Kiti Security Council, hatukusimama na ndugu zetu?

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,823
35,828
Kenya mara nyingi imejinasibu kwa maneno na vitendo kuwa ni ndugu zetu.

Rais Kenyatta ameutamka u ndugu huo mara kadhaa ikiwamo katika sekeseke la mipaka yetu inayoendelea kutatizika na virusi vya Corona.

Pamoja na matamko, rais Kenyatta alirejesha marundo ya pesa na dhahabu yaliyokuwa yamekamatiwa Kenya. Akimtuma waziri wake mwana mama ambaye mzee baba alikiri kuwa alikuwa mrembo kweli kweli.

Kumbe pamoja na yote tuliamua kumtosa vilivyo ndugu yetu huyu alipokuwa anatuomba uungwaji mkono kwenye jitihada zake za uwakilishi kule UNSC?

Kenyans React After Neighbors: Tanzania, Uganda and Ethiopia Vote Against Kenya in the UNSC Election

Kwamba kumbe hata huko kumtosa kwetu bado hakukusaidia kitu?

Ama kweli tumedhamiria. Kwani kwa kura yetu hii tumethibitisha wazi wazi kuwa damu yaweza kuwa nyepesi kuliko maji!
 
Ngoja nisubiri maoni ya 'wazalendo' nione.

Hao wenye kudhani kuwa ni peke yao wenye hati miliki ya uzalendo? Wasiotambua kuwa fimbo ya mbali haiui nyoka?

Hao ndiyo waliotufikisha hapa tulipo leo. Hazipo tena zama zile ambazo sisi tulikuwa machampioni wa siasa za kimataifa.

Ngoja tuone labda tunampango kabambe wa kuelekeza malori yetu Djibouti.
 
Back
Top Bottom