Kitila mwalimu wangu,kuwa mkweli utakuwa huru hata kwenye nafsi

RUTO

Senior Member
Dec 19, 2013
147
29
Mwalimu wangu Kitila Mkumbo hata kabla hujafukuzwa uanachama na chama changu CHADEMA,mimi nilikuwa mfuatiliaji mzuri wa makala zako katika gazeti la Raia Mwema. Hata baada ya kufukuzwa na chama, umeendelea kuandika lakini katika mtazamo tofauti. Eti unataka mbadala wa CCM na CHADEMA. Nakuunga mkono katika mbadala wa CCM lakini siyo CHADEMA. Na hii ni kwa sababu matatizo yanayoikumba CCM hayatibiki lakini ya CHADEMA yanatibika.Sababu ni kama zifuatazo:
1. CCM imepoteza ule mvuto wake kutokana na kuwa madarakanikwa muda mrefu
2. CCM imekithiri kwa rushwa kila idara yake na ndio maana kila aliye CCM yupo kimaslahi.
3. CCM imewasahau watendaji wake wa ngazi ya chini kiasi kwamba wanafanya kazi kwa kujitolea.
4. Kimekuwa chama cha matajiri na siyo cha wakulima na wafanyakazi
Sababu za kutohitji mbadala wa CHADEMA ni kama zifuatazo:
1. CHADEMA bado kina mvuto mkubwa kwa wanajamii kwani hakijawahi kuwa madarakani
2. CHADEMA kinadhibiti rushwa kwa dhati na kinawachkulia hatua watu wote wanaodhani wapo juu ya chama
3. CHADEMA kimeonyesha uwezo mzuri katika kusimamia halmashauri zilizoko chini yake.
4. CHADEMA kimeonyesha uwezo wa hali ya juu katika kuisimamia serikali bungeni.
5. CHADEMA kimekuwa chama chenye kutoa fursa kwa wote na haswa vijana.

Katika waraka waraka "Mkakati wa Mabadiliko 2013" ambao Mwl. wangu Kitila aliuhariri, anadai kuwa viongozi waasisi wa CHADEMA, yaani Mzee Mtei na Makani hawakuwa walafi wa madaraka kwa kuwa eti waliachia nafasi zao za uongozi wa chama baada tu ya kumaliza muhula wao wa kwanza. Ni sawa kabisa kwamba wazee hawa hawakuwa waroho wa madaraka, lakini Mwl. wangu utakubaliana na mimi kwamba waliachia madaraka katika harakati za kuangalia ni nani atakayeweza kuififikisha CHADEMA kule ilikotaka kufika kwa ufanisi zaidi. Na ndio maana kujenga hoja kwamba eti viongozi wa sasa ni waroho wa madaraka kwa kuwa hawakuachia madaraka kama walivyofanya waasisi wa chama ni ufinyu wa fikra kwani Mzee Mtei angekuwa mstari wa mbele kushinikiza viongozi wa sasa kuachia madaraka haswa ikizingatia baadhi ya watu waalio nyuma ya mkakati wenu Mwl. wangu wanadai Mzee Mtei anawachagulia viongozi.

Katika kutengeneza hoja kuwa kuna haja ya kuwa na mbadala wa CHADEMA siku mbili zilizopita Mwl. wangu Kitila aliandika post yake hapa na kuiposti hapa JF. Miongoni mwa mambo ambayo aliyazungumzia kuonyesha kuwa CHADEMA hakina tofauti na CCM hivyo kuna haja ya kuwa na mbadala wa vyote viwili ni kwamba viongozi wa CHADEMA wameendelea kupenda anasa kama walivyo CCM ambao wamekuwa wakiwatuhumu kwa mambo hayo hayo. Mambo hayo ni kama kuendelea kuendesha magari ya bei ghali na ya kifahari n.k. Sawa kabisa Mwl. wangu, lakini nikuulize kama kweli ulikuwa na nia ya dhati ya mabadiliko, mbona huyo huyo Zitto uliyemwona kuwa anafaa kuliendesha gurudumu la CHADEMA na anayeweza kukisafisha chama ndiye huyo huyo muumini wa fahari hizo hizo. Mwl wangu hukumbuki kuwa Zitto alishawahi kukiri yeye mwenyewe kumiliki magari ya kifahari kama Hammer na Range Rover? Hatusemi kwamba kaiba lakini kwa mwanasiasa kijana kama Zitto, tena kutoka kwenye nchi ya ulimwengu wa tatu asiyekuwa na biashara yoyote ni lazima tumtazame kwa macho ya mashaka.

Mwisho kabisa Mwl. wangu mbona ulikuwa mkali sana wakati ulipokuwa umeorodheswa katika ile ripoti ya MWENENDO WA ZITTO TANGU 2008 kwa kutajwa kupokea sh.200000/= kwa nyakati tofauti pamoja na Shibuda? Tena ikafikia hata kuituhumu idara ya Mnyika kwenye mitandao ilihali ulikuwa kiongozi tena mwenye haiba ya kipekee kwenye CHAMA?

Ahsante sana Mwl. wangu ila hayo ni maoni na mtazamo wangu kama mwana CHADEMA mwaminifu na pia mwanafunzi wako.
 
haswaaa mwanafunzi una upeo wa kufikiri kuliko mwalimu wako.
 
Ni nani asiyejua mbinu chafu za mwalimu katika kuangamiza demokrasia nchini???Anatumua vijana vibaya kuwapandikiza na kuwashurutisha kugombea nafasi mbalimbali kwa nia ya kukihujumu chama??Anajua uwezo wa Chadema katika kupata data.Wasomi wa nchi hii wanadhalilisha heshima ya elimu la Taifa hili.For me Kitila doesnt deserve my respect as an intellectual
 
Mwalimu anaona CHADEMA sio mbadala baada ya kufukuzwa chamani. Na mashaka na elimu yake. Acha uongo K.I.T.I.L.A hakuna mbadala zaidi ya CHADEMA kwa sasa. ACT-Tanzania bado sana jipangeni wasaliti
 
Mtoa mada ww ni kilaza!Hujui upuuz unaofanywa na chadema!Tuache uhun kwenye mambo ya msing au kifaranga?Kaz yenu kukuterea upuuz wa wakubwa zenu!Namtaka mama wa kifaranga ajitokeze
 
Mkuu RUTO, umepigilia msumari wa moto na umeuanika peupe unafiki wa mwalimu wako.

Eti viongozi wa CHADEMA wanapenda anasa na magari ya kifahari kama CCM hivyo hawafai, hivi ni nani CHADEMA anayemiliki magari ya kifahari kama Zitto ambaye eti Kitila alimuona ndiye anafaa!!, nimeipenda sana hii.
 
Mtoa mada ww ni kilaza!Hujui upuuz unaofanywa na chadema!Tuache uhun kwenye mambo ya msing au kifaranga?Kaz yenu kukuterea upuuz wa wakubwa zenu!Namtaka mama wa kifaranga ajitokeze
Hakuna hoja yeyote uliyoandika hapa ndugu!!, jenga hoja tuone kama kweli una chochote kichwani, ili tuone kama wewe sio walewale mashabiki wa CCM ambao wengi wao ni watupu vichwani.
 
Nilijaribu kuweka tofaut ya uchambuzi wa kitila wa 2008 na wa 2011. Na baadae alivyovuliwa uanachama. Kitila bakia kuwa mwl na sio mwanasiasa wewe ni mchu wa madaraka na sio kiongozi
 
Mtoa mada ww ni kilaza!Hujui upuuz unaofanywa na chadema!Tuache uhun kwenye mambo ya msing au kifaranga?Kaz yenu kukuterea upuuz wa wakubwa zenu!Namtaka mama wa kifaranga ajitokeze

Sembe ni mbaya kwelikweli.Umetokea wapi wewe?.Hivi umeisoma hbr hiyo na umeelewa kweli au tukusamehe tu haujitambui?
 
kitila ni janga lingine...tuliongezee pale zito alipoishia...
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom