Kitengo cha emergency Tanesco ni sooo!!

Wakuligo

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
259
105
Umeme umekatika line moja, tumewaita wamekuja na wanataka ganji, kwa kua hatuna basi mama mmoja kawatoa na kidogo alafu wamemhamishia kwenye line yenye umeme na wamesepa! Hiv hawa jamaa wa emergency lazima walipwe wanapokuja kufanya kazi? Hawa si wana overtime na mishahara?

Wamenivuruga.
 
Pole sana mdau - Bila hela hawafanyi hata kama wamekupa ripot numbar, ila ninawasifu kwa lugha nzuri na wepesi wa kupokea simu na hata kwenda eneo la tukio lkn matengenezo ni mpaka uingize mkono mfukoni! Sisi tuliripoti tatizo la umeme hapo kariakoo lln hawakuja kabisa kwa wiki mbili hadi tulipochanga hela tukawalipa.... Wanafanya wanavyojosikia -shamba la Bibi-
 
utafukiri umeme wanatupa bure,mgoja atawale raisi kwenye akili awabinafsishe waulize wenzao TTCL wanalia sasa hata hawaeleweki
 
hao jamaa ni majanga kuna mmoja ni mpangaji mwenzangu wao ni full viroba na michepuko hasa zamu za usiku sa unadhan bila ganji watapata wapi hela za anasa!ila si sawa wala haki, au watangaze kabisa kuwa kuna malipo na risiti watoe tena za efd ili tra wawakate na kodi
 
Hawa jamaa haana Maana kabisa kwangu wanaunguza vifaa vyangu kila siku na umeme wao mdogo (low Voltage). Tumeripoti mara kibao mwaka sasa hawajafika. Help desk yao ni ovyo kabisa hasa iliyopo kwenye website yao.Sijui watabadilika lini hawa
 
Mkuu wale jamaa hatari kuliko hata polisi hawajui kua mshahara wao unatoka hapo unaweza ukawaita km unakitu wala awakujali
 
Wangeweka wazi kwamba hii huduma inalipiwa...umeme wakate wao alafu kurudisha tunalipia sisi...this country bwana!!
 
Jamani si tanesco tu kila idara na wizara huduma bila mshiko hakuna. Sijui utaenda sehemu ipi hapa nchini upate hudima bila kutoa chochote.
 
Umeme umekatika line moja, tumewaita wamekuja na wanataka ganji, kwa kua hatuna basi mama mmoja kawatoa na kidogo alafu wamemhamishia kwenye line yenye umeme na wamesepa! Hiv hawa jamaa wa emergency lazima walipwe wanapokuja kufanya kazi? Hawa si wana overtime na mishahara? Wamenivuruga#%#!!

Siku ingine piga picha gari lao na jitahidi wakuone unapiga picha ...then ripoti vizuri hapa jamiiforum...
 
urgency kwao haipo, kama traffic vile akishaona ajali tayari hiyo ni dili, hawana tofauti kabisa. sijui hiyo BRN yao wanayozungumzia kama just kufurahisha watu kua nao wamo
 
watu walipewa kitengo wakajigamba wanalifumua shirika ili liendane na kasi ya maendeleo kumbe ni nguvu ya Juice!
 
Back
Top Bottom