SoC01 Kiti kizito wanachokalia wale wachache tunaowapa ruhusa ya kukaa juu yake

Stories of Change - 2021 Competition

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,625

Siyo hiki tunachokalia wengi, ni kile kizito wanachokalia wale wachache tunaowapa ruhusa ya kukaa juu yake. Kiti kinakuja na furushi zito, kinakutaka uwe tayari kuvuja damu na jasho, usimame imara na uendelee kutembea hata kama kuna mwiba kwenye kisigino. Unatakiwa uwakazie macho wanaokuangalia na uchape mwendo uhakikishe unawafikisha salama. Siyo wengine wawe na rangi ya njano wanang'aa na kupendeza wakati wengine wana rangi nyeusi hata kuonekana hawaonekani.

Viti vyetu hapa uwanjani siyo kama vya wale kule vimetengenezwa na chuma hata ukipiga teke unaumia wewe. Vya kwetu vimenakishiwa kwa mbao, sio kwamba havipo imara hapana ni kwamba fundi wetu anahitaji kuongenza manuva kidogo siku tukiifikia chuma basi kitakua imara kuliko vya kule.

Viti hivi vimejaa miba mingi, usipokua jasiri utaishia mlangoni urudi ulipotoka pasi na kutia mguu ndani. Kukaa hapa inabidi uwe na ule mkasi wenye makali wa kukata miba hii ili ukikaa miba isikuchome. Ni miba hii ndyio ipo shingoni mwetu kufanya tupumue kwa tabu. Aliyekalia kiti ana kibarua cha kutafuta mzizi wa fitina na “kuufyekelea” mbali ili tupate kupitisha chakula vizuri kooni.​

Dhamana.jpg

Mchoro, Dhamana 2021.
Ukipewa ufunguo wa kukalia kiti hapa uwanjani kwetu ujue “wananzengo” wana matarajio makubwa sana kwako. Matumatuaini yetu ni kua ukiwa katika kiti utautoa mwimba wa tako ili tuweze kukaa na kutoa mwiba uliokua mguuni. Tunategemea utapunguza visiki ili tukiwa tunatembea kuelekea shambani tupunguze na tuache kabisa kujikwaa.

Ukikalia kiti ufahamu upo vitani. Hakutakua na segere huko ushinde na godoro lako kutwa kucheza mziki na chereko kama wafulani wakimtoa kigori. Inabidi ujiandae siyo kwa mitutu na mapanga bali busara, akili, uthubutu na ujasiri. Ukiwa hapo inabidi uwe mzani, sio unga uwe kilo moja kushindana na kilo kumi ya mawe, usikenue sana ukasahau kuficha meno waja hawachelewi kukushika sharubu kuangalia kama ni zako au ukivuta zinavyofoka tu! Ni jukumu lako ukipewa nafasi ya kukalia pale kuhakikisha kila kete unayosogeza ni kwaajili ya ushindi wetu.

Sio kwamba nakutisha ukatishe safari yako kabla hata mwendo hujauanza, lakini kama huoni kule kuna rangi ipi utapanga vipi kuvikabili visiki na miwani yako imejaa saruji unachoona ni mwanga tuu unaopiga kwenye mashavu yako?! Ukivua miwani ukungu umetanda, turushe jiwe gizani litabahatisha huko mbele kwa mbele kwani si ndio wengi wamefanikisha?! Ilisikika sauti ikivuma, asiyejulikana!

Wakipewa uaridi miba hawaioni. Kwanza ina kazi gani wakati macho yao yamevutwa na rangi nzuri na pua zao zimezibwa na harufu ya kuvutia, masikio na vingine havina kazi, vyenyewe ni kufuata macho na pua vinavyoelekeza. Hapa ni kula kuku kwa mrija ponda raha uzee waja.

Kuna vinyonga wameona haya ndiyo makazi yao. Leo akiwa wa kijani, kesho mwekundu kesho kutwa wa zambarau. Kila rangi ina ngoma yake, mziki ukiisha ujue yametimia giza limeingia mambo yameisha. Ni kama furushi la mihogo umefungia kwenye kabati la panya, ukija kutahamaki njaa inakuzomea. Nani alaumiwe wakati tunajua kuna panya lakini hatufugi paka wala hatuweki dawa?!​

Kinyonga ndani ya suti.jpg

Mchoro, Kinyonga ndani ya suti 2020.
Hivi kwani mwenye shibe anamjua mwenye njaa?! Au ndio anakula zaidi mpaka ashindwe kuhema?! Anapumzika kidogo apate hewa ili aongeze kingine. Uchu, umejaza vitu tele lakini kuna vingine vipo chini kuna nafasi hapo kichwani nikijaribu kuviweka vitakaa tuu. Kwanini wabebe wengine wakati kwangu kuna upenyo hapa?!

Ni wivu tuu umewajaa, kwani hata wangekua mimi si wangefanya hivyovyo?! Acha "niwekeze" kesho watoto wangu watatumia. Aliyekua na usongo wa kuzikamata kuwa kama yeye siku nyavu zikitikiswa unafikiri mtoto wa nyoka atageuka kua kondoo? Au tubaki na matumaini huenda yeye si kama wao?!

Huu ndio mwimbo wao tumezoea kuusikia. Mistari tumeikariri vya kutosha, tukisikia mdundo tuu tunajua fulani amefika tunacheza na kumpa ushirikiano wote. Cha ajabu ni kwamba tunataka tubadilishe nyimbo lakini kila ukiwekwa sisi ndio wa kwanza kucheza, tena tunalisakata hasa tunauona mwimbo ni mpya. Mpaka mwimbo uje uishe tunasahau na kiu yetu ya kutaka ladha na mirindimo mingine yenye kutia vionjo na kutuburudisha zaidi!​

Uchu.jpg

Mchoro, Uchu 2020.
Kwani unafikiri hawaoni kwamba maji yako shingoni tunapumulia juu juu kusubiri uokozi kabla hatujazama?! Unafikiri hawasikii kelele na vilio vya maumivu zinazonyesha kila leo kama mvua za masika zisizokua na vikomo?! Wanaona na wanasikia tena wanajitapa mkono wangu ni mrefu popote ulipo tupo huwezi kujificha ukakimbia kumulikwa na darubini yetu kali. Wako “busy” kusema nyama ya ng'ombe tumeichoka sasa tunaka "ostyers”.

Wao ni kupishanisha mikono huku wamekenua, kupitisha msumeno wenye makali upande mmoja na wao wameshika kuliko butu na pamefunikwa na kitambaa. Wanasema uchafu uko huko nje wao wamezungukwa na uzio vipindupindu mpate nyie wenyewe. Wamesahau anga letu ni hili hili hutaona uchafu lakini harufu utaipata. Nzi nae hayuko nyuma atahakikisha ripoti inakufikia. Wametulia kama maji mtungini wakidhani hili haliwahusu kwamba linachagua tuu sie "kajamba nani" wanasahau tumekalia gogo moja tukianza kuzama sisi wao wapo nyuma yetu.​

Tufaa lililo oza.jpg

Mchoro, Tofaa lililo oza 2020.
Ni sisi ndio tunaenda kununua nyanya mbovu na kupikia mchuzi alafu tutegemee chakula kiwe kitamu. Mizoga yetu huku haitupwi jalalani. Mizoga yetu tunaiweka vizuri na kuipamba ikapambika. Tena ni sisi ndio tunahakikisha ipo imara wakati wote utadhani labda siku itabadilika na kuwa nyama safi.

Mizoga yetu inakua maridadi tena ina nguvu inaweza ikakuchapa kibao hata usifanye kitu zaidi ya kuugulia maumivu chini chini kwani ukitoa sauti utaamsha popo na wengine washindwe kulala. Sio kwamba tumefungiwa mbuzi kwenye gunia la hasha tumepewa huku tunaona tukiwa macho mchana kweupe. Tumekubali wenyewe kubeba mzoga mgongoni huku tukishangilia.

Tusifanye mambo kama kichwani kumejaa hewa. Anayekalia kiti anatoka uwanjani kwetu tunapocheza mpira wote. Kabla hatujampa nafasi ya kukaa kwenye kiti huwa tunajiuliza uchezaji wake uwanjani ukoje? Mechi zilizizopita je, hakugeuza uwanja ukawa ulingo kama chura alichofanya juzi kidole kimoja kikavunjwa wakati ndio kwanza mechi ilikua inaanza?! Rekodi zake kwa misimu iliyopita ilikuaje? Tukimpa kiti mwenye rekodi nzuri tuna uhakika wa kushinda mechi kwa nafasi kubwa na tukimpa mwenye rekodi mbaya sina haja ya kumalizia sababu majibu tayari tunayo, tupange vikosi vyetu vizuri tusije kufanya bora liende tukaja kushtuka kitumbua kimeshaingia mchanga.

Ukiwa kama kondoo unaefata mwongozo wa mchungaji inabidi usikae kimya tuu kama unanyolewa hata ukiona mchungaji anataka kutumbukia kwenye shimo usiseme. Mchungaji bila kondoo hana cha kuongoza, lazima uwe imara mchungaji afanye kazi yake ipasavyo maana yupo hapo kwasababu wewe upo. Lakin hapa kwetu uwanjani kondoo inabidi uufyate hata kama unaona kuna mbwa mwitu wanakuja kwa nyuma.

Ukisema wewe unamfundisha kazi. kama unataka kuchinjwa watu wale nyama wewe jifanye umepewa kipaza sauti. Hapa uwanjani kwetu ukitaka upate mambo yapenye kwenye anga basi katafute kichwa cha simba ujivike upate na miguu ya kuku watu wasijue wewe ni nani, hapa “mwananzengo” utapiga kelele utakavyo na hivi hawajui wewe ni nani utawapa joto ya jiwe washinde wakijibu mapigo yanayotoa pumzi kwa mkosa hewa bila wenyewe kujua. Sheria ya hapa uwanjani kwetu ni kua mjinga upate kuliona jua, jifanye moto umwagiwe maji uzimike.​

Madaraka.jpg

Mchoro, Madaraka 2020.
Sio kwamba hatupendi anga letu jekundu libadilike na kua bluu inayovutia iliyochanganyika na nyeupe, au kwamba hatutaki kuacha kula makombo kila siku na tupate chakula bora chenye afya na kila kirutubisho. Tunapenda na sisi tuwe kama wale ama tuwazidi kabisa lakini nyoyo zetu zimejaa kiza, hewa inayotuzunguka imejaa unga tumevaa miwani hatuoni tumelala usingizi. Kiti tunakiona kimeanguka lakini nani ataamka na kukiota akakiweka vizuri?

Nani atathubutu kumfunga paka kengele kama panya wote wametawanyika hakuna anaemsikiliza mwenzake. Dereva wetu anakwenda kasi mpaka gari inaanza kupaa, abiria tumekaa kimya kuomba “upako” ushuke apunguze mwendo. Lini tutaamka tumpe kiti dereva hodari anaeendesha kwa ustadi na weledi bila kuziba masikio kuchambua akasikia mwimbo, maana hata saa mbovu hua inatoa majira sawa mara moja vipi ukiwa na saa nzima? Lini tutapata dereva atufikishe salama mwendo wake akiumaliza akijua abiria wake hawavuti ile hewa inayofanya bendera kua punguani kugeuka kule mluzi unapoita?!

Hapa uwanjani kwetu kuna watu tofauti tofauti na wengi ni sisi ambao waliopewa dhamana kukalia viti tunawaona kwa manati. Watu ambao uwezo wetu ni kukaa chini ukapigwa na vumbi kwasababu hata kuvuta kigoda kukalia ni majanga michuzi imeweka uadui na sisi. Ni matarajio yetu kila mtu mwenye kuomba kukalia kiti hatatufanya tujute kutia vyema kwenye kisanduku.

Usiende kua kioo kinachoonyesha kiza tunaokuangalia tukaingia shimoni, bali ukawe dira yenye mwangaza muda wa mwingine kukalia kiti ukifika tusianze kutafuta kwa tochi wa kumpa fimbo aendeleze mbio. Walau hivi vilio vilivyopo hapa uanjani vikome na kila mtu aanze kutabasamu. Wenzangu na sisi tupumzike kukaa kwenye vumbi tusogee kwenye mikeka, ile sabuni iliyokua ikitaabishwa na vumbi ikawe ziada ya kutumika kesho.

Tukipata mgeni akija akirimiwe vizuri ale ashibe na apumzike, uchovu ukiisha jembe mkononi tunaenda wote kulima shambani. Ujio wake sio wa kula kulala tuu akiondoka amenenepa hata kutembea hawezi, kama anavyofaidi kukaa kwetu na sisi tupate jasho lake kule shambani kwetu. Ni ndoto yetu ukipata nafasi kukaa kwenye kiti utakaa kwaajili yetu, na kila mtu uanjani atapiga konde kufuani akijivunia kwamba aliekalia kiti kweli ni tunu.​
 
View attachment 1972871

View attachment 1873977

View attachment 1873978
Mchoro, Uchu 2020.
Kwani unafikiri hawaoni kwamba maji yako shingoni tunapumulia juu juu kusubiri uokozi kabla hatujazama?! Unafikiri hawasikii kelele na vilio vya maumivu zinazonyesha kila leo kama mvua za masika zisizokua na vikomo?! Wanaona na wanasikia tena wanajitapa mkono wangu ni mrefu popote ulipo tupo huwezi kujificha ukakimbia kumulikwa na darubini yetu kali. Wako “busy” kusema nyama ya ng'ombe tumeichoka sasa tunaka "ostyers”.

Wao ni kupishanisha mikono huku wamekenua, kupitisha msumeno wenye makali upande mmoja na wao wameshika kuliko butu na pamefunikwa na kitambaa. Wanasema uchafu uko huko nje wao wamezungukwa na uzio vipindupindu mpate nyie wenyewe. Wamesahau anga letu ni hili hili hutaona uchafu lakini harufu utaipata. Nzi nae hayuko nyuma atahakikisha ripoti inakufikia. Wametulia kama maji mtungini wakidhani hili haliwahusu kwamba linachagua tuu sie "kajamba nani" wanasahau tumekalia gogo moja tukianza kuzama sisi wao wapo nyuma yetu.​

View attachment 1873983
Mchoro, Tofaa lililo oza 2020.
Ni sisi ndio tunaenda kununua nyanya mbovu na kupikia mchuzi alafu tutegemee chakula kiwe kitamu. Mizoga yetu huku haitupwi jalalani. Mizoga yetu tunaiweka vizuri na kuipamba ikapambika. Tena ni sisi ndio tunahakikisha ipo imara wakati wote utadhani labda siku itabadilika na kuwa nyama safi.

Mizoga yetu inakua maridadi tena ina nguvu inaweza ikakuchapa kibao hata usifanye kitu zaidi ya kuugulia maumivu chini chini kwani ukitoa sauti utaamsha popo na wengine washindwe kulala. Sio kwamba tumefungiwa mbuzi kwenye gunia la hasha tumepewa huku tunaona tukiwa macho mchana kweupe. Tumekubali wenyewe kubeba mzoga mgongoni huku tukishangilia.

Tusifanye mambo kama kichwani kumejaa hewa. Anayekalia kiti anatoka uwanjani kwetu tunapocheza mpira wote. Kabla hatujampa nafasi ya kukaa kwenye kiti huwa tunajiuliza uchezaji wake uwanjani ukoje? Mechi zilizizopita je, hakugeuza uwanja ukawa ulingo kama chura alichofanya juzi kidole kimoja kikavunjwa wakati ndio kwanza mechi ilikua inaanza?! Rekodi zake kwa misimu iliyopita ilikuaje? Tukimpa kiti mwenye rekodi nzuri tuna uhakika wa kushinda mechi kwa nafasi kubwa na tukimpa mwenye rekodi mbaya sina haja ya kumalizia sababu majibu tayari tunayo, tupange vikosi vyetu vizuri tusije kufanya bora liende tukaja kushtuka kitumbua kimeshaingia mchanga.

Ukiwa kama kondoo unaefata mwongozo wa mchungaji inabidi usikae kimya tuu kama unanyolewa hata ukiona mchungaji anataka kutumbukia kwenye shimo usiseme. Mchungaji bila kondoo hana cha kuongoza, lazima uwe imara mchungaji afanye kazi yake ipasavyo maana yupo hapo kwasababu wewe upo. Lakin hapa kwetu uwanjani kondoo inabidi uufyate hata kama unaona kuna mbwa mwitu wanakuja kwa nyuma.

Ukisema wewe unamfundisha kazi. kama unataka kuchinjwa watu wale nyama wewe jifanye umepewa kipaza sauti. Hapa uwanjani kwetu ukitaka upate mambo yapenye kwenye anga basi katafute kichwa cha simba ujivike upate na miguu ya kuku watu wasijue wewe ni nani, hapa “mwananzengo” utapiga kelele utakavyo na hivi hawajui wewe ni nani utawapa joto ya jiwe washinde wakijibu mapigo yanayotoa pumzi kwa mkosa hewa bila wenyewe kujua. Sheria ya hapa uwanjani kwetu ni kua mjinga upate kuliona jua, jifanye moto umwagiwe maji uzimike.​

View attachment 1873987
Mchoro, Madaraka 2020.
Sio kwamba hatupendi anga letu jekundu libadilike na kua bluu inayovutia iliyochanganyika na nyeupe, au kwamba hatutaki kuacha kula makombo kila siku na tupate chakula bora chenye afya na kila kirutubisho. Tunapenda na sisi tuwe kama wale ama tuwazidi kabisa lakini nyoyo zetu zimejaa kiza, hewa inayotuzunguka imejaa unga tumevaa miwani hatuoni tumelala usingizi. Kiti tunakiona kimeanguka lakini nani ataamka na kukiota akakiweka vizuri?

Nani atathubutu kumfunga paka kengele kama panya wote wametawanyika hakuna anaemsikiliza mwenzake. Dereva wetu anakwenda kasi mpaka gari inaanza kupaa, abiria tumekaa kimya kuomba “upako” ushuke apunguze mwendo. Lini tutaamka tumpe kiti dereva hodari anaeendesha kwa ustadi na weledi bila kuziba masikio kuchambua akasikia mwimbo, maana hata saa mbovu hua inatoa majira sawa mara moja vipi ukiwa na saa nzima? Lini tutapata dereva atufikishe salama mwendo wake akiumaliza akijua abiria wake hawavuti ile hewa inayofanya bendera kua punguani kugeuka kule mluzi unapoita?!

Hapa uwanjani kwetu kuna watu tofauti tofauti na wengi ni sisi ambao waliopewa dhamana kukalia viti tunawaona kwa manati. Watu ambao uwezo wetu ni kukaa chini ukapigwa na vumbi kwasababu hata kuvuta kigoda kukalia ni majanga michuzi imeweka uadui na sisi. Ni matarajio yetu kila mtu mwenye kuomba kukalia kiti hatatufanya tujute kutia vyema kwenye kisanduku.

Usiende kua kioo kinachoonyesha kiza tunaokuangalia tukaingia shimoni, bali ukawe dira yenye mwangaza muda wa mwingine kukalia kiti ukifika tusianze kutafuta kwa tochi wa kumpa fimbo aendeleze mbio. Walau hivi vilio vilivyopo hapa uanjani vikome na kila mtu aanze kutabasamu. Wenzangu na sisi tupumzike kukaa kwenye vumbi tusogee kwenye mikeka, ile sabuni iliyokua ikitaabishwa na vumbi ikawe ziada ya kutumika kesho.

Tukipata mgeni akija akirimiwe vizuri ale ashibe na apumzike, uchovu ukiisha jembe mkononi tunaenda wote kulima shambani. Ujio wake sio wa kula kulala tuu akiondoka amenenepa hata kutembea hawezi, kama anavyofaidi kukaa kwetu na sisi tupate jasho lake kule shambani kwetu. Ni ndoto yetu ukipata nafasi kukaa kwenye kiti utakaa kwaajili yetu, na kila mtu uanjani atapiga konde kufuani akijivunia kwamba aliekalia kiti kweli ni tunu.​
Mungu NISAMEHE kwa uzembe wangu, sikuiona post Bora namna hii kwa wakati muafaka.
 
Back
Top Bottom