Kitimoto kilo moja watu tunafyeka lakini kilo moja ya nyama ya ng'ombe hatutoboi, tatizo liko wapi?

Vitu vinavyoonekana haramu ndo huwa vitamu ndugu.. ile ngoma ikikaangwa ukiulizwa hata jina lako unaweza kulisahau kwa muda.. yule kiumbe anakula hadi mbao au hata watoto wake.. lazima awe mtamu tu..
Na iendelee kuwa haramu ivyo ivyo ili tuendelee kufidi maana isingekuwa haramu hata bei yake ingekuwa mara dufu ya nyama na ingeishia kuwa mboga ya vigogo na masultani kwa utamu wake .
 
Wakuu ukienda ukaagiza Nyama kiti moto kilo moja unakula na kumaliza fasta hata wakati mwingne unatamani kuongeza, hebu piga Picha Nyama kilo moja ya ng'ombe huko nyumbani tunakula watu kumi na inabaki

Swali hivi kweli ile Nyama inakuwa ni kilo moja Au wanatuibia? Inakuwa kweli ni kilo moja ile Nyama ya kiti moto? Au wanatuibia? Au kuna sababu ingine?
Nikiagiza kilo moja huwa nakataa kama ni kilo moja, ila nusu kilo naamini
 
Nyama ya ng'ombe 1Kg humalizi? labda unakulaga nyama mbichi wewe

ila hujakutana na Beef Ribs zenyewe zilizopikwa kwa viwango vyote

hapa naongelea vitu za namna hiii

chefkile_83126698_250792039237256_7846878158615027930_n.jpg
chefkile_87217423_244759396519245_3616692873406430241_n.jpg


Hizi vitu sio tu ukila unamaliza kilo 1 ila unaweza ukajikuta unakula kama

yule jamaa wa kwenye JAMBO NA VIJAMBO.
 
Back
Top Bottom