Kitendo cha Yanga kumleta Koffi Olomide ni ujanja wa kujaza uwanja kwenye siku ya Wananchi, hawana watu wala nini

Ikiwa kama tunataka kupima uwezo wa timu kujaza mashabiki kwenye kinachoitwa Yanga Day , basi ni vema tuache kujidanganya kutumia ujanja ujanja kama huu ambao yanga wanautumia.

Kitendo cha kumleta Mopao uwanjani hii inamaanisha hata mimi Mwanasimba lazima nihudhurie tu , sisi wengine ni wapenzi halisi wa Rhumba na mimi ni mpenzi wa kutupwa wa Koffi , sasa kwenye nchi ambayo uchumi umekufa kiasi cha mapromota kushindwa kuleta mwanamuziki yeyote kwa miaka 8 , halafu inatokea nafasi ya kucheza Rhumba la Koffi hatuwezi kuacha.

Kwahiyo hata mkiona siku yenu watu wamejaa sana mjue sisi wengine tutakuja kusakata Rhumba tu , msije mkadhani MNA WATU , ukweli ni kwamba hamna lolote , kama mnabisha muondoeni Koffi Olomide muwekeni Konde Boy halafu muone nani atakuja.

View attachment 1906357
Ndo maana ata sisi makoro koro fc tulimleta diamond asaidie kujaza uwanja msimu uliopita,,na tukamtaka ataje jina la bwana mwamed kwenye nyimbo kumpaisha na kunogesha tamasha hivyo ata hawa mabingwa wa kihistoria kumleta koffi ni jambo la kawaida na nyie mnaweza kumfata saida karoli akawasaidia kuwajaza watu uwanjani
 
Back
Top Bottom