Kiti cha spika kimegeuza bunge letu kuwa butu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kiti cha spika kimegeuza bunge letu kuwa butu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Byendangwero, Jul 11, 2012.

 1. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #1
  Jul 11, 2012
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Leo mbunge wa Kigoma mh. Kafulila alitoa rai bungeni ya kwamba anao ushahidi wa kutosha wa kuthihirisha ya kwamba kushindwa kwa serikali katika kesi ya Richmond kulitokana na njama zilizosukwa ndani ya serikali yenyewe. Kufuatia kauli hiyo, ilitolewa hoja ikimtaka spika/mwenyekiti aliyekuwa anaoongoza kikao hicho amtake mh. Kafulila awasilishe ushahidi huo hapo bungeni ili hufanyiwe kazi. Katika hali hisiyo ya kawaida wanasheria mkuu wa serikali, ambaye kimsingi ndiye ambaye alikuwa anatuhumiwa kuhusika kwenye njama hizo aliamka na kupinga kutolewa kwa ushahidi huo ambao bila shaka ungeli muumbua yeye mwenyewe. mwenyekiti wa kikao hicho naye kwa upande wake akaungana na mwanasheria mkuu kuzuia ushahidi huo husitolewe mbele ya bunge. Kwa maoni yangu, katiba ya yetu inamtaka yeyote yule mwenye kuwa na ushahidi wa vitendo vya uhalifu kutoa ushahidi huo kwa mamlaka husika; kama hivyo ndivyo, kiti cha spika kimevunja katiba kwa kukubali kutumika kuficha ukweli wa mambo.
   
Loading...