Kitilya asota rumande miaka 2

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
19,074
42,852
IKIWA ni zaidi ya miaka miwili tangu aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya na wenzake kufi kishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wameendelea kusota rumande kwa sababu upelelezi bado haujakamilika.

Aprili Mosi 2016, Kitilya ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kampuni inayoshughulikia Uwekezaji wa Mitaji na Dhamana (Egma) pamoja na maofisa wawili wa Benki ya Stanbic akiwemo aliyekuwa Miss Tanzania (1996), Shose Sinare na Sioi Solomon ndio ilikuwa mara ya kwanza kufikishwa mahakamani hapo na kusomewa mashitaka nane ikiwemo ya utakatishaji fedha.

Hata hivyo, washitakiwa hao wanaendelea kusota rumande kwa sababu mashitaka ya utakatishaji fedha yanayowakabili hayana dhamana kisheria. Jana upande wa mashitaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Patrick Mwita alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba wanawasiliana na wachunguzi ili wajue upelelezi umefikia wapi.

Mwita aliieleza mahakama kuwa upelelezi bado haujakamilika kwani wanaendelea kuwasiliana na wachunguzi. Baada ya kueleza hayo, Hakimu Shaidi aliahirisha kesi huyo hadi Novemba 16, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na kuangalia kama upelelezi umekamilika ama la.

Washitakiwa wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka ya kula njama, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kutakatisha fedha. Wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Machi 2013 na Septemba 2015 wakati wa mchakato wa mkopo wa dola za Marekani milioni 550 kwa Serikali ya Tanzania kutoka Benki ya Standard Chartered Uingereza.

Wanadaiwa kuwa Machi 2013 jijini Dar es Salaam walijipatia dola za Marekani milioni sita, wakionesha kuwa fedha hizo zilikuwa ni malipo ya ada ya uwezeshaji upatikanaji wa mkopo na zililipwa kupitia Kampuni ya Egma T Ltd.

Washitakiwa hao wanadaiwa kutakatisha fedha kwa kuhamisha, kuchukua na kuweka dola za Marekani milioni sita katika akaunti tofauti za benki. Kati ya Machi 2013 na Septemba 2015, wanadaiwa kuwa waliweka fedha hizo katika akaunti mbalimbali zilizomilikiwa na kampuni ya Egma na kwamba walipaswa kufahamu kuwa fedha hizo ni mazao ya uhalifu wa kughushi.
 
Kwan Huyo Sioi Ndio Yule Mkwe Wa Lowasa Au Ni Mwingine! Ndio Yule Aliyegombea Ubunge Akashindwa Na Joshua Nasari? Sorry Lkn.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom