Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,525
- 1,522
Kila kukicha kunafunuliwa jipya kuhusu Ufisadi na kigugumizi cha Chama Twawala kushika hatamu na kuwajibika.
Butiama tumekwenda, tumefuta mwafaka, tukamhani Julius, tukaunyamazia uhujumu, tukaapiana kushikamana, tukumbushane Mei, kujipanga kula kupya.
Left and right you hear same stories of Uhujumu. Sasa kisima kingine cha pesa za umma Benki ya Posta kimevumbuliwa, lakini kila siku CCM wako kimya.
Je wako wapi wale wanaojiita CCM Safi? Kwa nini mnaendelea kulelea Uhujumu, Ufisadi, Uzembe na kukosekana na Uwajibikaji? Ikiwa mnakerwa na Udhalimu, inakuwaje mnaendelea kukumbatiana na Madhalimu?
Mama Kilango, Mwakyembe, Seleli, na wengine mliopigia baragumu Richimondi na na uhakika mnanguruma chinichini kuhusu EPA, Chenge na uhujumu mwingine. Kwa nini mnaendelea kuwa wanachama na waumini wa Chama ambacho kinakataa kujisafisha kwa dharura na kwa maendeleo kwa manufaa ya Taifa?
Je viapo vyenu vya Utii kuitii Katiba ya Tanzania vimekwenda wapi? Au ni kiapo cha kuitii CCM na maslahi yake kwanza? Mwamkiri mwamkubali na kumtumikia Shetani na mambo yake yote? Mmelewa mvinyo gani mpaka kila siku na kila saa mnaimba "Nasadiki"?
Nyerere mwasisi wa Chama Chenu alisema kuwa CCM si Mama yake, anaweza achana nacho saa yeyote ile. Je mnaogopa nini kuachana na CCM? Ni maslahi gani mnaogopa kuyapoteza kwa kuiacha CCM Solemba?
Wakulu msifikirie nawashikilia bango kina Kilango na Mwakyembe pekee, bali ni pamoja na ile sehemu ya nne ya CCM ya wale ambao waliwahi kuwa viongozi wakuu wa Chama na Serikali.
Mwinyi, Salim, Malecela, Msuya, Kawawa, Salmin, Bilali, Sozigwa, Ameir, Kificho, Kinana na Warioba, je nyie mnaoshikilia ile sehemu ya nne ya Kitenge mko wapi na wale ambao ni wafuasi wenu?
Kina Rwegasira, Mwakanjuki, Hassan Moyo, Lawrence Gama, Mang'ula na utitiri mwingine wa wanaoaminika kuwa CCM safi wako wapi? Mwandosya why hugging and hanging with the thugs? Even Jumbe, Dourado and Samata are this silent? Where are Bruno Mpangala, Hashim Mbita, Sarakikya, Ibrahim Kaduma na Sepeku?
Mnashindwaje kulitumikia Taifa na kulinda maslahi ya Taifa na Mtanzania na kuukana ufidhuli na Uchafu wa CCM kwa kutoa sauti moja ya ukali na kulazimisha zile sehemu tatu zilizobakia za Kitenge zijirudi au mjitoe kabisa CCM?
Mnakubalije pamoja na Urobo wenu kuzidiwa kete na umahiri na hizi pande tatu, Kikwete, Mkapa na Chenge ziwashinde?
Kikwete na Mtandao wake, wako wapi leo kina Lowassa,Karume, Rostam, Msabaha na wengine?
Mkapa ana nguvu gani yeye na kina Kigoda, Mramba, Sumaye, Rupia au Yona na wafuasi wao?
Mnapigwa piku hata na Chenge, Msekwa, Anna Abdallah, Karume, Nahodha, Sitta, Membe, Meghji, Nchimbi, Karamagi na Makinda?
Hivi leo wakirudi Nyerere, Karume, Wakili, Sokoine, Mnauye, Kolimba na Mzee Thabit Kombo mtawaambia nini?
CCM imegawanyika kambi nne, tatu zinalinda maslahi ya Chama na Ufisadi, kwa nini nyinyi kambi ya nne msimeguke basi mkaunda umoja wenu wa pekee na kutetea Mlalahoi?
Wikiendi njema mkiwa mnatafakari "vijisenti"!