu ni matokeo ya utawala wa Chama cha Mapinduzi. Wananchi watambue kuwa wakati wowote viongozi wa CCM wanajaribu kukana kuwa CCM haijamtuma mtu kufanya ufisadi wanajaribu kuruka kitu ambacho hakiwezekaniki. Ni rahisi kwa mama kumkana mtoto wake kuliko kwa CCM kukana ufisadi nchini. Ni mpaka watakapokubali kuwa wao ni sehemu ya tatizo hapo ndipo Chama cha Mwalimu kitakapoanza kweli kujisafisha kutoka ndani. Kwa sasa hivi, hawataki kujiangalia kuwa yawezekana tunachokiona huku nje ni dalili tu ya kile kilichomo ndani.

  Nimeiandika kwa kumbukumbu ya Mwandishi mahiri ambaye ni kutokana na kazi zake alinifanya nipende kusoma vitabu na kuandika hadithi mimi mwenyewe. Hii ya leo ni kumbukumbu ya Gwiji wa Riwaya Marehemu Ben R Mtobwa. Kuanzia kesho hadithi yangu ya “Mtikisiko” itaanza katika mfululizo kwenye MwanaKijiji.COM - Home. Karibuni.

  Niandikie: mwanakijiji@mwanakijiji.com
   
 2. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #2
  Nov 20, 2008
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Naomba nitoe ufupisho wa siri hiyo kubwa;

  CCM ni chanzo cha matatizo yote tuliyonayo Tanzania na pia ya husika na mafanikio yanayoonekana.

  Sasa tupime; Leo hii hapa Tanzania ukiweka mzani kupima mambo hayo mawili Matatizo na Mafanikio kwa zaidi ya miaka 45 ya uhuru, upande gani utaelemewa? Basi huko kutakako elemewa ina maana CCM ndiyo kipimio halisi cha uwezo wake!
   
 3. Kuntakinte

  Kuntakinte JF-Expert Member

  #3
  Nov 20, 2008
  Joined: May 26, 2007
  Messages: 704
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mkuu heshima mbele,

  Hapa umemaliza mwana yaani Nyundo Utosini
   
 4. t

  tarita Senior Member

  #4
  Nov 20, 2008
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 156
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mwanakijiji,
  Naona unataka kufukua mambo. Kwamba ni kwa nini fedha za EPA zipelekwe kwenye kiini macho cha kilimo,narudia kiini macho cha kilimo
  Kumbuka kashfa ya Richmonduli ilanza vipi.UTAGUNDUA.
  Sasa hivi kuna mikakati ya kufufua kiwanda cha mbolea cha Mijingu kilichoko kule Arusha.Serikali imeisha peleka bilions eti kukifufua.ULIZA. Nani mwekezaji wa kiwanda hiki.Kama ilivyo kwa mwekezaji katika reli ya kati ,kwa nini mwekezaji apewe mamilioni ya umma?!!!WIZI TU MWINGINE WA KINAMNA.
  Ebu tufanya namna ili tuifahamu ghiliba hii.

  MAANA yake ni kwamba hizo hela za EPA zipelekwe kwenye kunua mbolea.UNAIPATA hiyo?!!Mwenye kiwanda hajulikani.Ebu fanya uchunguzi utajuwa.

  PESA za EPA ZIRUDI KULEKULE .Kutoka kushoto kwenda kulia.SUBIRI mwone
  wenye akili TUMEISHA JUWA.Waziri mkuu PINDA analijuwa hili pamoja na la Reli ya kati au anatumiwa tu!!
   
 5. SaidSabke

  SaidSabke JF-Expert Member

  #5
  Nov 20, 2008
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 1,968
  Likes Received: 222
  Trophy Points: 160
  Kumbe wa JF wengine huongea busara. Tatizo watu wengine hulaumu bila kutazama upande ungine wa shilingi.
   
 6. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #6
  Nov 20, 2008
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mwanakijiji

  Heshima mbele, makala mzuri.

  Wananchi sio kama hawaoni au hawaelewi hayo matatizo.

  Wananchi walio wengi hawaoni chama mbadala kwa CCM. Wananchi wa Moshi Mjini, Tarime, Karatu, Kigoma, Pemba n.k wao wameona vyama mbadala, hao wengine bado....tuwape muda huku tukiendelea kuwaelimisha kama hivi.

   
 7. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #7
  Nov 20, 2008
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Ni changamoto kwa washikadau wa upinzani......! 2010 wajitahidi kusimamisha watu makini kwenye majimbo yaliyosalia...wana nafasi kubwa sana ya kuibuka na ushindi.........!
   
 8. K

  Kakulwa Senior Member

  #8
  Nov 20, 2008
  Joined: Oct 10, 2008
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  hizi hoja ndiyo tunazozijadili hapa JF kila siku.Sasa siri yenyewe iko wapi?
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Nov 20, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  hivi makala imesema siri ambayo JF hawaijui? Ni siri iliyoko hadharani lakini CCM haitaki watu waione na kuikubali. Lakini kuna watu ambao wanaamini kabisa kuwa matatizo yao yanatokana na "Utendaji mbaya" au "mafisadi" au "Mtu binafsi" lakini hawayahusishi na Chama tawala.
   
 10. P

  P. Mwainunu New Member

  #10
  Nov 20, 2008
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwanakijiji nakuheshimu kwa threads unazotoa lakini hapa hakuna siri hata watoto waliohojiana na Mkuu wa wilaya uso kwa uso wanayajua yote haya na zaidi ya hayo. Mimi ninachoomba wakina Slaa, Zitto na wengine wazidi kusonga mbele na vijana na wakina mama wengi wafumbue macho na kuona, wazibuke masikio na kusikia hapo ndipo mwisho wa dude hili liitwalo CCM litakapomongonyoka.
   
 11. Ukweliii

  Ukweliii Member

  #11
  Nov 20, 2008
  Joined: Feb 10, 2008
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huo ndio ukweli.
  Unafanana kabisa na mengi yanayojitokeza na yajayo waweza kuhisi...

  Waandishi wa habari wakombele sana kukosoa na kuweka ukweli wazi... lakini
  Ukija uchaguzi CCM wanashinda

  Mjadala wa kidemokrasia ni namna gani hoja hizi zinageuzwa kuwa kura
  vinginevyo tutakuwa tuna "mpigia mbuzi gitaa..."
   
 12. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #12
  Nov 20, 2008
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mkjj, umegusia mengi ya muhimu kwenye nakala yako ambayo yanabidi kufichuliwa zaidi au kuwekwa pamoja na kuonesha chanzo cha matatizo haya, yaani CCM. Na ninakubaliana nawe, akhsante. Lakini kwa vile hiyo nakala umeashiria kuwa imewekwa kwenye gazeti pia; najiuliza, iwapo nakala kama ilivyo juu imechapishwa hivyohivyo, je kweli mhariri mkuu wa gazeti la Tanzania Daima anahariri kazi yako kabla ya kuichapisha?! Najua makosa katika uandishi huwa yapo na nivigumu mtu kuandika bila hitilafu za hapa na pale, haswa kwa watu ambao hatujasomea fani ya uandishi.

  Basi mkuu, kutoka kwenye nakala yako naona umezidisha kutumia nukuhu za misemo au mafumbo. Nadhania kabisa kuwa ungeweza kuipunguza au pahala pengine haikuwa inahitajika maana tafsiri au mantiki zake zinajulikana tayari katika jamii. Kingine kinachoendana na hiki ni matumizi yako ya punctuation marks. Kama nilivyosema hili ni tatizo la wengi wetu, ila kwa vile unaandika articles ambazo zinachapishwa katika jamii basi nilitegemea kuwa mhariri mkuu angezidi kukujenga na kukuimarisha zaidi kwa kukusahihisha na kukujulisha pale unapofanya makosa, ili kwenye nakala za majuma yafuatayo zisiwe na makosa yaleyale. Kwa kweli mkuu kama anayaona makosa yako katika uandishi halafu hakusahihishi na kukujulisha atakuwa hakutendei haki na hawatendei haki wasomaji wa gazeti pia.

  Kingine cha nyongeza ni kule kupendelea kurefusha nakala. Kwa vile umesema waziwazi mara kwa mara jinsi vile unavyopenda uandishi, bila shaka utakuwa na style yako kwani kila mwandishi ana style yake ya uandishi. Hata hivyo jambo ambalo nadhania linapaswa kukumbukwa na kuzingatiwa ukiwa mwandishi ni kule kuepuka kuchosha wasomaji wako. Kwenye habari zinazolenga mustakabali wa Taifa letu moja kwa moja ambazo wengi tunakutegema kwa umahiri wako, kujituma kwako, uzalendo wako na nyenzo mbalimbali ulizonazo, basi hili iwe moja ya changamoto kwako. Usizirefushe sana mkuu pasipo lazima.

  Nyongeza ya mwisho kama pendekezo kwako Mkjj. Nafikiria ingekuwa vyema zaidi kama utapata muda na kuandika riwaya walau fupi katika kumuenzi na kuweka kumbukumbu kwa kinara na rafikiyo aliyetutoka, marehemu Mtobwa. Hata hivyo kwa jinsi nikusomavyo, naamini uko njiani kuandika a more reflective dedication. Unisamehe kama nimekukwaza mkuu, ni maoni yangu baada ya kusoma post yako hapo juu. Shukrani.

  SteveD.
   
 13. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #13
  Nov 20, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  mBONA HUJAZUNGUMZIA OIC?
   
 14. L

  Lione Senior Member

  #14
  Nov 20, 2008
  Joined: Dec 1, 2007
  Messages: 115
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Jamani,
  naamini wengi tumeisoma hio makala,jamaa(mwanakijiji)amesema siri iliyo wazi,kama siri iko wazi,kune wengine hawaiona,kuna wengine hawailewi,kuna wengine hawaijui kama ndo hii,ndio maana,huyu mwana kijiji akachukua jukumu lakiuitoa kabisaa nje,nini sebuleni,ili wale wavivu hata wa kuingia varandani,sebuleni,waweze kuiona,si mtetei mwanakijiji,lakini katika hili,namshukuru,kwa kuwasaidia vipofu,na viziwi weengi,barvo mwanakijiji.
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Nov 20, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Umeanza lini kunichagulia vya kuzungumzia?
   
 16. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #16
  Nov 20, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280

  Nimechukulia kila neno, pendekezo, ushauri na hoja moyoni. Nitajitahidi kurekebisha kasoro hizo. Asante sana na ningependa pia kusikia ukosoaji wa watu wengine kuhusu uandishi wangu. Umenisaidia kuliko unavyoweza kufikiri. You are a true friend. Usengwile dadi, havache na Mulungu akuhenje, ndaga fijo na lori nkamu gwangu, Wabecha bangosha, danke, thank you!
   
 17. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #17
  Nov 20, 2008
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hizi bifu mpaka lini??????????
   
 18. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #18
  Nov 20, 2008
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Vema kabisa,

  Mwenyewe nilipoiona nika-scroll kwenda chini nikaona ndefu nikaahirisha kuisoma, nilipokaa na kutafakari nikaona sina tofauti na jamaa anayesaini mikataba bila kuangalia content ndani yake (recall Buzwagi), nikarejea na kuisoma. Imeandikwa vema lakini kama alivyodokeza SteveD basi jaribu kupunguza urefu wake kwani sisi (watanzania) japo twaongea kwa kirefu lakini kusoma twataka kwa kifupi.

  :)
   
 19. c

  care4all Senior Member

  #19
  Nov 20, 2008
  Joined: Feb 25, 2007
  Messages: 103
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Usanii hauko CCM tu, hata huku kwenye upinzani nako wanakatisha tamaa...tunacheza na watu wale wale miaka yote harafu tunatarajia mabadiliko..Naomba kama kuna anayejua sera ya chama chochote cha siasa Tanzania kilicho toa mchanganuo wa kina namna watakavyo kuza Elimu (hasa ya juu), Kilimo, technolojia na afya atuwekee hapa tuchambue. Vyama vyetu vya siasa havina tofauti sana na timu zetu za mpira na hata tunavyo ongelea vyama kama vile tunatwanga story za Yanga na Simba. Kila chama kina mafundi wake kama vile zilivyo vilabu vya mpira....Hi ndio imetu cost wanyonge wa Tanzania na itaendelea kutu cost daima..wengine tunakimbilia kupamba majina ya watu au vyama kishabiki tu, labda kuna wanaonufaika moja kwa moja kama siyo kuwatengenezea watu wachache ulaji tu, lakini je ni chama gani chenye nia yadhati ya kumkomboa mlalahoi and HOW? At least Mr. Mrema (in my opinion) tried and he will be remembered one day...they way I see it, we just have political teams not parties,paparaz being part of political game, no technical know how but technical know who.
   
 20. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #20
  Nov 20, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  I have always raised "wordiness" as an issue with Mwanakijiji.Economy of words is an area that needs improvement, otherwise you will lose a lot of readers.

  It is not necessarily due to readers lazyness some people can get through the length of Tolstoy's "War and Peace" and Gibbons "The Decline and Fall of Rome" not to mention the history of having gone through the entire bible forward and backwards by age 10, so some can read when they want to.

  But one has to make a choice between a lot of reading, the complete works of Shakespeare, WSJ,NYT, The Nation, The Economist, Columbia Journalism Review, US News and World Report, Newsweek, Time, IPPMedia, Mwanakijiji.com you get the idea. And the choice must be justified, and I find some of your posts to be unjustifiably long.

  The challenge is, to say the most using the least amount of the most effective words.
   
Loading...