Kitendo hiki cha CCM kinafanana na kafara la kisiasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kitendo hiki cha CCM kinafanana na kafara la kisiasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mghaka, Sep 17, 2011.

 1. M

  Mghaka JF-Expert Member

  #1
  Sep 17, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 320
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ziko imani chafu miongoni mwa watu matajiri ambao hawakubahatika kupata elimu ya biashara au uongozi. Watu hawa huamini kuwa kwa njia za kishetani wanaweza kung'arisha nyota zao au kuitakasa biashara zao ili zisitawi. Katika sayansi nyota za kisiasa na biashara zinang'arishwa na ubunifu wa mwanasiasa au mfanyabiashara mwenyewe.

  Katika nguvu za giza nyota ya kisiasa au biashara wengi wanaamini kuwa hung'arishwa kwa kutumia damu ya mwanadamu tena si kila mwanadamu bali ni ndugu wa karibu na kipenzi cha muovu huyo wa kisiasa au katika biashara.


  Unampenda lakini cheo chako cha kisiasa `ni bora kuliko umpendaye na ndiyo maana unamtosa ili baadaye aje kulinda biashara yako au cheo chako. Sijui ukweli wa imani hii ya kijinga lakini watu wanasema wako watu wanafanya haya sitaki kuwa shuhuda wa upumbavu huu na kama kweli wapo watu wa namna hii hawa ndio watu wasiostahili kuishi na kufurahia uhai ambao mungu baba ametuzawadia wanadamu wote. Maana yake uhai wao unastahili kutwaliwa kwa nguvu ya umma au sheria. Bahati mbaya vitendo vyao havina ushahidi na kwa hiyo wamefanikiwa kutoroka nguvu ya sheria na umma unaowazunguka. Mabo yao hufanywa gizani na katika usiri mkubwa

  hivi karibuni tumeshuhudia ccm ikimtosa rostamu kisiasa ili ijitakase. Ilifanikiwa kumtosa lakini kumbe nia yake ya kisiasa ilikuwa kumfanya msukule wa kisiasa ili aendelee kuilinda katika nguvu za giza kupitia kivuli chake na kwa ndani tu si kujitokeza katika nguvu na uhai wake kisiasa. Mwanzoni wengi hatukuelewa dhamira ya ccm lakini baadaye tumekuja kujua kuwa hawamtaki rostamu yeye binafsi lakini nyota yake wanaitaka ili itumike kuking'arisha chama igunga. Undumilakuwili huu unatosha kulinganishwa na mtu anaeua ndugu zake na kuwafanya misukule kwa manufaa yake binafsi

  kwa kuwa wameweza kumtosa mwanawao ili waweze kujimilikisha jimbo la igunga si kazi kubwa kuitosha nchi ili wabaki madarakani. Katika tabia waliyoionyesha igunga kwa kuviringisha agenda yao ya kujitakasa na kuwatosa akina nnauye na wenzake ili wamkumbatie rostamu washinde igunga hatupaswi kuwaangalia kwa maana ya igunga tu ni lazima tuwaangalie katika upana wa dhamana tuliyowapa na ujuha huu wa siasa za majitaka na uchwara walizoziendesha kuanzia mwezi wa nne.

  Kwa kweli hii sasa inapaswa kuwa agenda ya taifa na tulizungumze katika upana wake na wananchi waione ccm kama chama kigeugeu kisichopaswa kuaminiwa kwa lolote na kinyimwe dhamana ya kuongoza. Katika siasa dhambi kubwa kuliko zopte ni kushindwa kusimamia yale unayoyaamini kwa sababu tu unataka kura. Ukihubiri kondomu weka msimamo wako hata ukialikwa roma. Kubadili agenda na itikadi kwa sababu unataka kuomba kura ni dhambi isiyosameheka milele

  ni chukizo lisilostahili kusamehaka mioyoni na machoni kwa watanzania na wanaigunga wote wakati huu na ujao

  jina la bwana lisujudiwe milele yote kwa kuwa wakweli katika nafsi zetu wakati wote iwe katika kutaka kufanikisha shida zetu au shida za watu wengine
   
 2. M

  Mthuya JF-Expert Member

  #2
  Sep 17, 2011
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 1,415
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Nduguyangu kamaulikua hujui kwenye siasa hakuna urafiki wa milele wala uadui wa milele
   
 3. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #3
  Sep 17, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  That is CCM, umesema hawafai wanapaswa kuuwawa na seal 6, na kuzikwa deep sea kama Bin Laden
   
 4. H

  HAKI bin AMANI Senior Member

  #4
  Sep 17, 2011
  Joined: Sep 5, 2011
  Messages: 156
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM bila mapacha watatu haiwezekani. Nafananisha na methali isemayo, ganda la muwa la jana chungu kaona kivuno. Sasa hivi wamechanganyikiwa wanatapatapa hawana mashiko wanalamba matapishi yao. Ukimsikia waziri aliyepewa dhamana anasema "fedha za msaada hata kama ni za shetani ni halali kuzichukua" kama alivyowahi sema Bw. Bernard Membe ni hatari. Ujue watawala wamefilisika kiasi cha kumtumaini sheitwan. Washindwe na walegee.
   
 5. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #5
  Sep 17, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hapa ndo wanaigunga wanatakiwa waambiwe ukweli huu waamue nao kukataa au kukubali kushiriki matapishi pamoja na ccm. Wanajua kabisa kuwa wanadanganywa lakini kwa sababu ya pesa na uelewa mdogo wa mambo watakuwa wagumu kibadilika maana wameshafika mahali pa kuukana utu wao kwa sababu ya shida nyingi.

  Tunaweza kuwaombea ili Mungu awafunguwe ufahamu wao na macho yao waone mateso yao na waseme
  TUMENYONYWA VYA KUTOSHA SASA BASI.
   
 6. Kabakabana

  Kabakabana JF-Expert Member

  #6
  Sep 17, 2011
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 5,559
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  wana mda mchache sana ts time they disappear from our life.Tanzania bila magamba inawezekana
   
 7. d

  dotto JF-Expert Member

  #7
  Sep 17, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  ccm haina uongozi imara. hivi Mwl. Nyerere angefanya haya ya akina Kikwete na Mkapa kuhusu RA?
   
Loading...