Kitine: Kuna waziri ameiba fedha za nchi huko nje ametia mfukoni mwake kutafutia urais | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kitine: Kuna waziri ameiba fedha za nchi huko nje ametia mfukoni mwake kutafutia urais

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tumaini Makene, May 5, 2012.

 1. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #1
  May 5, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,617
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Wazee wawili wastaafu wa nchi hii wako Channel Ten kwenye kipindi cha Je Tutafika. Nafikiri leo ndiyo siku yake (kama si marudio). Ni Dkt. Hansy Kitine na Dkt. Kiwanuka.

  Mada ni uadilifu na uwajibikaji serikalini. Mzee Kitine kama kawaida yake...leo anasema anashangaa inakuwaje watu wachafu wameendelea kuteuliwa katika nafasi ya uwaziri baada ya MSUKO (hii yangu) mpya wa jana.

  Anasema mathalani kuwa waziri mmoja amepewa fedha za nchi huko Comoro, Moroco na Libya, ametia mfukoni mwake. Amezifanya ni za kwake. Waziri huyo kwa sasa anajenga au kamaliza kujenga hoteli kubwa katika makao makuu ya moja ya mikoa ya Kusini mwa Tanzania.

  Mzee Kitine anashangaa, anasema sasa huyo waziri anausaka urais, sasa kama sasa ni fisadi akiwa rais atakuwaje, ataacha kwa sababu kapata urais aliokuwa anautaka.

  Kipindi ni kizuri. Wazee wanajenga hoja vyema juu ya uwajibikaji wa serikali na viongozi kwa wananchi. Kiwanuka anasema uongozi wakati wa Mwalimu ilikuwa ni utumishi. Unatumikia watu, si watu wakutumikie wewe.
   
 2. F

  FJM JF-Expert Member

  #2
  May 5, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Tumaini, nadhani watu wanamvutia pumzi tu huyo waziri!
   
 3. M

  Molemo JF-Expert Member

  #3
  May 5, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Mbona kama anamzungumzia waziri wa mambo ya nje kwa mafumbo.
   
 4. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #4
  May 5, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  Bila shaka anamsema Membe!

  Hofu yangu isije ikawa ni kulipiza visasi...lakini kama anasukumwa na uzalendo, then well and good!!

  Kwanini nasema isije ikawa visasi?
  Nakumbuka ni Waziri Membe ndie ambae aliibua kashfa ya Hans Kitine kutumia mamilioni ya shilingi huko Washngton isivyo halali. Kama sikosei, suala lenyewe lilikuwa linahusiana na matibabu. Enzi hizo ni watu wachache sana walikuwa wanamfahamu Bernad Membe, kwani alikuwa ni mbunge tu kupitia jimbo la Mtama.
  Kama kumbukumbu zangu zipo sawa, ni kashfa hiyo ndiyo ilisababisha Hans Kitine kujiuzuru uwaziri!
   
 5. N

  Nteko Vano JF-Expert Member

  #5
  May 5, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 436
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Haswa nafikiri anamzungumzia Membe. Watu wa mambo ya nje mliopo humu tuleteeni data hapa JF.
   
 6. frema120

  frema120 JF-Expert Member

  #6
  May 5, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 5,103
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Yap! kamsema membe sanaaa, wanamalizia sasa channel 10
   
 7. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #7
  May 5, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Siasa za kuchafuana tu hizo hamna jipya hapo!

  Hakuna serikali inayotoa msaada kwa serikali nyingine kupitia account binafsi ya waziri, huo ni uongo na ujuha.
   
 8. F

  FJM JF-Expert Member

  #8
  May 5, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Ndio sababu tunaaswa tusirushe mawe wakati tuko kwenye nyumba ya vioo.
   
 9. U

  Ubongo Silaha Senior Member

  #9
  May 5, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 140
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Siku hizi uongozi ni Ulaji...ukiteuliwa umeula
  Utanunua nyumba ya dola 410,000
  Utaitwa mheshimiwa na sio ndugu kama wakati ule
  Utaharibu na hutajiuzulu hadi ZZK akusanye saini 70 bungeni ndipo mkuu wa kaya atishike na kuchukua hatua
  Caucus ya Chama haitakuandama hadi ule mwenyewe na wao uwanyime au uwazibie wenye madili yao kula (muulize Omari Nundu)
  Utafungua makampuni hewa ya kukagua magari na bila woga hadi leo utaendelea kuwa madarakani maana unajua anayepaswa kukuwajibisha ulimkatia mgawo hana ujasiri huo...labda ashinikizwe!
  Uongozi wa sasa ni dili kubwa ndio maana watu wanafanya sherehe wakiupata
  Hilo la utumishi wa umma wanajua Kitine na Kiwanuka na Warioba na Kaduma na kizazi chao... Wenzao hawajui hayo
   
 10. C

  CDM Member

  #10
  May 5, 2012
  Joined: Jan 19, 2012
  Messages: 73
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Sawa kabisa, anamsema Membe ndo alimchomoa uwaziri. Kitine naye Fisadi kama mwagwanda wenzake
   
 11. Whisper

  Whisper JF-Expert Member

  #11
  May 5, 2012
  Joined: Jun 2, 2009
  Messages: 502
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nimeona Kitine amemfagilia sana Gideon Cheyo, John Chiligati na Anna Tbaijuka kuwa ni viongozi wasafi. Mzee naona hana cha ku loose. Yaani kamchana Membe ki aina, yaani JK amesahau kutoa kasa lingine kwenye system.
   
 12. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #12
  May 5, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Uko sahihi kabisa naona mzee kitine hapa hasukumwi na uzalendo bali ni kulipa kisasi kutokana na membe kuongoza safu ya mashambulizi dhidi yake kipindi kile alipokuwa waziri tena wa utawala bora,alitumia nafasi yake kufanya ufisadi kwa kutumia fedha za umma kumpeleka mkewe akatibiwe ng'ambo lakini kina membe na kina mohammed abdul aziz nafikiri kwenye kamati iliyoundwa kuchunguza tuhuma za ufisadi wake wakagundua makubwa ikiwa ni pamoja na kugundua hospitali ambayo mzee kitine na mkewe waliwasilisha stakabadhi kuhalalisha malipo hewa ya matibabu ilikua ni hospitali ya mmbwa na si binadamu,membe akauweka hadharani bungeni ushahidi huo kwani alisafiri mpaka huko ughaibuni kufuatilia hiyo kashfa iliyomhusu bosi wake huyo wa zamani wakiwa TISS na inasemekana uhasama ulianzia huko TISS.
   
 13. F

  FJM JF-Expert Member

  #13
  May 5, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Tuko sahihi tukisema kuwa Membe hana tofauti na Dr Kitine?
   
 14. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #14
  May 5, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,617
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Mkuu sijui kama unajua unacho-argue. Nani kasema kuwa zimewekwa kwenye akaunti binafsi? Nway kwa maelezo ya Mzee Kitine anasema kuwa fedha zilizotolewa huko Comoro zilitokana na Tanzania kumsaidia 'yule jamaa mganga wetu' (hii ni yangu) kupambana na wale waasi waliopindua serikali.

  Zile za Morocco zinatokana na masuala ya kuwatambua Polisario. Anasema aliwaambia jamaa huko kuwa suala hili lina mchakato hivyo kuna fedha zinahitajika. Wakampatia. Juu ya Libya aliisema kwa mbali lakini hakusema ilikuwaje hasa...

  Kwani lini Mzee Kitine amekosa moral authority ya kuikosoa serikali hii na viongozi wake? Kwa wengi wetu bado anayo. Kwa wenye kumbukumbu wanajua kuwa alikuwa mtu wa kwanza kumtaja Jairo hadharani. Katika namna hii hii alivyofanya leo. Tuliokuwa tunaangalia kipindi siku hiyo tulijiongezea tukajua mzee anamaanisha nani. Leo yako wapi wakubwa.
   
 15. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #15
  May 5, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Frankly speeking huyu anaetajwa ni Benard Membe. Hotel anayojenga ipo Mtwara pembezoni mwa Bahari. Niliiona mwezi uliopita nilipokuwa Mtwara.

  TUMBIRI wa JF
   
 16. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #16
  May 5, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Tume ya katiba,
  Yani wewe hata mtu akikushtua flani anakuibia power window ya gari yako utaendelea kusema ni siasa za kuchafuana. Pole lo!

  TUMBIRI wa JF
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #17
  May 5, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,617
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Asante kwa maelezo mazuri. Lakini kumbukumbu zinaonesha kuwa tehn Kitine hakuwa waziri full. Alikuwa Naibu Waziri (I stand 2 b corrected). Je tuhuma hizo zilitosha kuondoa moral authority yake kuzungumzia masuala ya kuijenga nchi kwa kuweka sawa uongozi huu. Ikizingatiwa kuwa amewahi kuwa kiongozi wa sekta nyeti na muhimu (tena wakati huo kumbuka ilivyokuwa nyeti kweli).

  Lakini suala muhimu hapa, kwa hiyo ni sawa kusema kuwa Membe (kama ni yeye aliyemaanishwa katika kauli hiyo) na Kitine hawana tofauti. Maana ukiziweka vyema sentesi zako katika inferences unapata conclusion hiyo kuwa Membe (kama ni yeye waziri mhusika) na Kitine hawana tofauti, hivyo unakubali kuwa waziri aliyezungumzwa kweli siyo mwadilifu eeh?
   
 18. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #18
  May 5, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,343
  Likes Received: 1,810
  Trophy Points: 280
  Spies...never end their tales. Kila kukicha kuna jipya.
   
 19. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #19
  May 5, 2012
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Hujauma maneno.

  Picha za Hotel hiyo zitakuwa hapa JF soon!

   
 20. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #20
  May 5, 2012
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,276
  Trophy Points: 280
  Wote wezi hakuna wakulaumiwa wote siwasafi kwani naye Kitine alikwapua hera ya umma kwa udanganyifu hivyo naye simsafi,membe naye vilevile!!
   
Loading...