Kitinda Mimba WANAPODEKEZWA!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kitinda Mimba WANAPODEKEZWA!!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Nov 18, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 18, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,237
  Likes Received: 5,619
  Trophy Points: 280
  Kitinda Mimba  Eti vitinda mimba wengi hudeka sana?[​IMG] Wataaalamu wa masuala ya haiba na saikolojia ya watu wana mengi ya kusema kuhusu nafasi unayozaliwa katika familia (birth order) na athari zake.
  Ukweli ni kwamba watoto kuwa tofauti kitabia hutokana nafasi yako katika kuzaliwa (wa kwanza, katikati au mwisho) ktk familia, aina ya wazazi, idadi ya watoto na wakati mwingine mazingira na malezi.
  Kwa mfano ukizaliwa peke yako automatically utakuwa na tabia aidha za kifungua mimba au kitinda mimba.

  Kitinda mimba wengi huwa ni watu ambao wanajichanganya sana kwani tangu watoto huwa wanakuwa na hali ya kujihusisha na wengine na si watoto wa kuchungwa sana kama kifungua mimba hivyo huwa na ujasiri wa kufanya jambo lolote hata kama lina risk kubwa.

  Pia kitinda mimba huwa na tabia tofauti kwani wazazi huwa hawaelekezi nguvu nyingi kama kifungua mimba (hawako strictly sana) na pia kitinda mimba yeye siku zote hubaki mtoto tu kwani hana mwingine chini yake na kila analosema na kufanya kwa wazazi huhurumiwa kwa kuwa yeye ndo mtoto.

  Hawa vitinda mimba mara nyingi hupewa kila wanachohitaji hadi wanakuwa spoiled na matokeo yake huwa wanadeka sana.
  Pia hawa huwa hawaogopi maisha kila kitu hukiona rahisi tu hawana shida sana ya kuwaza kwamba maisha ni vita badala yake huona maisha kama zawadi tu ni kuishi.

  Je, unahisi kuoa au kuolewa na kitinda mimba huweza kuathiri ndoa kwa kiasi fulani?
   
Loading...