Kitengo cha ukaguzi wa dhahabu chazinduliwa - Kweli kitakuwa na Msaada?

Kuntakinte

JF-Expert Member
May 26, 2007
701
33
Kitengo cha ukaguzi wa dhahabu chazinduliwa

Basil Msongo

HabariLeo; Sunday,September 30, 2007 @00:02

WAZIRI wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi amesema, serikali ipo katika mchakato wa kudhibiti biashara ya madini hivyo kitengo kipya cha ukaguzi wa dhahabu kitaiwezesha serikali kufahamu kiwango na thamani ya dhahabu inayopelekwa kuuzwa nje ya nchi.

Aliyasema hayo Dar es Salaam jana muda mfupi kabla ya kuzindua kitengo hicho kitakachokagua dhahabu inayozalishwa katika migodi mikubwa na pia kukagua biashara ya madini katika migodi mikubwa.

Karamagi alisema anaamini kuwa wafanyakazi wazalendo katika kitengo hicho wataweza kufanya kazi hiyo na kwamba, serikali itawasaidia kutimiza wajibu huo ikiwa ni pamoja na kuwapatia vitendea kazi na ujuzi.

“Shughuli kubwa inayofanyika katika maabara hii ni kufanya uchunguzi wa sampuli za madini kujua wingi na thamani halisi ya madini yanayosafirishwa nje kwa ajili ya kuuzwa pamoja na maandalizi ya taarifa mbalimbali kuhusiana na uzalishaji na biashara ya dhahabu kutoka migodi mikubwa,” alisema.

Kwa mujibu wa Waziri Karamagi kitengo hicho kitafanya kazi kwa miaka miwili wakati wizara inakamilisha mchakato wa kuunda chombo cha ukaguzi wa uzalishaji wa madini kwa kuanzia na dhahabu na hatimaye madini yote ikiwa ni pamoja na yanayozalishwa na wazalishaji wadogo.

Mkuu wa Kitengo hicho, Idan Nyalusi alisema wataalamu waliopo hapo wanaweza kuifanya kazi hiyo na kwamba, miongoni mwa kazi zitakazofanyika ni kuchunguza mabaki ya dhahabu kubaini kuwapo au kutokuwapo kwa madini mengine.

Nyalusi alisema kitengo hicho pia kitachunguza dhahabu iliyoyeyushwa ambayo kwa kawaida huwa na uzito wa kilogramu 20 hadi 25 kufahamu kiasi cha dhahabu na madini mengine yanayokuwa yamechanganyika na dhahabu hiyo.

Aliwaeleza waandishi wa habari kuwa watakuwa wakipokea sampuli 180 hadi 240 za mchanga wa dhahabu kila mwezi na kwamba, muda wa uchunguzi unategemea aina uhalisia wa dhahabu inayochunguzwa na kwamba kitengo hicho kitaiwezesha serikali kudhibiti ubora wa dhahabu inayosafirishwa nje ya nchi.

Kitengo hicho kipo chini ya Wizara ya Nishati na Madini na kinafanya kazi hiyo ikiwa ni matokeo ya kusimamishwa mkataba kati ya serikali na kampuni ya Alex Stewart (Assayers) Government Business Corporation (ASAGBC).

Serikali ipo katika utekelezaji wa mikakati ya kuongeza mapato yanayotokana na madini na imekuwa ikichukua hatua kadhaa ikiwa ni pamoja na kuipitia upya mikataba ya madini kubaini udhaifu uliopo kwenye mikataba hiyo.
 
Kuna kitengo cha uchambuzi wa Almasi huko UK kinaitwa TANSORT, nacho ni butu tu, hakuna cha maana sana kinachofanywa toka kianzishwe...sina hakika hiki cha dhahabu kitafanikiwaje kama mikataba ya makampuni ya madini yenyewe mikataba yao ni uchovu mtupu
 
Back
Top Bottom