Kitendo hiki cha CCM yangu kuwaamini Wanasiasa kama huyu kunakidhalilisha Chama na kisirudiwe tena

Prognosticator

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
40,128
2,000
Hatimaye aliyekuwa Mbunge wa CCM Jimbo la Nachingwea, Hasani Masala ambaye hakuweza kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kutimkia ACT Wazalendo mapema leo ameongea na waandishi wa habari kuwa amerudi CCM na kuomba radhi kwa mwenyekiti wa CCM na wana CCM pamoja na viongozi wa Wilaya.

Amesema atahakikisha mbunge aliyepitishwa na CCM anapita kwa kishindo na kura za rais na madiwani zinapatikana kwa wingi.

Masala amepokelewa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Nachingwea, Rafael Saanane, amempongeza Masala kwa kuomba radhi kwa rais pamoja wanachama wa Wilaya ya Nachingwea.

Uhuru

CCM yangu wakati tunaendelea Kujihadhari sana na Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI nadhani na Virusi vya 'Kisiasa' kama hivi tuviepuke vile vile.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom