Kithuku Umesema Kweli, lakini.....

Mchumia juani

Member
Jan 28, 2008
27
13
Umesema mambo ya kweli mifumo yetu iliyopo haitoi nafasi ya kuuelimisha umma wa watanzania ili kujikinga na maradhi, bahati mbaya hata sisi wahudumu wa afya ambao tunaelimishwa kwa fedha za hawahawa watanzania hatujengewi misingi ya kutoa elimu ya afya kwa umma nitakupa sababu chache tu kwa nini elimu ya afya kwa umma hapa tanzania haijafanikiwa.

Kwanza kabisa ni ukosefu wa Vipaumbele,yaani kama patient information ingepewa kipaumbele magonjwa kama kisukari, pressure, Ukimwi, Magonjwa ya zinaa n.k yasingekuwa kwa kiwango cha sasa kwani mengi ya hayo hutokana na mpangilio mbovu wa maisha au vakula tunavyokula pasipo kujua madhara yake kwa kuwa tu hatufahamu. Hii ni kutokana na Sera mbovu ya afya ambayo haitoi kipaumbele katika Kinga.Juhudi ziko ktk tiba ambayo hao waheshimiwa huko wizarani wanapata chao kirahisi.

Pili Msururu wa wagonjwa kama Daktari nawaona Wagonjwa zaidi ya 50 kwa siku kuanzia saa 2 hadi saa 10 sasa unategemea nitaanza kjuhubiri elimu ya afya wakati kuna foleni ya Wagonjwa huko nje ambao lazima wote ni waone?

Tatu Wagonjwa watu wenyewe hawana mwamko wa kutafuta na kusoma habari za afya, Nilikuwa naandika makala ktk gazeti fulani watu waliokuwa wakiuliza maswali walitaka zaidi Tiba kuliko uelewa kuhusu ugonjwa walionao ,hapo tayari kuna tatizo.

Nne tumewahi kuna kituo cha Elimu ya Afya kwa umma pale Chuo kikuu cha Afya Muhimbili,Shangaa nani anakitumia?

Tano Ni watu wenye Mawazo batili kama yako(samahani kwa kutumia neno Batili) Ukifanya Sammury ktk vitu vya Msingi ktk afya unapoteza maana, Kila taarifa ya afya ni muhimu kwa hiyo kama watu hawana muda wa kusoma maelezo ya afya kuna kuelimika hapo? Kuona kwamba kila jambo la afya ni la msingi ndio maana wanaosomea Udaktari wanazeekea vyuoni.

Kwa leo ni hayo machache tu Kithuku lakini usimlaumu Kaisa, shule aliyotoa hapo juu ni pana na kama ukiamua kusoma utajifunza mengi.
 
Ni kweli, wengi hatusomi/kufuatilia elim ya afya zaidi ya kutaka kujua kutibu, laiti elimu hii ingekuwa imeeleweka vizuri, wengi tungepona na magonjwa mengi.
 
Back
Top Bottom