Kitengo cha dawa asilia Muhimbili chagundua tiba ya Kisukari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kitengo cha dawa asilia Muhimbili chagundua tiba ya Kisukari

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Aug 15, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 15, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Kitengo cha Utafiti wa Dawa Asilia cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, kimegundua dawa za asilia za aina tatu za kutibu magonjwa ya kisukari na kibofu cha mkojo.

  Kitengo hicho ambacho kazi yake ni utafiti wa dawa asilia, kimefanikiwa kugundua dawa hizo katika kipindi cha miaka 38 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1974.

  Dawa zilizogundulika na kuonyesha mafanikio makubwa ni aina ya Morizela zilizopo kwenye mfumo wa juisi ambazo moja ina sukari na nyingine haina ambazo zimeonyesha mafanikio makubwa katika tiba ya kisukari.
  Dawa nyingine ni aina ya Prucan ambayo hutibu wagonjwa wenye matatizo ya kutopata haja ndogo, magonjwa ambayo huwapata zaidi wanaume wazee.

  Akizungumza na gazeti hili, Kaimu Mkurugenzi wa kitengo hicho, Dk. Ester Innocent, alisema pamoja na kwamba dawa hizo zimeshaanza kutumika, lakini bado hazijaingia sokoni kwa vile bado ziko kwenye Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA).
  Alisema TFDA ikishatoa usajili wake, kitengo hicho kinaweza kuingia mikataba na wenye kampuni za kutengeneza dawa ili zizalishwe kwa wingi na kuwafikia wagonjwa wengi popote walipo.

  Alisema kwa sasa dawa hizo zinapatikana kwa uchache sana kutokana na kuzalishwa hospitalini hapo na ikishapata usajili, itapatikana kwa wingi.

  Kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi huyo, pamoja na kitengo hicho kuanza muda mrefu na hatimaye mwaka huu kutoa rasmi dawa hizo, wengi wataona imechukuwa muda mrefu lakini akasisitiza kuwa utafiti kwa kawaida huchukuwa muda mrefu.
  Dk. Innocent alisema watafiti mara nyingi ni wepesi kugundua tiba ya dawa, lakini dawa hiyo haiwezekani kutumika bila kujua madhara

  yake, hivyo wanalazimika kuanza tena utafiti wa kuyajua madhara hayo na kuyadhibiti.
  Hata hivyo alisema zipo dawa nyingi za asili zinazofanyiwa utafiti lakini ambazo utafiti wake uko karibuni kukamilika ni za aina 11 zinazotibu magonjwa mbalimbali kama malaria, pumu, tumbo, ngozi na magonjwa nyemelezi ya ukimwi.
  Alisema kitengo hicho kinakabiliwa na changamoto nyingi hasa za uhaba wa fedha na hivyo kujikuta kuchelewa kutoa matokeo ya tafiti zao kwa wakati.  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

   
 2. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #2
  Aug 15, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Karibuni hivi utaiona na A49 ya Dr. Msigwa, mbadala wa wa ARV's, bodi ya chakula na madawa Zanzibar na Mkemia mkuu Zanzibar wameshaipitisha kuwa haina madhara wala sumu.

  Tutaweka kopi humu baada ya muda wa siku si nyingi.
   
 3. U

  Ubungo JF-Expert Member

  #3
  Aug 15, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hongereni watafiti wa madawa ya asili.
   
 4. bereng

  bereng Senior Member

  #4
  Mar 6, 2013
  Joined: Feb 5, 2013
  Messages: 114
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sasa hakuna haja ya kuendelea kuteseka na maradhi kwani kuna uponyaji kupitia bidhaa ziliyotengenezwa kwa mmea wa asili (Aloe Vela) zinazotibu maradhi sugu kama vile; kisukari, shinikizo la damu, kubalance homoni na uvimbe kwa wanawake, matatizo ya ngozi, vidonda vya tumbo, kuongeza CD4 kwa haraka, pamoja na maradhi mengine mengi.
  Lakini pia kwa mtu anayetaka kutumia kama kinga ili asipate magonjwa hayo anaweza kutuona na kupata huduma. Kwanini uchague huduma zetu?. 1. Tunatoa bidhaa bora zilizotengenezwa kwa mmea wa asili zenye uthibitisho wa kimataifa unaokidhi viwango. 2. Tunakupa dhamana ya siku 60 ambapo tutakurudishia pesa yako usipopata matokeo mazuri. 3. Tunatoa ushauri namna ya kuepuka maradhi bure. 4. Tutakuletea bidhaa pindi utakapokuwa unahitaji baada ya kuwa mteja wetu utakapoona ubora wa bihaa za kampuni yetu

  KUMBUKA MALI BILA AFYA NJEMA NI KAZI BURE.
   
 5. Brightman Jr

  Brightman Jr JF-Expert Member

  #5
  Mar 7, 2013
  Joined: Mar 22, 2009
  Messages: 1,233
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Hiyo aloe vera inauzwaje? Mie niko shy nitaipata wapi huku?
   
 6. bereng

  bereng Senior Member

  #6
  Mar 7, 2013
  Joined: Feb 5, 2013
  Messages: 114
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  bei sio kubwa mdau. hapo shy unaweza kuipata, tuwasiliane ili nikuelekeze kuna mtu atakupatia hapo shy
   
 7. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #7
  Mar 7, 2013
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  Watanzania msipende kudanywa na hawa wapenda hela ambao wanageuza magonjwa ya wengine kwao biashara.
   
 8. okaoni

  okaoni JF-Expert Member

  #8
  Mar 7, 2013
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 1,197
  Likes Received: 466
  Trophy Points: 180
  acha utapeli wewe ! mshaaona TZ shamba la bibi la kuibia wagonjwa? weka kwanza certificate kutoka wizara ya afya ikionyesha dawa yako imefanyiwa analysis za kisayasi na kudhibitisha kuwa hayo maalovera yako yanatibu. wanasayasi dunia nzima wanahangaika hawajapata tiba sahihi za magonjwa hayo wewe unatangaza kienyeji tuu?Hujui hapa mtandaoni dunia nzima wanaona au unafikiri ni wajinga wajinga tuu.Nakushauri buni biashara nyingine hayo majuice ya aloevera watu wamegonga sana ya yale makampuni ya kimarekani na afrika ya kusini lakini hakuna kitu. huna jipya
   
 9. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #9
  Mar 7, 2013
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,787
  Likes Received: 1,038
  Trophy Points: 280
  mi niliposikia aloe vera nimeshapata kichefuchefu
   
 10. P

  Paul Ndatala Member

  #10
  Sep 7, 2015
  Joined: Jul 17, 2015
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  VIDONGE KWA WANAOSUMBULIWA NA KISUKARI PAMOJA NA MWILI KUFA GANZI

  Uyoga umekuwa ukitumiwa kwa miaka takribani 200 iliyopita katika kutibu magonjwa mbalimbali ya mwanadamu.

  Watu wengi hawaupendi na hawatumii uyoga mara kwa mara.
  Ndiyo maana tunazidi kushuhudia magonjwa ya ajabu ambayo yanapelekea vifo vingi sana.
  Kupitia uyoga, hasa uyoga mwekundu, magonjwa kama hayo yanaweza kutoweka kabisa endapo tu watu watachukua hatua za haraka.

  KAZI ZA DAWA ITOKANAYO NA UYOGA KATIKA MFUMO WA VIDONGE.
  1. Huukinga mwili dhidi ya virusi
  2. Hukinga ini lisipatwe na matatizo
  3. Huondoa sumu mwilini
  4. Hushusha shinikizo la juu la damu
  5. Huzibua mishipa ya damu kutokana na kuganda kwa damu
  6. Inazuia vimbe za aina zote
  7. Inazuia hali ya aleji
  8. Inazuia saratani.
  9. Husawazisha kiwango cha sukari mwilini10.Husawazisha kiwango cha vichochezi mwilini (hormones)
  10.Huzuia maambukizi ya bakteria.
  11.Ina ongeza nguvu mwilini hasa kwa wale wanaochoka sana, hasa wenye kisukari.

  Ukungu upatikanao katika uyoga una kazi nyingi sana kama ilivyotajwa hapo juu.
  Kutokana na uhaba wake timu ya wataalamu wa mimea wameweza kuuchuja vizuri na kuuweka katika mfumo wa vidonge, hivyo kuwa rahisi kwa mtu kuupata.

  Dawa hii ina vidonge 60
  Mtu atumiapo vidonge hivi huweza kutatua matatizo mengi ya kiafya, na kuongeza kinga ya mwili hasa kwa wenye kisukari na wanaougua maradhi ya ukimwi.

  Utaipata popote ukihitaji, kama utaratibu wetu ulivyo wale wa mikoani huwa tunawatumia.

  MTU YEYOTE ANAWEZA KUTUMIA VIDONGE HIVI.
  NI VYA ASILI ASILIMIA 100,%

  KWA HIYO ZINA MATOKEO MAZURI KATIKA 0758986658
   
Loading...