Kitila Mkumbo: Jinsi Profesa Mathew Luhanga alivyoniingiza katika taaluma

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,797
11,959
Kitila Mkumbo

Siku ya Jumamosi tarehe 20 Februari 1999 imebaki kuwa rejea katika maisha yangu. Hii ni siku ambayo Profesa Mathew Luhanga, wakati huo akiwa Makamu Mkuu wa Chuo (VC) Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), aliniita ofisini kwake asubuhi majira ya saa tatu. Hii ilikuwa ni baada ya mimi kumaliza muda wangu wa uongozi wa Jumuiya ya Wanafunzi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, maarufu kama DARUSO, kufuatia uchaguzi wa uongozi mpya uliofanyika siku ya Jumatano tarehe 17 Februari 1999.

Baada ya kumsalimia na kunikaribisha ofisini kwake, na baada ya kuwa nimeshaketi, aliniambia kuwa ameniita kunieleza jambo moja tu, na ninamnukuu kadri ninavyokumbuka maneno yake kwa kuwa hayajawahi kutoka masikioni mwangu: “wewe ni principled, usiache kuwa principled, utafika mbali sana”. Tuliongea naye kwa muda wa nusu hivi na tukaagana akinieleza kuwa alikuwa anaelekea Zanzibar. Tuliagana na Profesa Luhanga akinitakia kila la heri katika masomo na maisha yajayo baada ya kumaliza vizuri muda wangu wa uongozi.

Kwa wanaomfahamu Profesa Mathew Luhanga watakubaliana nami kwamba kuitwa naye ofisini kwake kwa mtu yeyote aliyekuwa UDSM, awe mfanyakazi au mwanafunzi, wakati ule halikuwa jambo jepesi. Profesa Luhanga alikuwa amejijengea heshima kubwa sana na wakati mwingine hata kuogopwa. Hivyo, hakuna mtu ambaye angetamani awe katika mazingira ya kuitwa naye tena ofisini kwake na tena siku ya Jumamosi. Pengine kikubwa zaidi ni kupewa maneno mazuri kama yale kutoka kwa mtu muhimu sana kama Profesa Luhanga lilikuwa jambo kubwa sana kwa kijana kama mimi wakati huo nikiwa naelekea kufikisha miaka 28 na ndio kwanza najipanga kuanza maisha baada ya chuo. Nilijisikia fahari sana. Maneno yale yamebaki kuwa mwongozo muhimu katika maisha yangu binafsi, kitaaluma na sasa katika siasa.

Matukio mawili makubwa yalimfanya Profesa Luhanga anione nipo principled. Tukio la kwanza ni Mwaka 1998. Profesa Luhanga, akiwa VC wa UDSM, aliitisha mkutano na wanafunzi wote kuelezea maendeleo ya programu ya mabadiliko na maboresho ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, maarufu wakati ule kama Institutional Transformation Programme (ITP) iliyokuwa inasimamiwa na Profesa Tolly Mbwete (Mungu aendelea kumrehemu). Programu hii ililenga, pamoja na mambo mengine, kuongeza idadi ya wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Kwa kiasi kikubwa wanafunzi tulikuwa hatuungi mkono programu hii kwa kuwa ilikuwa inasababisha msongamano mkubwa sana madarasani na sehemu zingine muhimu za huduma. Hata hivyo, uongozi wa chuo ulikuwa unakataa kwamba hakuna msongamano wowote. Kama kawaida yake, Profesa Luhanga akawa anatupa changamoto kwamba wanafunzi tulete ushahidi wa kisayansi kama kweli kulikuwa na msongamano madarasani.

Kufuatia changamoto ambayo Profesa Luhanga alitupa mara kwa mara kuhusu ushahidi wa kuwepo msongamano madarasani niliamua kujipa homework. Katika wiki moja ya Februari 1999 niliandaa diary nikawa ninarekodi madarasa yote yaliyokuwa yamejaza wanafunzi kuliko uwezo wake. Nilianzia vyumba vya semina vilivyopo eneo la majengo ya Sayansi ya Jamii, nikaaenda majengo ya mihadhara ya ATA na ATB, mihadhara ya sayansi, Kitivo cha Sheria na nikamalizia na majengo ya mihadhara ya Kitivo cha Uhandisi, wakati huo maarufu kama FOE. Nilifanya kazi hii kwa wiki nzima na nikakusanya taarifa kuhusu idadi ya wanafunzi ukilinganisha na viti na meza zilizokuwepo. Kila darasa nilirekodi vizuri idadi ya wanafunzi, idadi ya viti, somo gani na mwalimu gani alikuwa anafundisha.

Siku ya Jumamosi ya tarehe 7 Februari 1998 ilikuwa ndiyo siku ya mkutano kati ya VC na wanafunzi wote uliofanyika katika ukumbi maarufu wa Nkrumah. Nilikuwa nimejiandaa kikamilifu kushiriki katika mkutano huu nikiwa na ‘nondo’ zangu kikamilifu kabisa. Wanafunzi wengi walichangia lakini bila ‘data’ na Profesa Luhanga, kama kawaida yake ukiongea bila data, aliwabamiza hasa huku akiwebeza kwa hoja zao nyepesi. Bahati yangu nikapata nafasi ya kuongea. Niliposimama nilijitambulisha na kuanza kueleza jinsi ambavyo ITP ilikuwa imeleta shida na ilikuwa inaharibu kabisa sifa ya UDSM. Nikamwaga data hatua kwa hatua nikitaja darasa moja baada ya lingine, muda, somo na mwalimu aliyekuwa anafundisha.

Wanafunzi walishangilia san sana, Nkrumah nzima ikalipuka kwa shangwe kubwa sana. Kilichoshangaza wanafunzi wengi ni pale Profesa Luhanga aliposimama na kusifia sana mchango wangu, akisema huo ndio usomi anaotarajia kutoka kwa mwanafunzi wa Mlimani. Baada ya hapo hakuchukua muda mrefu akafunga mkutano, akiahidi kwenda kuzifanyia kazi changamoto zilizoibuliwa, hasa za upungufu wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia. Hata hivyo, alisisitiza kuwa wasingeacha programu ya ITP kwa sababu ya changamoto bali wataendelea kuitekeleza na huku wakitatua changamoto hizo hatua kwa hatua.

Tukio la pili linahusu ziara ya Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kufuatia taarifa za ujio wa Rais Mkapa chuoni tarehe 16 Februari 1999 Profesa Luhanga aliniita ofisini kwake tarehe 11 Februari 1999 kwa malengo mawili. Mosi, kunipa taarifa kuhusu ujio wa Rais Mkapa kama kiongozi wa wanafunzi. Pili, kunitaka niwasilishe kwake majina ya wanafunzi ambao wangeuliza maswali siku hiyo na maswali ambayo wangeuliza ili wayawasilishe kwa Rais kwa ajili ya maandalizi. Nilimshukuru kwa taarifa lakini nilikataa wazo lake la kuwasilisha majina ya wanafunzi na maswali watakayouliza. Nikamshauri kuwa maswali yaje tu naturally pale pale ukumbini baada ya Rais kuhutubia.

Hatukukubaliana na tukaachana bila kuelewana kuhusu jambo hili. Aliendelea kunitafuta wiki nzima akisisitiza niwasilishe majina ya wanafunzi na maswali yao. Nami niliendelea kung’ang’ania msimamo wangu..

Hadi siku ya ziara ya Rais Mkapa, Jumanne tarehe 16 Februari 1999, hapakuwa na majina wala maswali kutokana kwa wanafunzi. Hatimaye majira ya mchana saa nane Rais Mkapa aliwasili chuoni na kulakiwa na viongozi wa chuo, nikiwemo mimi kama Rais wa DARUSO. Tukaingia ukumbi wa mikutano wa Baraza la Chuo (Council Chamber) kumpa Rais Mkapa briefing kabla hajaelekea ukumbi wa Nkrumah. Katika briefing yake Prof. Luhanga akashauri kuwa kungekuwa na kipindi cha maswali na majibu ambacho kwa ushauri wake ilikuwa ni kwamba Rais angekiongoza mwenyewe na atakapoona inatosha atamaliza mkutano.

Rais alikubaliana naye na tukaelekea Nkrumah. Rais Mkapa alitoa hotuba nzuri sana na wanafunzi wakamshangilia sana, pamoja na kwamba hatukuridhishwa na maelezo yake kwamba kipaumbele chake kikubwa kilikuwa ni uchumi na sio elimu kama ambavyo sisi wanafunzi tungependa iwe. Ilipofika kipindi cha maswali na majibu Rais Mkapa alijibu kwa umahiri mkubwa.
Baadaye nilipokutana naye Profesa Luhanga alicheka sana akiniambia kuwa mawazo yangu kuhusu wanafunzi kuwasilisha maswali yalikuwa sahihi, na kisha akanitania akisema kuwa ‘au ulikuwa unawasiliana naye’!!

Itaendelea Jumatatu ya tarehe 20 Septemba 2021.

Sehemu ya Pili soma;

Nasikia Mkumbo ni mtu wa system tangia zamani. Nani anaweza kukanusha? Isijekuwa alikuwa anamchora VC
 
Hivi ni Mimi sijui maana ya kuwa principled au kuna kitu kilibadilika tokea miaka hiyo?
 
Aaaaaaaa principled wapi wakati Mkumbo ni kigeugeu tu tangu akiwa Rais wa DARUSO sisi tunakumbuka jinsi alivyokuwa anawauza wanafunzi inapofikia issue ya mgomo. Hakuna kwamba alikuwa principled or what!!!
 
Itaendelea Jumatatu ya tarehe 20 Septemba 2021.
Kwenye hii mada inayoonekana itakuwa na mwendelezo, namtahadharisha Mh. Waziri arejee hotuba ya mwisho ya Mama siku alipokuwa anawaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni.

Nashauri pia Mh. Waziri ajikite zaidi kwenye mambo mapana ya Nchi ya kutuletea maendeleo sisi watanzania maskini, badala ya yeye naye kuanza kutuletea humu series za miaka ya 1999 ambazo haziwasaidii chochote watanzania.

Tuseme kwa mfano, mimi Makanyaga nilete series humu; halafu na Mh. Waziri naye tena awe na series humu jukwaani?

Nini sasa itakuwa tofauti kati ya Makanyaga na kiongozi mkubwa huyu wa Nchi ambaye amepewa majukumu mazito kwa ajili ya kuwakwamua watanzaina waliokwama, tena katika kipindi hiki ambacho muda siyo mrefu wamempoteza kiongozi mwingine mkubwa wa nchi?

Naanza kupata picha kuwa huko mbele ya safari, kuna chances kubwa sana za watu kuja kuanza kumlaumu Mama na kwa mapungufu ambayo ni yao wenyewe
 
Kaka Kitila hebu nyoosha maelezo. Wewe ulibebwa na TISS kwa kiwango kikubwa. Hebu niambie, kwa uwezo wako na ufaulu wako kabla ya chuo, ulikuwa wapi hadi ukaanza chuo na 25years?. Anyway, nakutania tu kaka yangu
 
Nadhani tungebaki kwenye hoja iliyo mezani kwa kile Prof. Kitila Mkumbo katabainisha alisifiwa na VC wa UDSM Prof. Luhanga kuwa alikuwa principled, na kwa maelezo yake aligoma kuchukuwa wazo la Prof. Luhanga la kutafuta vijana ili wapeleke maswali na IKULU itafute majibu.

Well, kuwa principled ni law of relativity.
Bila shaka Kitila ni kiongozi kwa vitendo na mwendelezo record ambayo ameionesha kwa kupewa majukumu toka akiwa Daruso, Makamu mkiti UDASA, Mkiti UDASA, kuwa Dean wa kitivo cha Elimu DUCE, kuwa kamati kuu CDM, kuwa katibu mkuu na sasa Waziri;

Suala la TISS au vinginevyo, kwa kuwa ile ni kazi na lazima iwe na Watanzania wanaotakiwa kuifanya kwa maslahi ya taifa, kama yupo huko au vinginevyo bado haliondoi uwezo ambao kauonesha kwa kupanda kwa mtiririko unao-onekana.

Kitila Mkumbo ni mzuri wa kujenga hoja (a very good debater with facts) na hiyo sifa ya kiongozi; sio lazima tutakubalia nae kwa yote aliyofanya akiwa DARUSO, UDASA, CDM, ACT, Katibu Mkuu (W) Maji na sasa Waziri wa Viwanda.

Tuna vijana ndani ya CCM wanasifiwa kama presidential materials, ila ukiwaweka jukwaani huoni wana hoja zenye mashiko; bila shaka wamepanda kwa merits za kifamilia based mzee wake alikuwa "big shot" na sio kwa merits za kuonesha uongozi kwa kusimamia maamuzi unayofanya kwa wakati huo kwa maslahi ya wengi.

Tusubiri sehemu ya pili na bila shaka itakuwa na mambo ya kujifunza kwa kukubaliana nae au kutokubaliana nae.

Kila la heri Prof. Kitila kutumegea sehemu ya yaliyopita ambayo yamechangia kwa namna moja ya nyingine leo kutishirikisha.

Freddie
 
Kitila Mkumbo

Siku ya Jumamosi tarehe 20 Februari 1999 imebaki kuwa rejea katika maisha yangu. Hii ni siku ambayo Profesa Mathew Luhanga, wakati huo akiwa Makamu Mkuu wa Chuo (VC) Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), aliniita ofisini kwake asubuhi majira ya saa tatu. Hii ilikuwa ni baada ya mimi kumaliza muda wangu wa uongozi wa Jumuiya ya Wanafunzi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, maarufu kama DARUSO, kufuatia uchaguzi wa uongozi mpya uliofanyika siku ya Jumatano tarehe 17 Februari 1999.

Baada ya kumsalimia na kunikaribisha ofisini kwake, na baada ya kuwa nimeshaketi, aliniambia kuwa ameniita kunieleza jambo moja tu, na ninamnukuu kadri ninavyokumbuka maneno yake kwa kuwa hayajawahi kutoka masikioni mwangu: “wewe ni principled, usiache kuwa principled, utafika mbali sana”. Tuliongea naye kwa muda wa nusu hivi na tukaagana akinieleza kuwa alikuwa anaelekea Zanzibar. Tuliagana na Profesa Luhanga akinitakia kila la heri katika masomo na maisha yajayo baada ya kumaliza vizuri muda wangu wa uongozi.

Kwa wanaomfahamu Profesa Mathew Luhanga watakubaliana nami kwamba kuitwa naye ofisini kwake kwa mtu yeyote aliyekuwa UDSM, awe mfanyakazi au mwanafunzi, wakati ule halikuwa jambo jepesi. Profesa Luhanga alikuwa amejijengea heshima kubwa sana na wakati mwingine hata kuogopwa. Hivyo, hakuna mtu ambaye angetamani awe katika mazingira ya kuitwa naye tena ofisini kwake na tena siku ya Jumamosi. Pengine kikubwa zaidi ni kupewa maneno mazuri kama yale kutoka kwa mtu muhimu sana kama Profesa Luhanga lilikuwa jambo kubwa sana kwa kijana kama mimi wakati huo nikiwa naelekea kufikisha miaka 28 na ndio kwanza najipanga kuanza maisha baada ya chuo. Nilijisikia fahari sana. Maneno yale yamebaki kuwa mwongozo muhimu katika maisha yangu binafsi, kitaaluma na sasa katika siasa.

Matukio mawili makubwa yalimfanya Profesa Luhanga anione nipo principled. Tukio la kwanza ni Mwaka 1998. Profesa Luhanga, akiwa VC wa UDSM, aliitisha mkutano na wanafunzi wote kuelezea maendeleo ya programu ya mabadiliko na maboresho ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, maarufu wakati ule kama Institutional Transformation Programme (ITP) iliyokuwa inasimamiwa na Profesa Tolly Mbwete (Mungu aendelea kumrehemu). Programu hii ililenga, pamoja na mambo mengine, kuongeza idadi ya wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Kwa kiasi kikubwa wanafunzi tulikuwa hatuungi mkono programu hii kwa kuwa ilikuwa inasababisha msongamano mkubwa sana madarasani na sehemu zingine muhimu za huduma. Hata hivyo, uongozi wa chuo ulikuwa unakataa kwamba hakuna msongamano wowote. Kama kawaida yake, Profesa Luhanga akawa anatupa changamoto kwamba wanafunzi tulete ushahidi wa kisayansi kama kweli kulikuwa na msongamano madarasani.

Kufuatia changamoto ambayo Profesa Luhanga alitupa mara kwa mara kuhusu ushahidi wa kuwepo msongamano madarasani niliamua kujipa homework. Katika wiki moja ya Februari 1999 niliandaa diary nikawa ninarekodi madarasa yote yaliyokuwa yamejaza wanafunzi kuliko uwezo wake. Nilianzia vyumba vya semina vilivyopo eneo la majengo ya Sayansi ya Jamii, nikaaenda majengo ya mihadhara ya ATA na ATB, mihadhara ya sayansi, Kitivo cha Sheria na nikamalizia na majengo ya mihadhara ya Kitivo cha Uhandisi, wakati huo maarufu kama FOE. Nilifanya kazi hii kwa wiki nzima na nikakusanya taarifa kuhusu idadi ya wanafunzi ukilinganisha na viti na meza zilizokuwepo. Kila darasa nilirekodi vizuri idadi ya wanafunzi, idadi ya viti, somo gani na mwalimu gani alikuwa anafundisha.

Siku ya Jumamosi ya tarehe 7 Februari 1998 ilikuwa ndiyo siku ya mkutano kati ya VC na wanafunzi wote uliofanyika katika ukumbi maarufu wa Nkrumah. Nilikuwa nimejiandaa kikamilifu kushiriki katika mkutano huu nikiwa na ‘nondo’ zangu kikamilifu kabisa. Wanafunzi wengi walichangia lakini bila ‘data’ na Profesa Luhanga, kama kawaida yake ukiongea bila data, aliwabamiza hasa huku akiwebeza kwa hoja zao nyepesi. Bahati yangu nikapata nafasi ya kuongea. Niliposimama nilijitambulisha na kuanza kueleza jinsi ambavyo ITP ilikuwa imeleta shida na ilikuwa inaharibu kabisa sifa ya UDSM. Nikamwaga data hatua kwa hatua nikitaja darasa moja baada ya lingine, muda, somo na mwalimu aliyekuwa anafundisha.

Wanafunzi walishangilia san sana, Nkrumah nzima ikalipuka kwa shangwe kubwa sana. Kilichoshangaza wanafunzi wengi ni pale Profesa Luhanga aliposimama na kusifia sana mchango wangu, akisema huo ndio usomi anaotarajia kutoka kwa mwanafunzi wa Mlimani. Baada ya hapo hakuchukua muda mrefu akafunga mkutano, akiahidi kwenda kuzifanyia kazi changamoto zilizoibuliwa, hasa za upungufu wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia. Hata hivyo, alisisitiza kuwa wasingeacha programu ya ITP kwa sababu ya changamoto bali wataendelea kuitekeleza na huku wakitatua changamoto hizo hatua kwa hatua.

Tukio la pili linahusu ziara ya Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kufuatia taarifa za ujio wa Rais Mkapa chuoni tarehe 16 Februari 1999 Profesa Luhanga aliniita ofisini kwake tarehe 11 Februari 1999 kwa malengo mawili. Mosi, kunipa taarifa kuhusu ujio wa Rais Mkapa kama kiongozi wa wanafunzi. Pili, kunitaka niwasilishe kwake majina ya wanafunzi ambao wangeuliza maswali siku hiyo na maswali ambayo wangeuliza ili wayawasilishe kwa Rais kwa ajili ya maandalizi. Nilimshukuru kwa taarifa lakini nilikataa wazo lake la kuwasilisha majina ya wanafunzi na maswali watakayouliza. Nikamshauri kuwa maswali yaje tu naturally pale pale ukumbini baada ya Rais kuhutubia.

Hatukukubaliana na tukaachana bila kuelewana kuhusu jambo hili. Aliendelea kunitafuta wiki nzima akisisitiza niwasilishe majina ya wanafunzi na maswali yao. Nami niliendelea kung’ang’ania msimamo wangu..

Hadi siku ya ziara ya Rais Mkapa, Jumanne tarehe 16 Februari 1999, hapakuwa na majina wala maswali kutokana kwa wanafunzi. Hatimaye majira ya mchana saa nane Rais Mkapa aliwasili chuoni na kulakiwa na viongozi wa chuo, nikiwemo mimi kama Rais wa DARUSO. Tukaingia ukumbi wa mikutano wa Baraza la Chuo (Council Chamber) kumpa Rais Mkapa briefing kabla hajaelekea ukumbi wa Nkrumah. Katika briefing yake Prof. Luhanga akashauri kuwa kungekuwa na kipindi cha maswali na majibu ambacho kwa ushauri wake ilikuwa ni kwamba Rais angekiongoza mwenyewe na atakapoona inatosha atamaliza mkutano.

Rais alikubaliana naye na tukaelekea Nkrumah. Rais Mkapa alitoa hotuba nzuri sana na wanafunzi wakamshangilia sana, pamoja na kwamba hatukuridhishwa na maelezo yake kwamba kipaumbele chake kikubwa kilikuwa ni uchumi na sio elimu kama ambavyo sisi wanafunzi tungependa iwe. Ilipofika kipindi cha maswali na majibu Rais Mkapa alijibu kwa umahiri mkubwa.
Baadaye nilipokutana naye Profesa Luhanga alicheka sana akiniambia kuwa mawazo yangu kuhusu wanafunzi kuwasilisha maswali yalikuwa sahihi, na kisha akanitania akisema kuwa ‘au ulikuwa unawasiliana naye’!!

Itaendelea Jumatatu ya tarehe 20 Septemba 2021.

Sehemu ya Pili soma;

Prof Kitila itendee haki wizara ya biashara. Hizi hadithi za kusifiana zimekuwa nyingi. Yes, pengine uko principled. Hilo linatusaidia nini watanzania? We lack the actions that turn around even the dire situations into some big stuff. Usomi wetu uwe wa vitendo. Sisi kina Yakhe ndio tutuje kuwasifia badala ya kujisifia wenyewe
 
Mambo ya chuo kikuu hayalisaidii taifa wafanyabiashara wanataka uwepo wa sera nzuri za biashara, acha masihala
Angalau kwa sasa hivi kuna muda wa kutosha na hivyo sioni tatizo lolote kama tukiendelea tena na series yetu hii
 
Maisha bhana ! kwahiyo Kitilla ndio basi tena , baada ya kuzindua tela la Trekta pale sabasaba ndio shughuli imeisha , anasubiri kumaliza miaka yake mitatu kwenye ubunge wa mchongo , Dah !
 
Back
Top Bottom