Kitendo kilichofanywa na polisi Dodoma na Kilimanjaro hatutakivumilia tena

Zapa RadioFm

Senior Member
Feb 12, 2016
112
171
Baraza la Vijana wa Chadema ( BAVICHA) tunalaani vikali kitendo cha jeshi la Polisi kuvamia Mahafali ya CHASO mkoa wa Dodoma na Kilimanjaro kuzuia isifanyike.

Vitendo hivyo ni vya kihuni na havina ubinadamu wala havikufuata misingi ya Kidemokrasia na Utawala bora.Wakati Polisi wakifanya hivyo kwa CHADEMA huku ccm wanafanya mahafali zao na wanalindwa na jeshi la polisi,Ujinga huu sasa umefika mwisho.

Polisi wamevamia Mahafali ya vijana wetu na kuizuia kwa kuwa eti hakukuwa na kibali cha Mahafali, tumewauliza Polisi ni sheria gani inasema mtu akifanya Mahafali lazima aombe kibali cha Mahafali kwa la Polisi??

Polisi Dodoma walishindwa kujua hata wao kwanini wanazuia Mahafali,wakijichanganya eti kuna ugonjwa na mwisho wake wakasema maelekezo kutoka juu,hivi huyo alie juu ninani?,alichaguliwa nanani?? Anaishi wapi??

Polisi wamejivika majukumu yasio wahusu nakujifanya wao ni viranja wa ccm ,haisaidii kuendelea kutunyanyasa wakafikiri kuwa wanatufundisha uoga ,bali sasa wanatupa ujasiri wa kutafuta namna ya kuitafuta haki yetu ya msingi na wasitegee wakiivuruga nchi hii wataweza kuirudisha kama awali.

Nchi hii inapo kwenda ni kubaya sana,na sisi kama vijana hatutakubali kuona watu wachache wanataka kuharibu amani ya nchi kwa kukandamiza Demokrasia jambo ambalo ndio hasa litaanzisha machafuko halafu tukawanyamazia.

Tukiyaacha haya yaendelee katika nchi yetu,nikukubali zama za utumwa kurudi upya kwa njia nyingine kupitia Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na ccm kwa kutumia jeshi la Polisi ambalo muda wote limekuwa likiteleza maagizo haramu ya watawala.

Kuanzia Leo hatutakubali kupokea amri yeyote ya jeshi la Polisi yenye misingi ya kukandamiza Demokrasia ya nchi yetu kwakuwa tumepoteza imani na namna ambavyo jeshi la Polisi limekuwa likitekeleza majukumu wajibu wake kwa kutofuata utaratibu.

Tunapenda kuliambia jeshi la Polisi Kiwango cha uvumilivu kwetu kama vijana kinaelekea kufika mwisho na sasa tutaanza kuchukua hatua ya kupinga dhulumu,uonevu na ukandamizaji unaofanywa na jeshi la Polisi nchini kwa maelekezo ya Watawala.

Hatutachokaza mtu ,tutafuata utaratibu wa Kikatiba na hatutakubali kuvunja sheria ila hatutakubali kuona tena tunaendelea kunyanyaswa na jeshi la Polisi pamoja na watawala.

Mmetuzuia tusifanye mikutano tumekubali,mmetuzuia vikao vyetu vya ndani tumekubali,mmetuzuia kukaa vijiweni na wananchi wetu tumekubali sasa hata Mahafali zetu mnazuia??

Nafikiri umefika wakati wakuwaonesha Watanzania ninani anaevuruga amani ya nchi hii,hatutaa kimya tena .

Jiandaeni kutupiga,kwakuwa mna nguvu za kutupiga,jiandaeni kutufunga kwakuwa mnazo magereza za kutosha,jiandaeni kutupiga risasi na mabomu na maji ya kuwasha kwakuwa nyie ni jeshi lenye nguvu kuliko yote duniani.

Kumbukeni hakuna silaha yeyote wala jeshi lolote lililowahi kuishinda nguvu ya Umma,Polisi mnaipeleke nchi kubaya kusiko julikana.

Imetolewa June 19

BAVICHA Taifa
 
jeshi la polisi limefanya kazi nzuri sana, wananchi tunapongeza!! wakiandamana wapigwe, wavunjwe na miguu!!
 
Mkuu japo mimi inaniuma sana.. Angalia hii sheria ya Mitandao mkuu
Asante Mkuu.
Mimi siyo mwanasiasa lakini huwa sipendi mtu aonewe. Kama ukiamua kutoa haki toa kwa wote. Ukisema hutowi haki basi usitoe kwa wote. Mambo ya kubaguana kwa Itikadi za vyama vya siasa au dini au kabila siyo mazuri kabisa. Ndo maana inafikia watu tunashindwa kuzuia temperaments zetu
 
Bavicha, naomba muwe wastaarabu acheni kutumia watoto wa watu kama jukwaa lenu la kisiasa, hayo mafahali mukayafanyie kwenye bar ya mtu tena nje ya chuo tena katika muda huu wa mfungo wa mwezi mtukufu kweli? Hapana!

Mbona Lowasa kafanya shughuli yeke pale karimjee hall bila matatizo yeyote, sasa nyie huko kays hotel munataka kuwafanyia mambo gani watoto wetu? hivi mulipata ridhaa ya uongozi wa chuo kuwakusanya watoto wa watu huko danguroni? hivi mlipata ridhaa ya wazazi wao? najua mwanangu yuko chuo huko kays hotel anafanya nini tena katika mfungo wa mwezi ramadhani?

Simsubiri wamalize masomo yao muwaalike kwenye makongamano yao badala ya kuwa hadaa na vijipombe vyenu, nani asiyejua matendo ovu yanayofanywa na wanachuo wamalizapo masomo yao hizo vurugu za "LY" unataka kuniambia sumaye hazijui? huyo salum mwalim hazijui? haya nendeni na SUZA nako mkafanye mafahali simunawanachama huko pia?

Zimekuwepo tabia ya kumbi za starehe kuandaa sherehe za wanafunzi kwa lengo la kuwachukua wasichana ili wakawe vivutio vya wanaume kwenye bar zao, nani asiyejua magari ya mukesh yanavyozunguka vyuoni kukusanaya wasichana kwenda kwenye night clubs? nani asiyejua kuwa hao wasichana huingia bure kwenye hizo kumbi za starehe, nani asiyejua hayo mafahali ndio hutumika kuvalisha pete za uchumba mabinti wa watu na ndio siku za kuchana bikira zao, ifike sehemu tuheshimu utu wa mtu.
 
Acha waisome naamba eeeh,sisiemu mbele kwa mbelee.heheh hadi gladuesheni wamekaza?.huu ni woga wa aina yake.alafu tunajiitaga nchi ya demokrasia na amani,tena wasomi na phd zao wanaisifu kabisa,bora mie sjasoma lakini mungu kanijaalia utambuzi wakuyaona haya maigizo.Tanzania haina amani bali ina woga na unafiki tu.kwa haya yalojitokeza ndani ya miezi hii michache ya utawala mupya,naimani wenye akili zifanyazo kazi wataelewa ni aina gani ya watu ambao tumewapa dhamana ya kutuongoza.
 
Tayari tumeingia kwenye vurugu nadhani mkulu na asili yake ya ukaribu na Rwanda ana hamu na machafuko. Nina imani atayapata
 
Sio matamko tu wazee, watu waandaliwe.
You cant go to war against a trained and armed enemy with bare hands.
 
unaijua nguvu ya dola?? huwez kushindana na dola, mi nalipongeza jeshi la polisi kwa kuwatawanya hao wahuni wachache
Mkuu tusiwe biased. Kama Polisi wameamua kufanyakazi basi wafanye kazi kwa usawa. Kuna hatari kubwa mno viongozi wasiasa wanapogawa watu katika jamii. Mfano mdogo tumeanza kuuona zanzibar watu wanabaguana kwa sababu ya Itikadi za Vyama mpaka kwenye misiba, Nyumba za Ibada na kwenye sherehe. Mwisho wake unadhani ni nini?
Mwisho wake ni kuanza kuviziana. Huyu ni wetu yule siyo wetu piga ua. Hata Rwanda Mauwaji ya Kimbali yalitokana na ubaguzi kama huu. Ulianza kidogo kidogo baadaye ukaota mizizi. Kundi la waliobaguliwa waliposema basi inatosha wote tulishuhudia yaliyotokea. Wapinzani ni ndugu zetu, wazazi wetu, shemeji zetu, wengine wakwe zetu na rafiki zetu. Siyo kwamba hata wanaCCM walio na ndugu zao, marafiki zao, wakwe zao wanafurahi kuona haya wanayotendewa hao ndugu zao. Hiyo amani, umoja na mshikamano ambao viongozi wetu wanaimba kuilinda naona wao ndo wanaitengenezea nyufa.
 
Mkuu tusiwe biased. Kama Polisi wameamua kufanyakazi basi wafanye kazi kwa usawa. Kuna hatari kubwa mno viongozi wasiasa wanapogawa watu katika jamii. Mfano mdogo tumeanza kuuona zanzibar watu wanabaguana kwa sababu ya Itikadi za Vyama mpaka kwenye misiba, Nyumba za Ibada na kwenye sherehe. Mwisho wake unadhani ni nini?
Mwisho wake ni kuanza kuviziana. Huyu ni wetu yule siyo wetu piga ua. Hata Rwanda Mauwaji ya Kimbali yalitokana na ubaguzi kama huu. Ulianza kidogo kidogo baadaye ukaota mizizi. Kundi la waliobaguliwa waliposema basi inatosha wote tulishuhudia yaliyotokea. Wapinzani ni ndugu zetu, wazazi wetu, shemeji zetu, wengine wakwe zetu na rafiki zetu. Siyo kwamba hata wanaCCM walio na ndugu zao, marafiki zao, wakwe zao wanafurahi kuona haya wanayotendewa hao ndugu zao. Hiyo amani, umoja na mshikamano ambao viongozi wetu wanaimba kuilinda naona wao ndo wanaitengenezea nyufa.
nyie bavicha hamnaga maana, polisi wanafanya kazi yao nzuri sana na wanastahili kupongezwa kwa hili!! mikutano ya mahafali alafu kwenye hayo mnayoita mahafali MTU anaongelea uchaguzi mkuu, mara nilidhulumiwa, Mara ningetoa kauli nchi isingekalia, yaani uongouongo mwingi, eti nchi isikalike kisa katoa kauli, mbona ashasema zaidi ya Mara 10 kuwa kaibiwa kura na bado nchi inakalika!! hiyo mikutano yenu chadema haina maana, narudia tena haina maana na mkikaidi agizo la polisi MPIGWE mvunjwe na miguu!!
 
Back
Top Bottom