Wahusika kama mnapitia humu okeoni watu Musoma vijijini, ninapoandika bandiko hili katika kijiji kimoja tu cha Chitare kuna vifo vipya vitano (misiba mitano) mheshimiwa mbunge Pro Mhongo wapiga kura wako wanateketea kwa kipindupindu,
Elimu ya kutosha kwa wanavijiji kuhusu kipindupindu hakuna, huduma ya kwanza hakuna, Kambi kwa ajili ya kulaza wagonjwa hakuna, Mortual hakuna, maiti za waliokufa kwa kipindupindu ziko ndani zikisubiri watu wa Halmshauri kutoka Musoma mjini kuja kuzika, haki ya hawa wazazi na ndugu zetu kupata huduma za afya iko wapi?
Ajabu hili nijimbo ambalo hata kabla ya kutengwa lilikuwa wilaya kamili inayojitegemea lakini watendaji wote ofisi zao ziko Musoma mjini. Leo imetengwa na kuwa na majimbo mawili Butihama na Musoma Vijijini. Hii ni wilaya ambayo haina hospitali ya wilaya, haina kituo cha afya cha kueleweka, ukiacha kile cha pale Mrangi ambacho kipo tangu Tanzania ilipopata uhuru na kimechoka.
Hili jimbo pekee ambalo lina diwani mmoja tu wa ukawa, Serikali sikivu ya awamu ya tano wasaidieni Wajita kipindupindu kinawamaliza.